YOUTUBE PLAYLIST

Friday, August 12, 2022

USIKU WA MAVOKALI KILA IJUMAA NA TWANGA PEPETA


Siku maalumu ya Mavokali ni leo Ijumaa pale  Mawasiliano Park Ubungo, jirani kabisa na jengo yalipo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania yaani TCRA.
Kuanzia saa mbili kamili usiku na Twanga Pepeta Kisima cha Burudani.


Tuesday, August 9, 2022

MWANAMUZIKI SHAABAN KIBENGO KABUMBI -CADET BONGOMAN HATUNAE TENA




Marehemu SHAABAN KIBENGO- CADET BONGOMAN


Mwanamuziki Shaaban Kibengo  Kabumbi, aliyewahi kuwa muimbaji wa bendi kadhaa nchini kama Akudo Sound, Bicco Stars, na African Revolutions. Amefariki dunia alfajiri ya leo. Shaaban alikuwa maarufu kwa jina la Cadet Bongoman, jina  alilolipata enzi alipokuwa dansa miaka ya 90 kutokana na umahiri wake wa kumuiga vizuri Kanda Bongoman.
Katika miaka ya karibuni alikuwa akipiga muziki na kundi la Mambosasa Mini Band katika hoteli mbalimbali na kwa muda mrefu katika hoteli ya Concord Kariakoo. 

Mazishi ya Shaaban yalitegemewa kufanyika Kimara Mwisho leo 9 Agosti 2022


 

Shaaban kulia akiwa na marehemu Papa Wemba katika moja ya maonyesho



MUNGU AMLAZE PEMA SHAABAN KIBENGO 

Sunday, July 31, 2022

ASANTE SANA DR KEDMOND MAPANA, KATIBU MTENDAJI MPYA WA BASATA


 HAKUNA RAHA KUBWA KAMA PALE UNAPOONA SERIKALI INAZUNGUMZA NDOTO ZA WASANII, SERIKALI INAPOZUNGUZA MIPANGO YA KUENDELEZA SANAA KWA MUDA MREFU NA KWA KUTENGENEZA MFUMO UTAKAOFAIDISHA WASANII NCHI NZIMA.  HAKIKA MWANGA UNAONEKANA WA KUONDOKANA NA ZILE SHUGHULI ZA KUTENGENEZA MATUKIO AMBAYO NI YA SIKU MOJA NA KWA WASANII WACHACHE MAARUFU.

Friday, July 29, 2022

BASATA INAPOKEA KAZI ZA KUHAMASISHA SENSA


 

TWANGA PEPETA KISIMA CHA BURUDANI KILA IJUMAA MAWASILIANO PARK

 

Vokali kali toka kwa Charles Baba Kingunge, akiwa na wakali wenzake wa Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani, kila Ijumaa huwa zinasikika Mawasiliano Park Ubungo jirani kabisa na jengo yalipo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania yaani TCRA kuanzia saa mbili kamili usiku. Unakosaje?



 


SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...