Marehemu SHAABAN KIBENGO- CADET BONGOMAN |
Mwanamuziki Shaaban Kibengo Kabumbi, aliyewahi kuwa muimbaji wa bendi kadhaa nchini kama Akudo Sound, Bicco Stars, na African Revolutions. Amefariki dunia alfajiri ya leo. Shaaban alikuwa maarufu kwa jina la Cadet Bongoman, jina alilolipata enzi alipokuwa dansa miaka ya 90 kutokana na umahiri wake wa kumuiga vizuri Kanda Bongoman.
Katika miaka ya karibuni alikuwa akipiga muziki na kundi la Mambosasa Mini Band katika hoteli mbalimbali na kwa muda mrefu katika hoteli ya Concord Kariakoo.
Mazishi ya Shaaban yalitegemewa kufanyika Kimara Mwisho leo 9 Agosti 2022
Shaaban kulia akiwa na marehemu Papa Wemba katika moja ya maonyesho |
MUNGU AMLAZE PEMA SHAABAN KIBENGO
🙏🏾Pumzika kwa amani Shaaban Kibengo.Amen.
ReplyDelete