YOUTUBE PLAYLIST

Saturday, April 17, 2010

Orchestra Fuka Fuka

Kuna mdau aliomba azione picha za bendi ya Fuka fuka,hapa ni picha zilizotangaza ujio wa Bendi hii ambayo ilitokana na Orchestra Kamale ya Kongo. Haikukaa Tanzania muda mrefu lakini ndio iliyomleta mwanamuziki Tchimanga Assossa ambaye ameamua kuishi Tanzania toka wakati huo

Thursday, April 15, 2010

Swali la Leo

Mwanamuziki gani huyu aliyeshika gitaa?

Tancut almasi Orchestra enzi hizo


Tancut Almasi Orchestra, hapa wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma. Bahati mbaya Ray, Hashim, Kalala, Zacharia wameshatangulia mbele ya haki. Kuna utata kuhusu alipo Mohamed Shaweji. Uniform zinapendeza
(Kutoka kushoto.. Ray Mlangwa, Bakari Buhero, Hashim Kasanga, Mohamed Shaweji, John Kitime, Kalala Mbwebwe, Kawelee mutimwana,Abdul Mngatwa, Kibambe Ramadhan, Zacharia daniel, Akuliake 'King Maluu' Salehe)

Wanamuziki kutoka Kongo II


Katika makala za mwanzo mwazo za blog hii, kuna wadau walitaja nyimbo za bendi ya Nova Success ambazo walizipenda. Nimeona kuwakumbusha zaidi niiweke picha hapa ya Bendi hiyo iliyokuwa ikipiga Top Life Bar Kinondoni. Baadhi ya nyimbo zake ni Maeliza ,Sizeline na Cherie Jamila. Kiongozi wao aliitwa Papa Micky. Mara ya mwisho kusikia kuhusu bendi hii ni pale walipoamua kuelekea Msumbiji

Vijana Jazz ilikotokea





Mwaka 1971 Umoja wa Vijana wa TANU uliamua kuanzisha Bendi na kumpa jukumu hilo mwanamuziki John Ondolo Chacha. Ili kutaengeneza bendi, Marehemu Mzee Ondolo aliweza kuwashawishi vijana wa bendi ya Zezemba wakajiunga nae lakini hawakukaa nae muda mrefu kwani walikuwa ni waajiriwa wa kiwanda cha nguo cha Urafiki, hivyo akalazimika kujenga tena Bendi na kwenda hadi Bagamoyo alipoikuta bendi ya Kizibo na akapata wapigaji kumi. 1972 wapigaji wengine tena wakaacha bendi, hivyo akalazimika kutafuta wengine na kikubwa ni kuwa alimpata mpiga solo Hassani Dalali ambaye aliweza kuwatafuta wenzie. Bendi ilipelekwa JKT mwaka 1973, wakati huu tayari ilishampata mtunzi na mwimbaji kutoka TK Limpopo ya Juma Kilaza, kwa jina Hemed Maneti, na baada ya muda kidogo iliweza kumpata Hamis Fadhili kutoka Jamhuri Jazz.
1974 walienda Nairobi na kurekodi nyimbo ambazo ziliaweka msingi wa bendi hiyo. Baadhi ya nyimbo hizo ni Magdalena, Niliruka Ukuta. Mtindo wa bendi wakati huo ulikuwa Kokakoka Balaa

Belesa Kakere

Salehe Kakere, maarufu kama Belesa Kakere, hapa akitangaza kuhamia Orchestra Bima Lee. Hebu soma maelezo katika habari yake unapata picha kamili ya mwanamuziki huyu na kazi zake na historia yake kwa ufupi

Wednesday, April 14, 2010

Vyombo vya habari

Katika kusoma magazeti ya zamani,(nitazitoa baadhi ya makala hapa), imeniijia kuwa tunatatizo kubwa la uandishi na utoaji wa habari za shughuli za muziki. Makala za muziki za siku hizi, nyingi ni kuhusu nani kapagawisha wapi au mcheza show gani alikaa vibaya au ana uhusiano na nani. Kimsingi ni kama vile taarifa kuhusu muziki ni gossips zinazoendelea katika uwanda wa wanamuziki. Hakuna taarifa ya taaluma katika muziki huo. Unaweza kupata taarifa nzuri kuhusu Beyonce lakini ukakosa taarifa kuhusu Anna Mwaole ambaye yuko jijini Dar es Salaam. hili liko hata kwenye vituo vya redio vya wilayani, ambako huko nako watangazaji wengi wanaiga kuanzia uongeaji, mpangilio wa vipindi, maadili na kadhalika kutoka redio maarufu za Dar es Salaam.
Huko wilayani nako wanadai hawana taarifa za wasanii wa hapo wilayani kwa kuwa wasanii hawaleti taarifa zao, lakini mtu huyohuyo atakaa masaa kadhaa kwenye internet akitafuta taarifa zote kuhusu msanii wa nje. Napata taabu kujua aina ya mafunzo wanayopata waandishi katika vyuo vya uandishi siku hizi. Na tena nakumbuka kuwa wandishi wengi wa zamani hawakupitia vyuo kama vilivyo siku hizi kwanini hakuna ubora wa uandishi sasa? Kwanini tunakosa ufanisi zaidi siku hizi ? au ni mimi ndio mwenye kuona kuna tatizo ambalo halipo? katika makala nitakazoziposti hapa ambazo ni za miaka ya sabini naona kuna maelezo ambayo nayakosa katika uandishi wa siku hizi.

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...