YOUTUBE PLAYLIST
Thursday, April 15, 2010
Tancut almasi Orchestra enzi hizo
Tancut Almasi Orchestra, hapa wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma. Bahati mbaya Ray, Hashim, Kalala, Zacharia wameshatangulia mbele ya haki. Kuna utata kuhusu alipo Mohamed Shaweji. Uniform zinapendeza
(Kutoka kushoto.. Ray Mlangwa, Bakari Buhero, Hashim Kasanga, Mohamed Shaweji, John Kitime, Kalala Mbwebwe, Kawelee mutimwana,Abdul Mngatwa, Kibambe Ramadhan, Zacharia daniel, Akuliake 'King Maluu' Salehe)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Bwana Kitime hapo umenifurahisha. Kama wiki mbili tatu zilizopita niliwahi kuchangangia hoja hapa na nikazungumzia TANCUT na uniform zao zilivyopendeza. Wakati huo mkipiga uwanja wa Jamhuri. siku za jumapili mnapokuwa safarini Dodoma. Nilikuwa nasoma Mazengo lakini nilikuwa natoroka na kuja kuwaoneni hadi mwisho wa onyesho.
ReplyDeleteNami swali langu siku zote lilikuwa yuko wapi Mohammed Shaweji? Maana sauti yake ilikuwa burudani sana.
Mkuu,
ReplyDeleteNimekutumia ujumbe kuhusu Hashim naomba usiuchapishe nilichanganya habari. Kuna Hashim na Kulwa walikuwa blowers waliotokea kwa Father Canute. Kulwa alipita Vijana na baadaye nilimuona Ndekule. Hashim alikwenda Magereza Kiwira na baadaye alikuja Dar akazunguka bendi kadhaa. Akapotea baada ya blowing section kupotea katika bendi zetu za kisasa.
Mkuu,
ReplyDeleteAsante sana kwa kuliafiki ombi langu na kwa maelezo kuhusu Kulwa Milonge.
Marehemu Father Canute alizalisha blowers wengi sana. Katika Product zake yupo mpuliza trumpet ambaye alienda mpaka Simba Wanyika na baadaye Tanzanites. Mara ya mwisho nilimuona miaka ya mwanzoni mwa 90 pale TAZARA club tukaongea lakini sikumuuliza alikuwa na bendi gani kwa wakati huo.
Miaka michache iliyopita nilikuwa na taarifa kuwa Mohamed Shaweji yupo Nairobi. Hiyo ni kama miaka mitano nyuma. Kwa sasa sina habari zake, sijui wadau wengine.
ReplyDeleteMkuu,
ReplyDeleteNakunukuu:
"..Huyu Hashim Kasanga wa Tancut hajawahi kupiga blowing, alijaribu kujifunza wakati tuko wote TX Seleleka akaacha. Aliacha muziki akaokoka na kubadili jina na dini na Kuitwa Abraham akaajiliwa kama mlinzi, akauwawa na majambazi waliokuja kuiba katika petrol station aliyokuwa akilinda..."
Masikini mja huyu kwa maelezo niliyonukuu napata picha alihangaika na wakautoa uhai wake katika aina ya kuhuzunisha sana. Pamoja na yote nina imani amepumzika kwa amani. Amen.