YOUTUBE PLAYLIST

Thursday, April 15, 2010

Vijana Jazz ilikotokea





Mwaka 1971 Umoja wa Vijana wa TANU uliamua kuanzisha Bendi na kumpa jukumu hilo mwanamuziki John Ondolo Chacha. Ili kutaengeneza bendi, Marehemu Mzee Ondolo aliweza kuwashawishi vijana wa bendi ya Zezemba wakajiunga nae lakini hawakukaa nae muda mrefu kwani walikuwa ni waajiriwa wa kiwanda cha nguo cha Urafiki, hivyo akalazimika kujenga tena Bendi na kwenda hadi Bagamoyo alipoikuta bendi ya Kizibo na akapata wapigaji kumi. 1972 wapigaji wengine tena wakaacha bendi, hivyo akalazimika kutafuta wengine na kikubwa ni kuwa alimpata mpiga solo Hassani Dalali ambaye aliweza kuwatafuta wenzie. Bendi ilipelekwa JKT mwaka 1973, wakati huu tayari ilishampata mtunzi na mwimbaji kutoka TK Limpopo ya Juma Kilaza, kwa jina Hemed Maneti, na baada ya muda kidogo iliweza kumpata Hamis Fadhili kutoka Jamhuri Jazz.
1974 walienda Nairobi na kurekodi nyimbo ambazo ziliaweka msingi wa bendi hiyo. Baadhi ya nyimbo hizo ni Magdalena, Niliruka Ukuta. Mtindo wa bendi wakati huo ulikuwa Kokakoka Balaa

7 comments:

  1. Anonymous15:04

    Kumbe Hasani Dalali alikuwa mpiga solo. Sasa mbona wahasimu wake wanamkadia kwa kusema kuwa alikuwa mbeba na mpanga vyombo vya vijana jazz? Ninamaanisha huyo Dalali mwenyekiti wa Simba. Kwa nini wanamkandia mwezao hivi jamani.

    Mimi ni mwanayanga siwezi kukubali mtu azushiwe jambo hata kama ni mtani wangu simba.

    ReplyDelete
  2. wanaosema alikuwa mbeba vyombo ni waongo, picha na historia ndo hiyo. Yeye ndie msingi wa Vijana Jazz ya leo.

    ReplyDelete
  3. Anonymous00:35

    Mze Kitime, wewe ni ninja mwisho. Hivi una picha za kina assosa kipindi kiel walipokuja TZ na fukafuka? halafu lete picha zako ulipokuwa vijana enzi zile na kina mbwembwe katika ile albamu yenu ya penzi halina shule.

    Hivi kwa nini lakini Mze Kitime umeenda Njenje? We bwana ulikuwa unaliporomosha kweli gitaa. Hivi ni kweli wimbo wa malaine ni wewe uliyeimba na kama ni wewe ulikuwa unatumia lugha gani?

    Ombi, tafadhali rudi Vijana Mze wangu, nakumaindi sana katika umakini wako wa upigaji gitaa. Ombi la mwisho, hivi kuna dalili yeyote ukakutana na wanted muunde bendi yenu wenyewe kama urudio wako vijana utashindikana?

    Mze Kitime tafadhali fikiria HAYA NIKUOMBAYO!

    ReplyDelete
  4. Anonymous12:11

    Hivi Shabani Yohana Wanted yuko wapi na ana fanya nini? maana siku nyingi sijamsikia,

    ReplyDelete
  5. Patrick Tsere17:22

    John mbona humjibu huyo jamaa ombi lake? I support him kwa kweli.

    ReplyDelete
  6. Nitaweka picha za Fukafuka kipindi walipokuja Tanzania. Shaaban Wanted yuko Botswana na anaendelea kukung'uta gitaa huko na kuweka heshima, alirudi miaka miwili iliyopita kwa ajili ya kutembelea ndugu zake

    ReplyDelete
  7. Anonymous02:34

    Bw. Kitime umesoma habari za mkereketwa wa vijana humu? Si yeye pekee hata nami namuunga mkono, kwa nini usiunde bendi yako wewe, uende Botswana ukamrudishe Shaaban Yohana. Bw. Kitime tafadhali fanya ima, unahitajika sana katika ulimwengu wa muziki ndugu yetu.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...