Salehe Kakere, maarufu kama Belesa Kakere, hapa akitangaza kuhamia Orchestra Bima Lee. Hebu soma maelezo katika habari yake unapata picha kamili ya mwanamuziki huyu na kazi zake na historia yake kwa ufupi
YOUTUBE PLAYLIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Sauti ya Belesa Kakere katika nyimbo alizoimba ilikuwa na utamu wa aina yake. Tunamkubali na kumkumbuka.
ReplyDeleteBwana Kitime naomba niulize, Kakere yupo wapi? ameacha kabisa muziki? na Je, mwanamuziki wa kujitegemea Juma Kakere ni ndugu yake?
Asante sana
...kakere alikuwa na albamu ya solo akimshirikisha karama regesu wa msondo na khadija mnoga kama sikosei. ile bendi ilikuwa inaitwa Djakabe masters na ilibeba jina l awimbo wa Mama Mona. Ilikuwa ni albam kali kweli, na kama bado anapiga muziki tafadhali bw. kakere endeleza libeneke la ile albam, nimeipenda mno na bado ninayo mpaka sasa.
ReplyDeleteHivi Bw. Kitime kuna huyu jamaa wa Tanga ana nduguye (si marehemu sheggy) wanapiga muziki mzuri sana ila jina la bendi yao sijalikamata vizuri. Cha kushangaza huyu jamaa pia anaimba ama ana sauti nzuri kama ya sheggy. Unaweza kunitajia bendi za tanga pengine ninaweza kulimbuka jina la bendi yake. Nilimsikia kwenye club raha leo mwaka 1996 nilipokuwa TZ kwa likizo fupi. Yaani nataka kujuwa jina la bendi yake ili nijuwe kama bado anapiga muziki. Kwa kweli alinifurahisha mno kwa kazi yake.
ReplyDeleteKingine bw. kitime...kwa nini wewe na wanamuziki wengine msiandamane kupinga ma dj wa tz maana wanatuangusha mno. fleva si muziki wetu ila wao wnataka tuubeze kwa misingi ipi siijuwi? kuna uwezekano wowote hapa wa maandamano kama haya kweli?
Kakere naukumbuka ule wimbo wake akiwa na Bima Lee
ReplyDelete"...Ndoto yetu ya siku nyingii mwana mamaa, imekuwa kweliii...
Ahadi yetu tuloipanga sikuu nyingi, tumeitimiza...
Utakumbuka tulikuwa wote siku nyingi, tangu tuko masoomoni, Remmyy tulipendana....
tukapanga tufunge ndoa mimi nawe...
Sikumbuki jina la ule wimbo lakini maneno yake tu. Ulikuwa melodius. Baadhi ya mashairi ni kama "nasikia mwanisema eti kanipa dawa, wengine wanisengenya nimesahau kwetu. Yaacheni yale yaliyo ya kwetu, yashikeni yale yaliyo ya kwenu".
ReplyDeleteVery good song
Salehe Kakere alifariki yapata miaka miwili sasa! Alifia Tanga na alizikwa huko huko. Nduguye Juma Kakere yeye bado yumo katika muziki. Tunaomba Mwenyezi Mungu amrahisishie mitihani yake ya kaburini na amsamehe madhambi yake kisha amuingize Jannat Firdaus, Ameen.
ReplyDelete