Nimeona nirudie tena posting hii pengine iliwahii mno, miaka iliyopita karibu kila wilaya ilikuwa na bendi, naomba tusaidiane kukusanya kumbukumbu hizi muhimu kwa historia ya muziki wa Taifa letu. Kwa mfano pale Same niliwahi kukuta band ya Tanu Youth League siikumbuki jina lake, pia nimeshakuta bendi pale Igunga, Mwadui, Sumbawanga, Makambako, kule Mbeya, nakumbuka ilikuweko bendi ya Bwana Remmy, hebu tuchangie tuone tutafika wapi. Bendi hizi ziliwahi kutoa vibao vingi vilivyotingisha anga za muziki wakati huo. Kwa mfano Shinyanga Jazz na kibao chao Tenda wema uende zako kilichotungwa na kuimbwa pia na Mzee Zacharia Daniel, ambae mpaka kifo chake aliitwa Mzee Tenda wema, au vibao vya Mzee Zahir Ally Zorro akiwa na Kimulimuli, Kabwe,Tausi na vingi vingine , waliopitia JKT Mafinga wakati huo wanakumbuka raha ya bendi hii. Unajua kwanini Bendi iliitwa Kimulimuli? Bendi ilipata taa za stage zinazowakawaka zilizokuwepo pamoja na bendi kwa hiyo taa hizo kumulikamulika ndo kukatoa jina la Kimulimuli kuna kitu kingine muhimu, kwa kuwa bendi zilitoka sehemu mbalimbali kila moja ilikuwa na staili yake na hivyo kuleta utamu katika anga za muziki. Kila mtu atakubali hakuna kitu kinakosesha raha
(Pichani ni John Kitime na Kasaloo Kyanga wakiimba wimbo wa Masafa Marefu na kukumbuka walipokuwa wanaitwa Bush Stars)
Iringa-
Highland Stars
Tancut Almasi Orchestra
Chikwala chikwala
Ruaha International
Vico Stars
Mkwawa Orchestra
Kimulimuli JKT
TX Seleleka
Bose Ngoma
******
Morogoro
La Paloma Jazz
Cuban Marimba
Morogoro Jazz
Les Cubano
Vina vina Orchestra
Sukari JazzKilombelo Jazz
Malinyi Jazz
Kwiro Jazz
Mahenge Jazz
Kilosa Jazz
Les Cuban
******
Tanga
Atomic Jazz
Jamuhuri Jazz
Tanga International
Amboni Jazz
Bandari Jazz
Watangatanga
Lucky Star
Black Star
******
Tabora
Tabora Jazz
Nyanyembe Jazz
Kiko Kids
Usoke Jazz
******
Kigoma
Super Kibisa Orchestra
Mwanza
Orchestra Super Veya
******
Moshi
Orchestra
Bana Africa Kituli
********
Materu Stars
Saki Band
Super Melody
(Pichani Kibonge, mwanamuziki mkongwe wa Super Melody ya Dodoma)
Mara
Mara Jazz
Musoma Jazz
Tembo Jazz
Orchestra Sere sere
Super Matimila
******
Lindi
Mitonga Jazz
******
Masasi
Kochoko Jazz
Mtwara
Bandari Jazz
Shinyanga
Shinyanga Jazz




