Nimeona nirudie tena posting hii pengine iliwahii mno, miaka iliyopita karibu kila wilaya ilikuwa na bendi, naomba tusaidiane kukusanya kumbukumbu hizi muhimu kwa historia ya muziki wa Taifa letu. Kwa mfano pale Same niliwahi kukuta band ya Tanu Youth League siikumbuki jina lake, pia nimeshakuta bendi pale Igunga, Mwadui, Sumbawanga, Makambako, kule Mbeya, nakumbuka ilikuweko bendi ya Bwana Remmy, hebu tuchangie tuone tutafika wapi. Bendi hizi ziliwahi kutoa vibao vingi vilivyotingisha anga za muziki wakati huo. Kwa mfano Shinyanga Jazz na kibao chao Tenda wema uende zako kilichotungwa na kuimbwa pia na Mzee Zacharia Daniel, ambae mpaka kifo chake aliitwa Mzee Tenda wema, au vibao vya Mzee Zahir Ally Zorro akiwa na Kimulimuli, Kabwe,Tausi na vingi vingine , waliopitia JKT Mafinga wakati huo wanakumbuka raha ya bendi hii. Unajua kwanini Bendi iliitwa Kimulimuli? Bendi ilipata taa za stage zinazowakawaka zilizokuwepo pamoja na bendi kwa hiyo taa hizo kumulikamulika ndo kukatoa jina la Kimulimuli kuna kitu kingine muhimu, kwa kuwa bendi zilitoka sehemu mbalimbali kila moja ilikuwa na staili yake na hivyo kuleta utamu katika anga za muziki. Kila mtu atakubali hakuna kitu kinakosesha raha
(Pichani ni John Kitime na Kasaloo Kyanga wakiimba wimbo wa Masafa Marefu na kukumbuka walipokuwa wanaitwa Bush Stars)
Iringa-
Highland Stars
Tancut Almasi Orchestra
Chikwala chikwala
Ruaha International
Vico Stars
Mkwawa Orchestra
Kimulimuli JKT
TX Seleleka
Bose Ngoma
******
Morogoro
La Paloma Jazz
Cuban Marimba
Morogoro Jazz
Les Cubano
Vina vina Orchestra
Sukari JazzKilombelo Jazz
Malinyi Jazz
Kwiro Jazz
Mahenge Jazz
Kilosa Jazz
Les Cuban
******
Tanga
Atomic Jazz
Jamuhuri Jazz
Tanga International
Amboni Jazz
Bandari Jazz
Watangatanga
Lucky Star
Black Star
******
Tabora
Tabora Jazz
Nyanyembe Jazz
Kiko Kids
Usoke Jazz
******
Kigoma
Super Kibisa Orchestra
Mwanza
Orchestra Super Veya
******
Moshi
Orchestra
Bana Africa Kituli
********
Materu Stars
Saki Band
Super Melody
(Pichani Kibonge, mwanamuziki mkongwe wa Super Melody ya Dodoma)
Mara
Mara Jazz
Musoma Jazz
Tembo Jazz
Orchestra Sere sere
Super Matimila
******
Lindi
Mitonga Jazz
******
Masasi
Kochoko Jazz
Mtwara
Bandari Jazz
Shinyanga
Shinyanga Jazz
Mkuu,
ReplyDeleteSamahani, hivi kasheshe la TX Seleleka na Mzee Kambanyuma kule Iringa lilihusu nini?
Mheshimiwa kitime leo umenifurahisha maana umeweka picha ya mwanamuziki ninayemfahamu sana huyu muheshimiwa Kibonge. Niliwahi kuwa naye Morogoro kwenye tukio moja. Huyu jamaa alinisaidia sana kunipa story za wanamuziki wa zamani kwa kweli nilifurahi kukutana naye. Sasa Kitime naomba utupe historia ya Zahir Ally Zorro, kwa hakika nitafurahi.
ReplyDeleteSilikumbuki hilo sheshe la TX Seleleka na Mzee Kambanyuma labda ukinikumbusha nitakumbuka, ujue hiyo lazima ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya themanini ni zamani kiasi. Kweli Kibonge ni mwanamuziki wa siku nyingi na ana mengi, nategemea kuwafuata wanamuziki kama hawa niweze kurusha hewani matukio makubwa ya enzi hizo, na hali halisi ilivyokuwa
ReplyDeleteBwana John Kitime,
ReplyDeleteHongera sana kwa blog hii ambayo sisi wapenzi wa muziki wa hapa nyumbani tumekuwa tukifaidika sana kwa taarifa.
Nimefurahi kukuona hapo kwenye picha ukiwa na Kasaloo mkikumbushia wimbo wa Masafa Marefu. Ni wimbo ambao hauchuji. Nilikuwa nasoma Mazengo Sekondari wakati huo, kila TANCUT mkitembelea Dodoma basi lazima jumapili mchana mpige uwanja wa Jamhuri. Nilikuwa natoroka nakuja kuwasilizeni hadi mwisho. Bendi yenu wakati huo mlikuwa na sare (uniform). Wakati mwingine waimbaji wana sare yao na wapiga ala sare yao. Basi Kinye-Kinye Kisonzo kilikuwa kinanoga sana.
Wimbo huu wa Masafa marefu pamoja na nyingine nimesikia zimerudiwa na tena na kima Kasaloom kwa jina la Bush Stars. Mapigo ymekuwa ya haraka zaidi na kwa kweli utamu wa nyimba upo pale pale. Aliyepiga solo katika awamu hii amenichengua sana. John waweza kujua ni nani alilipiga hapo?
Nakutakia kila la heri pamoja na wachangiaji wote humu. Kwa kweli mnaleta burudani sana.
Danstan
naikumbuka Dodoma wakati huo,hata wakati wa mkutano wa Kizota 1987 tulikaa Dodoma hoteli miezi mitatu, ndipo zilipotungwa nyimbo kama Helena mtoto wa Arusha uliotungwa na Kyanga Songa, Butinini wa Kasaloo,na wimbo Binti Almasi wa John Kitime ambao haukurekodiwa kutokana na kamati ya RTD kudai unahamasisha watu kuiba almasi, na wimbo Pili wangu wa Abdul Salvador
ReplyDeleteKaka John, nakupongeza sana kwa kuanzisha kitu hii ambayo inatoa picha halisi ya Muziki wakati ulikuwa muziki hapa Kwetu Bongo. mi nakumbuka hata kwenye kata kulikuwa na bendi, mfano pale kwetu Ussoke kulikuwa na Bendi inaitwa Ussoke Jazz a.k.a Segere matata. Sijui nini kilitokea. Anyway tuyaache hayo, jambo la msingi ni kwamba nakupongeza sana kwa kazi nzuri unayoifanya kupitia hii ndude, tuko pamoja na nashukuru kwamba nimepata Source mpya ya Habari.
ReplyDeleteNimefurahi MZEE KITIME kunikumbusha bendi za mikoa mbalimbali zilizokua zikivuma.
ReplyDeleteLakini furaha yangu zaidi nia pale ulipo itaja bend kutoka mkoa wa mbeya iliokua inajulikana jina marufu la bend ya REMMY.Sisi wapenzi wa muziki wa wakati huo tulikua tukiita remmy madebe.mkongwe huyo wa muziki kwa sasa hatunae tena duniani,lakini tuna mkumbuka kwa jinsi alivyo kua akikonga moyo yetu kwa music safi sana.Pia nakumbuka zaidi bendi ya tancut alamas kianga songa na kasalo kianga wakiwa na gari vockswagen comb ambalo mara kwa mara niwapo Iringa nilikua nikiwaona nalo.
Je bend ya TOMA TOMA chini ya kings Tomas unaweza tupatia picha zake yakokwenye blogger.
Katika miaka ya sabini pale Musoma kulikuwa na bendi nyingine ikiitwa Mkendo Jazz- Segese; hiyo ni tofauti na Mara Jazz -Sensera.
ReplyDeleteArusha:
ReplyDeleteKurugenzi Jazz Band.
"...matumaini yetu wafrika siasa ya ujamaaa ohh, ujamaa hautakufa Tanzania twaulinda..., mawazo sahau ujamaa hautakufaaa...., fungeni vibwebwe tujenge ujamaa...."
Jamani wapo wapi kina Kasaloo na kianga songa wa Tan cut almasi? pia nimekumbuka ule wimbo wako wa "malaine" nadhani sijakosea kuandika...ungeweka verses zake na maana yake pia ingekuwa bomba!\Kazi nzuri!!!
ReplyDelete