YOUTUBE PLAYLIST

Saturday, March 13, 2010

Wanamuziki ndugu 1



Katika historia ya muziki kumekuweko na familia kadhaa ambazo zimekuwa zikitoa wanamuziki zaidi ya mmoja. Moja ya familia iliyokuwa maarufu ilikuwa ni familia ya akina Sabuni. Unawakumbuka? Niko katika mawasiliano na mwanamuziki mmoja aliyepiga na ndugu watatu kati ya hao na tutapata kumbukumbu nyingi karibuni

Kushoto Cuthbert Sabuni, chini ni Raphael Sabuni akiwa na mwimbaji wa kike ambaye bado natafuta jina lake lakini alijulikana kama 'Lady Soul'

9 comments:

  1. Duh! hao lazima walikuwa kabla sijaliwa hata siwajui je kuna nyimbo walizokuwa wakiimba ambazo twaweza kusikiliza?

    ReplyDelete
  2. Anonymous20:54

    This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli hapa tunaongelea wanamuziki hawa wakitamba mwishoni mwa miaka ya sitini na mwanzo wa sabini. Najua hii bendi ya Jets ambayo Raphael alikuwa akipigia ilikuja kuwa STC Jazz...STC(State Trading Company) zilikuja geuka zikawa RTC (Regional Trading Company) na kabla ya hapo kulikuwa na kitu kinaitwa COSATA...... Alipokuwa STC Jazz walirekodi nyimbo kama STC tuko hapa, Usiku wa manane, mwimbaji akiwa Marijani. Ngoja nikuwekee wimbo japo mmoja wa wa STC Jazz kwenye playlist yangu uusikie

    ReplyDelete
  4. Anonymous23:17

    Mkuu,

    Katika mada hii naomba tuwakumbuke na tuwaongeze wanamuziki wanandugu kama kina Misianias, Kinyongas (Dar Jazz mpaka Simba Wanyika), The Rajabus (STC mpaka Trippers), Balisdyas, Uvuruges, Kivovanis, The Sabunis (STC mpaka Juju Masai),Mhutos (Spaks mpaka Super Africa, Juju Masai, Winds 85, Watafiti, Chezimba, TatuNane),Kapingas (BarKeys mpaka Tanzanites), Chiduos (Barkeys mpaka Tanzanites), Chirwas, Galinomas, Swebes, Chopetas, Nombos, Nhigulas, wale waliokuwa Super Volcano hadi Kurugenzi jazz, na wale kina Adrian na nduguze siwakumbuki.

    Mkuu na wadau, kama tungekuwa wa kujipangapanga Tanzania nayo ingeweza kutoa Jackson 5 na The Jacksons au mnasemaje?

    ReplyDelete
  5. Patrick Tsere07:03

    John huyo dada akiimba na akina Sabuni siyo Alice Mhuto kweli? Maana kaka yake aitwae Michael Mhuto (siku hizi nasikia ni mtumishi wa Mungu Haleluja), alikuwa Flaming Stars akipiga na akina Sabuni.Kama kumbukumbu zangu ni sahihi.

    ReplyDelete
  6. Patrick Tsere07:07

    Dada Yasinta wimbo ambao ninaukumbuka ukipigwa na Flaming Stars wakiwa na akina Sabuni ni 'Mpenzi Maria sisahaux2 Hata nyota nazo nayo mbalamwezi haziwezi kusahaaau Maria.' Something like that

    ReplyDelete
  7. Anonymous02:16

    mzee ni kujana mwenye umri wa miaka 28 wakti nikiwa mdogo ni nilkua na mpenzi wa kusikiliza radio na ilikua ikinipotezea muda sana nilikua napendelea kusikiliza muziki huku nijipa matumaini iko siku nitautanngaza muziki nakuusimulia kuindani zaidi chaajabu iyo ndoto imepote leo hii nafanya kazi ya hotel kama bar man huku zanibar hoteli ya kutalii kubwa tu sasa ivi majuzi nilikua nabalizi kwenye hizi blog zakikwetu nikakutana na nawe nimependa sana kwa jinsi unavyo uelezea muziki wa dansi kwa kushirikiana na wadau wengine nikakumbuka ndoto zangu za kuusoma muziki na kuutangaza ili sasa mjukukmu nayo ya kifamilia ndo ivyo njiuliza niache kazi nije huko mjini unisaidie kinifundisha muziki hatimae niutangaze niuelezee katika radio ili watu na mie wanielewa na kuupenda muziki wewtu kweli napenda kusomea mziki ili tu nipate nafasi ya kuutangaza sijui kama ninaweza kuutangaza kwa kuimba ilia nkuomba msaada eidha unasidie kwa kunipa somo la muziki na kinilithisha baadhi ya vitu vya zamani ulivyonavyo ktk tasnia hii ya muzikiniko tayari kuacha kazi kwa sasa nije nhitimishe ndoto hii nijarivbu japo kutafuta kazi ya hoteli hapo dar ili mradi niweze pata nafasi ya kukufuata popota ulipo kwa ajili ya kji funza histiria ya muziki toka kwako na kwa wengine pia ni
    kijana wako sijui niseme jukuu wako ila ndhani mjukuu Adonisi Alfred Marinya

    ReplyDelete
  8. Anonymous02:36

    Mkuu,

    Info zinakuja poolepoole Auntie Alice katajwa kwingine katajwa Judy Hadebe! Itafika utaambiwa drummer mwanamke wa kwanza Tanzania aliitwa nani na mwanae aliyekuja kuwa drummer-cum-lead vocalist atatajwa!

    Unakumbuka nilihint waliohamia madhabahuni?

    ReplyDelete
  9. Kwanini usiwataje? its afact si dhambi tunakusanya historia. Nakumbuka nilipokuwa Oshekas, mke wa Band leader Briana Shaka alianza kupiga drums

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...