YOUTUBE PLAYLIST

Thursday, March 18, 2010

LIBENEKE

Mheshimiwa mmoja kaniomba niweke mwanga kwenye hili neno ambalo limetajwa hapo juu. Katika kumbukumbu zangu, Libeneke ulikuwa mtindo wa Butiama Jazz Band, bendi iliyokuwa chini ya uongozi wa marehemu mzee Mkwega, ikiwa na mpiga solo mzee Makelo ambae yuko Shikamoo Jazz, baadhi ya waimbaji akiwemo Saidi Hamisi ambaye kwa miaka mingi mpaka kifo chake alikuwa Vijana Jazz. Kulikuweko na wimbo ambao ulikuwa maarufu ukiwataja wanamuziki wa bendi hiyo na kibwagizo chake kilikuwa ....waache waseme, watachoka wao mtindo libeneke utatia fora...... Mkuu wa libeneke upo? Karibu wapenzi wa Butiama Jazz

16 comments:

  1. Anonymous12:17

    Mkuu
    Naomba kufahamu ule mziki wa Malaika umetungwa na nani? Vilevile nani alitunga ule wimbo "naomba nipate lau nafasi nipate kusema nawe kidogo aah Mamaa mwenzio naumia"

    ReplyDelete
  2. Aisee blogu hii inatufunza mengi.

    ReplyDelete
  3. Kuna utata kuhusu wimbo Malaika, lakini ninachofahamu wimbo ule haukutungwa na Fadhili William, kwani ulikuwa tayari unapigwa na bendi ambayo Fadhili William alikuwa ni fundi mitambo tu. Lakini yeye ndiye aliyeurekodi na hivyo sheria ya hakimiliki inamlinda na kumpa haki zote yeye. Nategemea kuanzisha blog yenye kutoa mafunzo kuhusu haki za wasanii, maana hili ni fundisho kubwa juu ya uelewa wa hakimiliki. Huo wimbo wa pili uliimbwa na Daudi Makwaia akiwa Kilwa Jazz lakini ulikuwa umeigwa kutoka wimbo wa Tabu Ley akiwa na African Fiesta baadhi ya maneno ya Tabu Ley yalikuwa............. Mokolo mosusu ngai nakanisi
    Naloti lokola ngai nakolala
    A mama
    Mokolo nakokufa

    Mokolo nakokufa, nani akolela ngai ?
    Nakoyeba te o
    Tika namilela.
    Liwa ya zamba soki mpe liwa ya mboka
    Liwa ya mpasi soki mpe liwa ya mai
    O mama
    Mokolo nakokufa
    Mokolo Nakokufa"
    Kwa kifupi yalikuwa maneno mazito yakisema....ya Siku nitakayokufa nani atakaenililia?

    ReplyDelete
  4. mzee kitime kwani mafunzo ya haki za wasanii hayatapanda humu. mie nadhani uwe na segment itakayotoa mafunzo hayo humu-humu.

    ReplyDelete
  5. Poa nilikuwa na nia ya kuwa na blog ya hali ya muziki sasa naona kuna mengi nyuma ya pazia yanafaa yajulikane

    ReplyDelete
  6. Anonymous21:49

    Mwakitime kwa ninavyoelewa mimi LIBENEKE ni ngoma ya asili katika maeneo ya Morogoro hasa Ifakara na Mahenge sina uhakika kama na Songea ipo. Nimeaijua miaka ya zamani sana hata kuicheza najua.

    ReplyDelete
  7. Anonymous21:55

    Makelo ni majina ya Ifakara na Mahenge sitashangaa kama Mzee Makelo ndio alioleta hilo jina LIBENEKE kwenye bendi maana ni ngoma ya maeneo aliyotoka.

    ReplyDelete
  8. Nauhakika huo ndio ukweli kuwa LIBENEKE ni ngoma kutoka huko kwa kuwa pamoja na kuwa bendi iliitwa Butiama Jazz, wanamuziki wake walitokea maeneo uliotaja, Mzee Makelo, Mzee Mkwega, Said Hamisi wote walikuwa Wapogolo. Bendi nyingi za zamani zilianza kwa mtindo huu, haswa wakati miji bado ni mipya watu wa kabila moja walipendelea kuishi pamoja na kuwa na starehe zao za pamoja. Zamani kulikuweko na Rufiji Jazz ya Wandengeleko,Kilwa Jazz iliyoanzishwa na wanamuziki kutoka Kilwa, Western Jazz, wanamuziki kutoka magharibi ya nchi hasa Kigoma na Tabora na kadhalika. Naona hilo ndo jibu haswaa la chanzo cha LIBENEKE. Ila kwa utamu zaidi nitamtafuta Mzee Makelo atupe stori nzima ya bendi hii.

    ReplyDelete
  9. Hapa tunajifunza mengi. Mimi nilijua rafiki yangu DC wa Tegeta alikuwa ameibua neno jipya.

    ReplyDelete
  10. Hahahaha Bwana Madaraka karibu ndani, tena mara ya mwisho tulikutana Community Centre Iringa ukiyarudi mapigo ya Sewando, Mpumilwa, Manji na Kakobe katika kundi zima la Mkwawa Orchestra,bila kumsahau Adam Mwakang'ata hahahaha. Hebu tia neno. Na najua ulihusika sana na Balisidya kiasi cha kumpa tiketi ya kwenda Sweden, picha ilitoka gazetini hebu tukumbushe japo najua mwisho wake bora usahaulike

    ReplyDelete
  11. Anonymous15:00

    Mzee Kitime siku utakayo acha kutuupdate humu utakuwa umeniudhi sana japo umri wangu si mkubwa sana ila miziki mingi nimeisikia wakati nakua kwenye miaka ya mwishoni mwa sabini na miaka ya themanini ila nilikuwa siijui chanzo chake na hapa nimeshukuru sana kwa kunipa jibu kuhusu wimbo wa malaika yaani siwezi kupitisha siku bila kutembelea humu. Tuwekee vitu kama leo nimefurahi sana nimekutana na Mafumu Bilali Mbondenga Chef Pride japo yy hanifahamu ila mie nimemtambua

    ReplyDelete
  12. Nadhani faraja ya mwenye blog yoyote au mtunzi yoyote ni kujua kuwa kuna watu wahamu na kazi yake , hivyo tuombe uzima. Jina la Mafumu ni Mafumu Bilali BOMBENGA anayo mengine lakini hayo tunaitana wenyewe tukikutana hahahaha

    ReplyDelete
  13. Patrick Tsere22:59

    John huo wimbo wa napenda nipate lau nafasi haukuimbwa na Ngulimba wa ngulimba Juma Mrisho na solo kukun'gutwa na Duncan Njilima?

    Hiyo ndiyo ilikuwa miaka ambapo bendi zinashindana kuiga bila ya kutunga nyimbo zao. Wao wanachofanya ni kuingiza maneno yao. Ingekuwa enzi za leo na mambo ya haki miliki naamini bendi zetu nyingi zingeadhibiwa.

    ReplyDelete
  14. kuiga kuko mpaka leo. Kofii akivaa nguo bila kuondoa lebo ndo itakuwa hivyo kwa wote. Hali ni mbaya watu wanaiga album nzima, wanabadili vibwagizo kuwa vya kiswahili , lakini kuanzia kucheza mpaka kuvaa ni hivyo tu. Mzee Makwaia yuko Magomeni karibu na Delux hiyo ni home work moja ya kusafisha ukweli

    ReplyDelete
  15. Patrick Tsere00:42

    Nafurahi kuona mchango wa mdogo wangu Madaraka ndani ya blog hii. Inaashiria kuwa wako waheshimiwa wengi tu siku za usoni watachangia humu ndani.

    ReplyDelete
  16. Kaka yangu Patrick, haya masuala ni wajibu. Rafiki yangu, DC wa Tegeta, amekuwa akiyaendeleza kwa muda mrefu katika kuhabarisha watu kuhusu masuala mbalimbali. Na mimi nimeona niwaunge mkono wanablogu wote, pamoja na ndugu yetu Kitime. Nimegundua si vibaya kuendeleza libeneke kwa mtindo mpya: http://muhunda.blogspot.com/2010/03/ccm-yaendeleza-rirandi-ughaibuni.html

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...