YOUTUBE PLAYLIST
Monday, February 1, 2010
Tulikuweko tupo tutakuweko
Wasanii ni kioo cha jamii, huu ni usemi ambao umezoeleka
Katika miezi miwili iliyopita kumejirudia jambo ambalo kila mara mimi huliona la ajabu
Tasisi moja imetangaza iko katika mchakato wa kutunga sheria ya kuwabana watunzi wa filamu kuhakikisha wanapeleka tungo zao kuhakikiwa kabla ya kuzitoa hadharani kwani nyingine zinakiuka maadili yetu.
Ningependa kuwakumbusha viongozi wanaopiga marufuku na hawa wanaotunga sheria za kubana watunzi kuwa wakumbuke, wasanii ni kioo cha jamii kwa hiyo yote yanayoendelea katika sanaa yanaonyesha jamii ilivyo. Hivyo basi kuvunja kioo, au kukataa kutumia kioo si njia ya kubadili ubaya wa sura yako.
Tatizo si wasanii, kwani wao ni sehemu tu ya jamii, tatizo ni mmomonyoko wa maadili katika jamii. Wakati unaruhusu vyombo vingine vionyeshe filamu zenye maadili ya kimagharibi masaa ishirini na nne na hivyo kutengeneza jamii inayokubali hayo, halafu kumkataza msanii wa Kitanzania asitunge hadithi ikiwa na maadili hayo mapya, atapata wapi wateja wa kazi zake? Atakachotengeza ataambiwa kazi zako zimepitwa na wakati.
Hata katika nchi ambazo zimeendelea kuna mfumo ambao hutengenezwa kulinda na kuendeleza maadili ya nchi hivyo wananchi kuishi wakiwa wana aina ya maadili ya nchi husika. Vyombo vya kurusha matangazo katika nchi nyingi huwa na asilimia iliyopangwa ya matangazo ambayo huitwa local content. Mfano kama mtu anataka kuendesha Radio au TV anajua kuwa asilimia sitini ya matangazo yake lazima yawe ni kutoka nchini, filamu, muziki na kadhalika, muziki hapa si bongo fleva na muziki wa dansi tu bali hata ngoma za kiasili. Jambo hili ni muhimu
Wakati Balozi wa
Serikali imeachia utamaduni unaendeshwa na wafanya biashara, matamasha mashindano , kutafuta vipaji na kadhalika kwa misingi ya biashara unafanya kitu kinacholipa. Serikali iwekeze tena
Thursday, January 21, 2010
Hebu jaribu kupata picha, umelima shamba lamba lako na kupanda mahindi ambayo umeyatunza vizuri na yako tayari kuvuna….. unaamka siku moja na kukuta kuna mtu kayavuna na ameanzisha biashara anapata fedha nzuri wewe huna hata fedha ya kula.
Au umenunua suti nzuri akaja mtu akaivaa harusini, kesho yake anakuja kukutaarifu jinsi walivyomsifia harusini.
Hiyo ndio picha ilivyo katika shughuli za sanaa
Wasanii hufanya kazi ngumu ya kutunga na kufanya mazoezi kisha kurekodi kazi zao, kabala hawajafaidi kazi zao hukuta shamba lao likiwa linavunwa kwa njia mbalimbali. Wengine hurudufu kazi zao, wengine huzitumia kutangaza biashara zao. Wengine huzitumia kuhamasisha mikutano
Kutokana na matumizi mengi ambayo yanaweza kutokana na kazi zilizotungwa, na kutokana na ugumu wa kudhibiti kazi hizi sheria zinazitwa za Hakimiliki hutumika katika kulinda maslahi ya mtunzi kwa upande mmoja na mtumiaji kwa upande mwingine.
Ulinzi wa hakimiliki umekuwa mgumu
Katika maeneo yote ya karibu ya vyuo na sehemu za elimu ya juu utakuta biashara kubwa ya mashine za fotokopi, kazi ya mashine hizi ni kurudufu maandiko na vitabu mbalimbali vya watu bila kujali kuwa waliotunga vitabu hivyo wanahitaji viuzwe ili wapate mafao
Kwa masaa ishirini na nne kila siku redio na baadhi ya Tv hurusha hewani nyimbo za watu, tena kwa vipindi ambavyo hutangazwa wazi kuwa vimedhaminiwa na kampuni kubwa mbalimbali zenye kuheshimika. Vituo hivi vinamilikiwa na kuendeshwa na watu wanaoheshimika katika jamii kwa kuhamasisha vijana wajiajiri, lakini ikishafika kwenye eneo la kulipia matumizi ya kazi za wasanii kigugumizi kikubwa kinatokea.
Watetezi wa haki mbalimbali za wananchi wa
Sheria za hakimiliki humpa mtunzi haki zifuatazo katika tungo zake;
(a) Kurudufu kazi
(b) Kusambaza kazi
(c) Kukodisha kazi
(d) Kutafsiri kazi
(e) Kubadili matum izi ya kazi
(f) Kuonyesha kazi hadharani-exhibition
(g) Kuifanya kazi hadharani-public performance
(h) Kutangaza kazi katika vyombo vya habari-broadcasting
(i) Kuwasilisha kazi kwa umma kwa njia yoyote
(j) Kuingiza kazi nchini
Mtunzi anaweza akaingia katika makubalianao na mtu mwingine ili kutumia moja au zaidi ya haki hizo ili kupata mafao yake.
Nadhani ukiangalia haki hizo hapo juu utaweza kuona jinsi haki za watunzi zinavyovyunjwa masaa ishirini na nne.
Ununuapo CD au DVD elewa kuwa umeipata kwa ajili ya matumizi yako binafsi, ukianza kuitumia kwa shughuli yoyote ile nyingine unaanza kuingilia haki zilizotajwa hapo juu. Hivyo basi kununua CD hakukupi haki ya kuanza kutoa nakala za CD hiyo, wala kuanza kuirusha redioni au kuipiga hadharani kwenye baa au hoteli, hapana, utahitaji kupata ruksa kuanza kutumia kwa kazi hizo za ziada. Ruksa hizi hupatikana kwenye Chama kinachoshughulika na mambo ya Hakimiliki
COSOTA hutoa leseni ambazo watumiaji wa kazi za muziki huzilipia na fedha zinazopatikana hugawiwa watunzi. Katika nchi ambazo taratibu hizi zinafanya kazi wanamuziki na wadau wengine wa muziki hupata fedha nyingi kutokana na matumizi ya kazi zao. Bado kuna tatizo kubwa la hili kwani kama nilivyosema utamaduni wa kudharau haki za watunzi bado ni mkubwa katika jamii ya
Jambo la kufurahisha ni kuwa tayari kuna wafanya biashara kutoka sehemu mbalimbali nnchini ambao wamekuwa wanalipia kwa matumizi ya kazi za muziki na COSOTA wamekwisha gawa fedha kwa mara ya saba kwa watunzi wa kazi mbalimbali.
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...