Wasanii ni kioo cha jamii, huu ni usemi ambao umezoeleka
Katika miezi miwili iliyopita kumejirudia jambo ambalo kila mara mimi huliona la ajabu
Tasisi moja imetangaza iko katika mchakato wa kutunga sheria ya kuwabana watunzi wa filamu kuhakikisha wanapeleka tungo zao kuhakikiwa kabla ya kuzitoa hadharani kwani nyingine zinakiuka maadili yetu.
Ningependa kuwakumbusha viongozi wanaopiga marufuku na hawa wanaotunga sheria za kubana watunzi kuwa wakumbuke, wasanii ni kioo cha jamii kwa hiyo yote yanayoendelea katika sanaa yanaonyesha jamii ilivyo. Hivyo basi kuvunja kioo, au kukataa kutumia kioo si njia ya kubadili ubaya wa sura yako.
Tatizo si wasanii, kwani wao ni sehemu tu ya jamii, tatizo ni mmomonyoko wa maadili katika jamii. Wakati unaruhusu vyombo vingine vionyeshe filamu zenye maadili ya kimagharibi masaa ishirini na nne na hivyo kutengeneza jamii inayokubali hayo, halafu kumkataza msanii wa Kitanzania asitunge hadithi ikiwa na maadili hayo mapya, atapata wapi wateja wa kazi zake? Atakachotengeza ataambiwa kazi zako zimepitwa na wakati.
Hata katika nchi ambazo zimeendelea kuna mfumo ambao hutengenezwa kulinda na kuendeleza maadili ya nchi hivyo wananchi kuishi wakiwa wana aina ya maadili ya nchi husika. Vyombo vya kurusha matangazo katika nchi nyingi huwa na asilimia iliyopangwa ya matangazo ambayo huitwa local content. Mfano kama mtu anataka kuendesha Radio au TV anajua kuwa asilimia sitini ya matangazo yake lazima yawe ni kutoka nchini, filamu, muziki na kadhalika, muziki hapa si bongo fleva na muziki wa dansi tu bali hata ngoma za kiasili. Jambo hili ni muhimu
Wakati Balozi wa
Serikali imeachia utamaduni unaendeshwa na wafanya biashara, matamasha mashindano , kutafuta vipaji na kadhalika kwa misingi ya biashara unafanya kitu kinacholipa. Serikali iwekeze tena
"Serikali imeachia utamaduni unaendeshwa na wafanya biashara, matamasha mashindano , kutafuta vipaji na kadhalika kwa misingi ya biashara unafanya kitu kinacholipa. Serikali iwekeze tena kama zamani katika sekata hii ili kuweza kufufua na kukuza utamaduni wa Mtanzania ambao sasa unakokwenda ndio tunaonyeshwa na wasanii ambao kwa kuwazuia haisaidii kubadili mwelekeo wa maadili ya watu."
ReplyDeleteWhat a CLOSING STATEMENT.
Truth, just truth and call it NAKED TRUTH.
Kwa kuongeza nguvu hapa, TUTAFIKA TUUUU