Wednesday, June 30, 2010

Stage Shows

Taratibu za akina mama kucheza show zilikuwa zikienda sambamba na shughuli nyingine za muziki kwa miaka mingi sana. Nimebahatika kukutana na akina mama wawili ambao walikuwa katika ngazi za juu za uchezaji miaka hiyo. Chini kushoto ni Maida Lwambo, yeye alianza shughuli za sanaa 1973, katika kikundi cha sanaa cha Magereza akishiriki , sarakasi na maigizo, mwaka 1977 akahamia kikundi cha sanaa cha Urafiki akiwa kama muimbaji katika kwaya, na mwaka 1979 hadi 1981 alikuwa akicheza show Orchestra Maquis Original, akahamia kwa miezi michache kwa Doctor Remmy,kisha kati ya 1985 mpaka 1988 alikuwa Orchestra Safari Sound(Dukuduku), na hatimae akarudi Maquis mpaka alipostaafu kucheza show. Kulia ni Anna Mganga, alieanza sanaa katika kikundi cha Tanzania Breweries mwaka 1974,akajiunga na kundi la sanaa la Bora Shoes, na hatimae mwaka 1981 akajiunga na Maquis, kwa muda mfupi mwaka 1983 alihamia OSS, lakini alirudi tena Maquis mbapo alikaa mpaka 1993, alipoacha kucheza show. Hawa wadada walikuwa ndio wanatikisa jiji katika fani yao miaka hiyo.

Tuesday, June 22, 2010

Saba saba..............

KWA KWELI KILA TUKIMALIZA MAZOEZI NATOKA NIMEFARIJIKA KUWA TANZANIA TUNA WANAMUZIKI WA KIWANGO CHA JUU ILA TARATIBU ZETU NDIO MBAYA. KWA WALE WATAKAOHUDHURIA ONYESHO LA HAWA WANAMUZIKI WAKONGWE WATAONA NINI MAANA YA NINACHOSEMA. NA LA KUSIKITISHA NI AINA YA MUZIKI UNAOPIGWA HAPA NAONA NDIO UKO UKINGONI KUONDOKA NA WAZEE HAWA

Monday, June 21, 2010

Sabasaba........

Mazoezi yanaendelea kwa nguvu .

Masoud Masoud alipita kujionea

King Kiki na Bi Shakila....what a combination!!!!!!!


King Kiki, Shakila, Bitchuka

Saturday, June 19, 2010

Disco

Haya djs walikuwa, na bado ni watu muhimu katika shughuli za muziki Tanzania, labda nikupe maelezo mafupi. Baada ya Biribi kupumzika, akazuka kijana huyu, kwanza kwenye parties maeneo ya Upanga, na baadae kuwa dj maarufu aliyejulikana kama Dj Emperor, akiburudisha sana pale Agip Motel na kisha kuhamia ghorofa ya saba New Africa Hotel, alifanya mambo makubwa Arusha pia wapenzi wa disco mnamkumbuka? na disko lake liliitwaje?
Friday, June 18, 2010

Tancut almasi Orchestra enzi hizo

Tancut Almasi katika onyesho mojawapo. Hawa dada wawili, ni Nana Njige(marehemu), na Nuru Mhina ambaye baadae aliolewa na Kabeya Badu ambaye ni muimbaji katika bendi ya Wazee Sugu. Trumpet Ray Mlangwa magitaa John Kitime na Kawelee Mutimwana,

Wednesday, June 16, 2010

Saba saba 2

Kama ambavyo niliwataarifu ni kweli wanamuziki wa zamani wamepania kufanya show moja ya pamoja siku ya Sabasaba katika ukumbi wa Karimjee. Pia imeonekana shughuli hii iwe inafanyika kila mwaka na ilenge kuwa tamasha la muziki la kila mwaka hapa Tanzania Bara. Wanamuziki wamekuwa wakifanya mazoezi ambayo kwa kweli yatawafurahisha wapenzi wa muziki wa Tanzania. Nawaletea picha mbalimbali za wanamuziki waliomo katika mazoezi hayo nina uhakika mtakuwa mnawafahamu wengi
Mwanzo