Taratibu za akina mama kucheza show zilikuwa zikienda sambamba na shughuli nyingine za muziki kwa miaka mingi sana. Nimebahatika kukutana na akina mama wawili ambao walikuwa katika ngazi za juu za uchezaji miaka hiyo. Chini kushoto ni Maida Lwambo, yeye alianza shughuli za sanaa 1973, katika kikundi cha sanaa cha Magereza akishiriki , sarakasi na maigizo, mwaka 1977 akahamia kikundi cha sanaa cha Urafiki akiwa kama muimbaji katika kwaya, na mwaka 1979 hadi 1981 alikuwa akicheza show Orchestra Maquis Original, akahamia kwa miezi michache kwa Doctor Remmy,kisha kati ya 1985 mpaka 1988 alikuwa Orchestra Safari Sound(Dukuduku), na hatimae akarudi Maquis mpaka alipostaafu kucheza show. Kulia ni Anna Mganga, alieanza sanaa katika kikundi cha Tanzania Breweries mwaka 1974,akajiunga na kundi la sanaa la Bora Shoes, na hatimae mwaka 1981 akajiunga na Maquis, kwa muda mfupi mwaka 1983 alihamia OSS, lakini alirudi tena Maquis mbapo alikaa mpaka 1993, alipoacha kucheza show. Hawa wadada walikuwa ndio wanatikisa jiji katika fani yao miaka hiyo.
YOUTUBE PLAYLIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Huyu dada Maida ndie yule alieimbwa katika muziki wa Maida mwanamke, mapenzi yangu umeharibu, kama ndio yeye nimefurahi sana kumuona
ReplyDelete