Tangazo jingine la dansi la miaka hiyo ambalo nina uhakika litaleta kumbukumbu kwa wapenzi wa Maquis wa enzi hizo za Mtindo wa Telemka Chekecha Scania LBT III, wakati huo gari za Scania ndizo zilikuwa maarufu nchini na Scania LBT III ilikuwa gari yenye saiz kubwa kuliko zote, na ndio yenye kusifika zaidi, karibuni tena wapenzi wa White House mchangie, mambo yalikuwa mazito chini ya uongozi wa Chinyama Chiyaza ambae alikuwa mpiga Saxophone katika bendi. Wakati huu Maquis ilikuwa na maendeleo makubwa sana ya kuwa na mashamba, magari, matrekta na hata kuwa na Kota zake pale Sinza Palestina. Hebu angalia majina yaliyopo katika bendi.
YOUTUBE PLAYLIST
Tuesday, March 2, 2010
Chinyama Chiyaza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Mkuu,
ReplyDeleteHiyo link hapo chini inaweza ongeza utamu wa mada hii
http://www.arushatimes.co.tz/2004/27/interview.htm
Aksante anon kwa kutuongezea utamu hapa
ReplyDeleteKitime!
ReplyDeleteHii blog sii ya mchezo. Huko nyumbani kwa wale wanaoujua "muziki' wa nyakati zetu, bila ya shaka wanakila haki ya kujivunia uwepo wa Blog hii ya watu makini.
Huyo anon amelenga maana baada ya kusoma mambo kwenye hiyo link nimekumbuka mbali sana. Vipi mnakuja lini London? tunawangoja kwa hamu sana tupate zenu tungo mpya. nasikia siku hizo mko juu.
Kila la kheri John.
Mkuu, shukurani kwa kutukumbusha mambo ya kina Chinyama Chiyaza wa Marguiz du Zaire. Marekebisho kidogo tu kwenye post yako, nadhani mtindo wao ulikuwa scania LBT 111 na si FBT.
ReplyDeleteEndelea kutuletee habari za vijana wa zamani.