Bendi gani iliimba wimbo- Mali ya mwenzio sio mali yako? Na dongo lilikuwa likielekezwa kwa nani?
YOUTUBE PLAYLIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Waliimba akina Daudi Makwaia na Western Jazz 1966 kwa kuiiga wimbo wa Dr Nico Kasanda. Madongo nafikiri yalikuwa yakielekezwa Kilwa Jazz. Kwa sababu Kilwa walikuwa wanawapiku Western na Dar Jazz kuiga hasa nyimbo za Franco. Wakati huo Duncan Njilima alikuwa ameletewa Rashid Hanzuruni kutoka Tabora Jazz kama soloist mshirika. Hanzuruni alikuwa mahiri sana kuiga solo ya Kasanda.
ReplyDeleteMheshimiwa rudisha kumbukumbu, hili dongo lilikuwa la Kilwa wakiimbwa na Dar Jazz kutokana na wao kuringia ukumbi wao siku hizi maarufu Kwa Madobi pale Jangwani karibu na Klabu ya Yanga. Kilwa walikuwa wampepanga tu ule ukumbi.Ila maelezo yako mengine ni matamu sana. Maana baada ya muda si mrefu nadhani Duncan Njilima na wenzie walianzisha bendi ya African Quilado.
ReplyDeleteNa upigaji gitaa wa Hanzuruni ukiwa na uimbaji wa Daudi Makwaiya unasikika mpaka leo kwenye ule wimbo walioiga kwa African Fiesta..Napenda nipate lau nafasi