Swali la leo......... Bendi gani ilipiga wimbo wa Banchikicha? Kwa msaada tu bendi hiyo ilishinda mashindano ya Bendi Bora Tanzania 1973
YOUTUBE PLAYLIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Sun Burst!
ReplyDeleteNi SUNBURST
ReplyDeleteWalikuwa ni SUNBURST
ReplyDeleteKwangu mimi swali ni gumu naona tumuachie MtiMkubwa.
ReplyDeleteHaswa...bendi hii ilikuwa na enzi zake lakini ikafanya makosa ya kufanya safari ya kwenda Msumbiji na ikatokomea, lakini ilikuwa bendi ya vijana iliyoanza kupanda ngazi nyingine katika ulimwengu wa muziki wa aina yake
ReplyDeleteMkuu,
ReplyDeleteNaomba safu ya wanamuziki wa Sunburst!
Sunburst walikuwa wanaingia katika anga ya crisscross music kama Osibisa. Walikuwa wanachanganya miziki ya kiasili na ya kisasa ya Kiafrika na elements za jazz, rock, funky, latin na kila kitu kilichoweza kuchanganywa kwenye mseto ule. Then mseto ukiwiva utamu unaotoka humo lazima uukubali tu hata ukiwa mbishi kama mtu wa Kigoma!
Wakati ule Afro 70 pia walitunga baadhi ya nyimbo zao katika mtindo huu wa crisscross.
Watafiti, Chezimba na hata Tanzanites pia walipiga Crisscross katika tungo zao.
TATUNANE walikuja kuibuka tena kwenye miaka ya '90 na mtindo huu huu wa crisscross. Walipanda chati haraka sana katika anga za kimataifa na hata nyumbani hususani kwa audience ya wenye sikio la kimziki na "expatriate community". Sina uhakika lakini nadhani TATUNANE ndiyo bendi pekee ya Kitanzania kushinda tuzo ya kikweli kweli ya kimataifa, Decouverters 91 inayoandaliwa na Radio France International. Mkuu, hebu imagine unashinda tuzo ilyoandaliwa na Radio France International tena bendi toka non Francophone country!? Unbelievable!?
Vijana wengine wa Tanzania waliotohoa mtindo huu kwa sasa ni Afrikali. Katika moja ya safari zake nyingi za ughaibuni Ankal Muhidin Michuzi aliniletea zawadi ya CD nyingi tu ikiwemo ya Afrikali. Nimewasikiliza hawa vijana na nimekubali kazi yao. Halafu wamevumbua wapi pa kuegemea kimziki. Muziki wao umeegemea kwenye mapigo ya Sindimba na uimbaji wa Kimakonde. Duuh, sallalleh! Una raha huo.
Nawaheshimu Wamakonde kwenye anga za muziki. Nilipokuwa kijana nilikuwa muhudhuriaji mzuri sana wa maonyesho yao pale kwenye mbuyu ilipokuwa Drive Inn Cinema palipojengwa Msasani Club na Ubalozi wa Marekani ilikuwa kila Ijumaa mpaka Jumapili jioni Wamakonde au Wanyasa walikuwa wanakutana kucheza na kuimba. I don't know where these people have moved to since the construction of Msasani Club and American Embassy?
Pia pale nyuma ya nyumba za jamaa wa usalama wa taifa kuelekea walipotaka kujenga studio za TFC na makaburini kwa Wahindi nyuma ya kijiji cha Makumbusho kulikuwa na kijiji kinaitwa Kimong'onyole nadhani mpaka leo kuna mkidigi wa Wamakonde kila weekend. Napenda sana kwaya/Acapella za kinamama au kinababa au mchanganyiko wa kinamama na kinababa wa Kimakonde. Unaweza ukasinzia huku umesimama wakati unawasikiliza.
Ngoma za Kimakonde ni nzuri sana kuanzia upigaji hadi uchezaji. Wanatune fulani ya vinganga (ngoma ndogo)vyao na fimbo wanazopigia huwa nyembamba sana kwa hiyo hutoa sauti/pitch ya juu kama wanapiga mbao kavu. Halafu mtonya (ngoma kubwa ya kuongozea wapigaji, waimbaji na wachezaji/leading drum) huwa wanauwekea bomba kubwa la plastiki kwa nyuma ambalo linakuwa lina amplify mdundo. Halafu wajanja sana wapiga mitonya huwa wawili au watatu au zaidi lakini yule anayekuja mbele ndiyo mnakuwa mnafikiri zile solo zote anapiga pekee yake kumbe wakati mwingine huwa ana mime tu hapigi kweli. Halafu kuna bomba la chuma na nondo vinavyopigwa kwa nondo kutia harmony. Aaarrggghhh, muziki unaotoka hapo hata uwe hujui muziki kiasi gani utakubali tu!
Tukirudi kwenye crisscross Devadip Carlos Santana naye nadhani ana aina yake ya crisscross music. Au siyo?
hay mabo ya wakubwa hayo
ReplyDeleteMkuu,
ReplyDeleteUjumbe wangu wa kwanza uliupata?
upi huo?
ReplyDeleteDa Mija,
ReplyDeleteUnajuaje kama anon
February 28, 2010 10:22 PM na March 1, 2010 6:41 AM siyo MtiMkubwa? Inawezekana akawa yeye!