YOUTUBE PLAYLIST

Friday, July 29, 2022

BASATA INAPOKEA KAZI ZA KUHAMASISHA SENSA


 

TWANGA PEPETA KISIMA CHA BURUDANI KILA IJUMAA MAWASILIANO PARK

 

Vokali kali toka kwa Charles Baba Kingunge, akiwa na wakali wenzake wa Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani, kila Ijumaa huwa zinasikika Mawasiliano Park Ubungo jirani kabisa na jengo yalipo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania yaani TCRA kuanzia saa mbili kamili usiku. Unakosaje?



 


Wednesday, July 27, 2022

RATIBA YA BONGO BEATS BAND


 ALHAMISI --- KIBOZONE MARAMBA MAWILI MBEZI

IJUMAA--- KALAMBEZI BAR UBUNGO TANESCO 

JUMAMOSI ---  MAGIC LOUNGE KWA LIPELANYA MBEZI MSAKUZI 

JUMAPILI ---DAGAA DAGAA UBUNGO KIBO 

KARIBUNI WAPENZI WETU,

 BABA AMEONDOKA MTOTO AMEBAKI, KAMA ZAMANI.

UTAENDA KUSTAREHE WAPI






 

Tuesday, July 26, 2022

DEKULA BAND YASHIRIKI FEST AFRIKA FESTIVAL YA FINLAND

Dekula Kahanga Vumbi na Menard Mponda mara baada ya onyesho la nguvu la Dekula Band

 Bendi kongwe yenye maskani yake katika jiji la Stockholm kule Sweden, siku ya tarehe 18 Juni 2022 ilitumbuiza katika tamasha la Kimataifa la Fest Afrika Festival, lililofanyika Tampere Finland.
Tamasha hili linalo endeshwa na Mtanzania anaeishi Finland, Bwana Menard  Mponda, ni tamasha la miaka mingi, ambalo limewahi kualika hata bendi kadhaa kutoka Tanzania zikiwemo Yamoto Band na Extra Bongo Band.


Dekula Band jukwaani.

Kwa habari zaidi za tamasha la Fest Afrika Festival ingia
FESTAFRIKA

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...