YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, February 3, 2010



Tancut Almasi Orchestra, bendi iliyokuwa namakazi yake Iringa kuanzia 1987, ilikuwa chini ya Kiwanda cha kuchonga almasi cha hapo Iringa, Diamond Cutting Company. Bahati mbaya wengi ni marehemu. Kutoka kushoto Buhero Bakari inasemekana ni mganga wa dawa za asili kwa sasa,marehemu Kyanga Songa, Kasaloo Kyanga yupo Dar anaendelea na muziki,Kabeya Badu, yuko na King Kiki na wazee sugu, Marehemu Kalala Mbwebwe, Abdul Mngatwa, yuko Iringa ameacha muziki, Akuliake Salehe aka King Maluu yupo Dar anaendelea na muziki

Tuesday, February 2, 2010

Hao si wengine bali ni wanamuziki wa The Revolutions, ambayo sasa inajulikana kama The Kilimanjaro Band aka Wananjenje. Pichani kutoka kushoto, Juma Omary(Drums/uimbaji),Mohammed Mrisho (Gitaa/uimbaji), Mabrouk Omary( Mwimbaji), Waziri Ally (Keyboards/ uimbaji), Marehemu Chuky,Keppy Kiombile(Bass /Uimbaji).Tangazo mojawapo la Kilimanjaro Band katika moja ya safari za Oman

UMUHIMU WA KULIPIA MATUMIZI YA MUZIKI

Ukitunga wimbo na ukiiweka katika hali ya kushikika mara hiyo unaanza kupata haki zote za wimbo hiyo. Wimbo ni mali itokananyo na ubunifu hivyo moja kwa moja unapata haki zinazostahili kutokana na mali hiyo na ni mali yako kama vile mali nyingine. Mara wimbo utakapokuwa tayari kutumika ni muhimu kusajili katika sehemu husika ili uweze kupata ulinzi na stahili zitakazopatikana kutokana na mali hiyo. Kuna haki za aina mbili, Performance Rights na Mechanical Rights.

Performance Rights ni zile haki zitokanazo na tungo ya muziki kutumika hadharani au kurushwa hewani. Hii inajumlisha pamoja na muziki kupigwa na Live Band na, au hata muziki uliokwisha rekodiwa kupigwa hadharani katika sehemu za hadhara kama restaurants, bar, klabu za usiku, kwenye maharusi, na kadhalika. Performance rights pia ni haki zinazoambatisha muziki kurushwa hewani kupitia radio na televisheni. Kutokana na kuweko kwa haki hizi, watu binafsi na makampuni ambayo yangependa kutumia kazi hizo ni lazima wapate ruksa kwa mwenye mali na hivyo mwenye wimbo kupata royalties kila wimbo wake unaporushwa hewani au kutumika hadharani.

Mechanical Rights ni zile haki zinazohusiana na kuweka tungo katika vinasa sauti kama vile kanda CD na DVD. Hivyo mtu au kampuni inapotaka kuweka kazi ya mtu katika kinasa sauti cha aina yoyote kutalazimika kuwepo na ruksa kutoka kwa mwenye mali au taasisi ambayo ina mamalaka ya Mechanical Rights za kazi hiyo. Watunzi hupata Mechanical Rights kwa nyimbo zinaposambazwa na wauzaji.

Ili kurahisisha ufuatiliaji na uratibu wa haki zilizotajwa hapo juu copyright collecting agency au copyright collecting society hutengenezwa ambapo aidha huwa ni chombo kilichobuniwa na watunzi au chombo kilichowekwa kisheria. Chombo hiki hupewa mamlaka na wanachama pia kutoa na kusimamia leseni mbalimbali kwa kazi walizozisajiri

Kwa hapa Tanzania Bara chombo ni COSOTA na Zanzibar COSOZA. Hivi ni vyombo vilichopewa mamlaka kisheria kushughulika kwa niaba ya watunzi kufuatilia haki zao, na kukusanya mafao yatokanayo na kazi hizo.

Ujio wa vinasa sauti bora na mtandao wa intanet unawezesha mamilioni ya watu kuweza kusikiliza wimbo kwa wakati mmoja katika maeneno mbalimbali ulimwenguni. Siyo siri kuwa matumizi kama ringtones ni biashara kubwa sana ambayo wasanii hawajapata manufaa stahili kutokana na mapato ya kazi zao.

Kuweko kwa taratibu za kukusanya mirabaha kuna wapatia fulsa wanamuziki wakongwe kuendelea kupata chochote na hata kutajirika japo nyimbo zao ni za zamani, napengine haziuziki tena. Mtunzi wa wimbo wa Red red wine alikwisha kata tama kimaisha uliporekodiwa upya wimbo huo ametajirika kutokana na wimbo huo.

Kuweko kwa vinasa sauti kumepunguza umuhimu wa kuweko kwa live music, hivyo malipo ya mirabaha inawezesha wanamuziki kupata mafao yao kwa kazi zao zilizotumika badala ya wao. Ni ukweli usiopingika kuwa kuna baadhi ya shughuli haziwezi kukamilika bila ya matumizi ya muziki. Kwa mfano biashara nyingi huongezea motisha kwa kupiga muziki. Mabaa, restaurant, magari ya kusafirisha abairia, na kadhalika. Haya ni matumizi makubwa tu ya muziki.

Shughuli mbali mbali za sherehe kama vile mikutano ya kisiasa, harusi birthday party hutawaliwa na muziki ambao matumizi yake huwa hayalipiwi kinyume kabisa cha haki za kimsingi za binadamu waliotunga nyimbo zinazotumika

Je unajua kuwa ile ule wimbo maarufu unaoimbwa kila wakati wa birthday unalindwa na hakimiliki? Wimbo huu ni mali ya America Online ambao hupata kiasi cha dola milioni 2 kila mwaka kutokana na mirabaha ya matumizi ya wimbo huu. Na wimbo utakuwa mali yao hadi mwaka 2030


Jerry Nashon aka Dudumizi, moja ya waimbaji na watunzi mahiri waliowahi kupita katika anga la muziki Tanzania, nyimbo zake nyingi kama Imakulata (Bima Lee), Thereza, VIP (Vijana Jazz) zilimuweka katika matawi ya juu katika enzi zake

Ujaji wa vinanda aina ya synthesizer ulitoa hukumu ya kifo kwa taaluma ya vyombo vya upulizaji katika bendi nyingi Tanzania. Msondo ngoma wamebakia na msimamo ambao umeweka Bendi hiyo katika ngazi ya pekee kutokana na kubakia na wapulizaji ambao ni wazuri sana, pichani, Mnyupe na Romario katika onyesho moja mjini Tanga
Anajulikana pia kama Zungu, ni mcheza show maarufu wa African Stars Band, huyu ni mtoto wa Salim Willis ambae alikuwa mojawapo ya wanamuziki wa Afro 70 Band. Willis kwa sasa anafanya shughuli nyingine japo bado anaweza kupiga gitaa vizuri kama ilivyoonekana kwenye album ya mwisho ya Marehemu Patrick Balisidya

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...