YOUTUBE PLAYLIST

Tuesday, April 20, 2010

The Rifters 2


Kuna mara nyingine nakosa la kusema nikifikiria hali iliyopo katika ulimwengu wa muziki leo hapa Tanzania. Akina Raphael walikuwa wanawaza nini wakati wanapiga hapa? na ilikuwa nyimbo gani? wanaonekana wana mawazo hawa ni The Rifters

Shaaban Yohana Wanted


Nilikutana na Shaaban Yohana kwa mara ya kwanza katika bendi ya Tancut, ambapo gitaa lake la solo husikika katika nyimbo zote zilizokuwemo katika album za kwanza za bendi ile. Alipiga gitaa katika nyimbo zifuatazo:-
Nimemkaribisha nyoka
Kashasha
Tutasele
Mtaulage
Masafa Marefu
Butinini. Lakini aliniacha Tancut na kwenda Vijana Jazz huko tukakutana tena ambako solo lake linakumbukwa katika nyimbo nyingi kama vile Aza, Ogopa Tapeli,Thereza, Shoga, Malaine nk. Aliacha bendi ya Vijana na kujiunga na Ngorongoro Heroes akatesa sana huko, kisha akatimkia Botswana ambako yuko mpaka leo, muda mwingi akiutumia kama mwanamuziki wa studio.

The Jets


Hawa ndio The Jets (1972), ambao baadae walikuja kuwa STC Jazz, ambayo ndio chanzo cha Biashara Jazz. Waliopo hapa wa kwanza Belino, Raphael Sabuni, Mgoro katika moja ya maonyesho yao. Marijanio Rajab alijiunga na kundi hili, na kuimba wimbo kama.... Ilikuwa usiku wa manane.

Monday, April 19, 2010

Flaming Stars


Familia ya akina Sabuni ilikuwa maarufu sana katika makundi ya vijana wapenzi wa muziki wa Buggy , John , Cuthbert, Raphael wote walikuwa wanamuziki, na kundi la Flaming Stars lilikuwa ni la akina Sabuni. Katika picha hii ya Flaming Stars unawatambua wangapi.?

Afro70 1974

Afro 70 wakiwa Namanga baada ya kutoka Nairobi kupata vyombo vipya. Walilazimika kupiga Namanga ili wapite na vyombo bila bughudha. Unawakumbuka majina?

Dar Es Salaam Jazz-majini wa bahari

Dar Jazz ndiyo kati ya bendi za kwanza nchini. Bado kuna utata wa kumbukumbu kwani katika kipindi cha mwanzo kulikuwekona Coast Social Orchestra inayosemekana ilikuja kuwa Dar Jazz. Wakati huohuo kulikuweko na YMCA Social Orchestra, hivyo ipi ya mwanzo ni kitendawili bado. Pichani ni Dar Jazz 1968. King Michael Enoch akiwa na kofia na nadhani hatupati taabu kumtambua Patrick Balisidya.Kama unavyoona amlifier ya magitaa ilikuwa moja tu, na chini kwenye kiti, kuna amlifier ambayo iliunganishwa kwenye cone spikas, zile spika za chuma tunazoziona kwenye sehemu za ibada na hizo ndizo zilikuwa kwa ajili ya waimbaji.

Tanzania All Stars


Ukitaka kujua umahiri wa wanamuziki enzi hizo ni vizuri ukazisikiliza nyimbo za Tanzania All Stars. Karibuni nitazitundika wote tuzisikilize, katika wimbo wa Samora, Zahir Ally Zoro aliimba Kireno, Jabali aliimba Kiarabu, Aziz Varda Kihindi we bwana wee. Haya tujikumbushe kwa kuwataja majina wote unaowaona hapo juu.

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...