YOUTUBE PLAYLIST

Monday, April 19, 2010

Dar Es Salaam Jazz-majini wa bahari

Dar Jazz ndiyo kati ya bendi za kwanza nchini. Bado kuna utata wa kumbukumbu kwani katika kipindi cha mwanzo kulikuwekona Coast Social Orchestra inayosemekana ilikuja kuwa Dar Jazz. Wakati huohuo kulikuweko na YMCA Social Orchestra, hivyo ipi ya mwanzo ni kitendawili bado. Pichani ni Dar Jazz 1968. King Michael Enoch akiwa na kofia na nadhani hatupati taabu kumtambua Patrick Balisidya.Kama unavyoona amlifier ya magitaa ilikuwa moja tu, na chini kwenye kiti, kuna amlifier ambayo iliunganishwa kwenye cone spikas, zile spika za chuma tunazoziona kwenye sehemu za ibada na hizo ndizo zilikuwa kwa ajili ya waimbaji.

9 comments:

  1. Anonymous12:30

    RIP 'King' Michael Enock. Mambo yako enzi za Dar Jazz na Sikinde yalikuwa si mchezo.

    ReplyDelete
  2. Patrick Tsere16:22

    Hapo kwenye picha yule kulia kwa King Michael alikuwa mpiga bezi mahiri akiitwa Yahya. Alikuwa na mapozi kweli kweli miaka ile ya kuburudisha haswa. Ninamkumbuka mpia ryhthm mahiri akiitwa Maclean. Bonge la baba ambaye akiushika ule mpini wa gitaa la rythm unaona he was really in control.

    Hao Dar Jazz ilianzishwa miaka ya 1937 kama Dar Young Africans na akina Hamisi Machapati na Mzee Muba. Miaka ya 1966 na hiyo ya 68 aliekuwa ampebakia duniani ni Mzee Muba. Maka makuu yao yalikuwa Gerezani mitaa ya Kipata au Kiungani kama sijasahau. Mimi tukiwa wanafunzi tulikuwa tunaenda kuhdhuria mazoezi yao. Kwa kweli Dar Jazz walipotunga nyimbo zao kama 'Kaseme Eliza upesi kama tumeonana...zilipendeza sana. Kwenye vocals alikuwa Juma Akida na Hamisi Nguru. Waimbaji wazuri sana. Baadae AKida akahamia Msondo na Sikinde.

    Patrick Balisdya akipiga second solo. Pia alikuwa kiongozi wa Dar Jazz B.Huko alikuwako mwimbaji Emmanuel Joseph ambaye baadaye alienda Western Jazz (Saboso)akaimba ule wimbo maarufu wa Veronica Dada."Oo oo Veronica dadaaa kama ukinitafuta njoo Kariakoo sikukuu street utanikuta western jazz dadaae'. Kitu kama hicho

    ReplyDelete
  3. Nina picha ya Emmanuel Joseph nitaitundika hapa usiku huu Mungu akipenda

    ReplyDelete
  4. Anonymous21:08

    Tafadhali tuwekee picha ya mkali aliyesahaulika, marehemu Wema Abdallah. Huyu hata Dr Nico Kassanda aliwahi kumvulia kofia kwa ucharazaji wake wa solo enzi za Saboso. Sikiliza nyimbo kama Jela ya Mapenzi, Rosa na Vigelegele ndipo utagundua utaalam wa mkali huyu ambaye ameshatangulia mbele ya haki.

    ReplyDelete
  5. Anonymous23:10

    balozi tuenzi na nyimbo za zamani humu bloguni. Ni wewe pekee tunayekutegemea, tuko nje ya nchi balozi wetu kupata vitu vya nyumbani ni ngumu sana.

    ReplyDelete
  6. BLACKMANNEN05:15

    Dar Jazz ni chimbuko la wanamiziki wengi sana wa Tanzania. Karibu kila mwanamziki wa zamani wa Tanzania alipitia Dar Jazz.

    Ahmed Kipande, Patrick Balisidya, Juma Mrisho, Dancan Njilima, Moshi William (Tx), Juma Akida, Emmanuel Joseph, Hamis Nguru na wengine wengi.

    Mzee (Marehemu) Michael Enock, alipenda kuendeleza wenzake, hakuwa mchoyo wa maendeleo kama ilivyo leo hii kwa wanamiziki wetu.

    Wao (wanamiziki wa siku hizi) kila kukicha ni ugomvi tu na ugomvi mwenyewe ni kugombea "Mabibi" au "Mabwana". Kaaazi kweli kweli.

    This Is Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  7. Patrick Tsere06:33

    John hivi hakuwa marehemu Rashid Hanzuruni ambaye Dr Nico Kasanda alipendezewa na umahiri wake wa kuzidonyoa nyuzi za solo. Ndiyo maana Western jazz walikuwa mabingwa wa kuiga nyimbo za African Fiesta kama vile Kodi ya mwenzio siyo mali yako na nyinginezo?

    ReplyDelete
  8. Anonymous13:20

    Mdau aliyemtaja Wema Abdallah (RIP) hapo juu amenikumbusha jinsi akina Lokassa ya Mbongo walivyodanganywa kuwa nyimbo kama Vigelegele, Rosa na Asha, ambazo waliimba katika albamu yao ya 'Nairobi Night' ya mwaka 1990 zimepigwa na Wakenya wakati ukweli ni muziki wa Tanzania. Nadhani hili lisingetokea kama enzi hizo kungekuwepo na mtandao na blog za kuuenzi muziki wa Tanzania kama hii.

    ReplyDelete
  9. Anonymous20:47

    mdau wa April 22, 2010 3:20 AM, ni kweli kabisaaaaa!

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...