BENDI maarufu ya Ngoma Africa band itashiriki katika burudani
za kukata na shoka zitakazotumbuiza wahudhuriaji wa tamasha la 15
la International African EXPO
Festival litakalofanyikaTübingen,
Ujerumani. Tamasha litakuwa kati ya tarehe 01September - 04th September
2022 Fest Platz, Tübingen, Ujerumani.
Ngoma africa band
watakuwa jukwaani Jumamosi 03 September 2022
Ngoma Africa, ni bendi yenye makao yake Ujerumani na
ilianzishwa mwaka 1993 na kiongozi wa
bendi hiyo Ebrahim Makunja anaejulikana pia kama Kamanda Ras Makunja. Bendi hii
ina wanamuziki wakali kama soloist Christian Bakotessa aka Chris-B, wengine ni
Jo Souza, Matondo Benda, Aj Nbongo, Flora William, Jessicha Ouyah, Vially
Nbongo, na wengio. Bendi hii ina mamilioni ya wapenzi na inajulikana kwa
kupagawisha kwa midundo yake yenye uasili wa Afrika ya Mashariki.
Ngoma Africa imeshaachia CD kadhaa ikiwemo CD yake mpya inayoitwa “BONGO TAMBARARE” , nyimbo mbili hizi "Mapenzi ya Pesa" na "Supu Ya Mawe" unaweza kuzisikiliza ukiingia hapa www.reverbnation.com/ngomaafricaband
No comments:
Post a Comment