YOUTUBE PLAYLIST
Saturday, August 21, 2010
Vijana Jazz enzi za Ngapulila
Kati ya awamu nyingi za Vijana Jazz Band moja iliyoleta changamoto na furaha ni ile awamu ya nyimbo , Ngapulila, Ogopa Tapeli, Adza. Pichani baadhi wa wanamuziki wa wakati huo. Picha ya kwanz a juu- Mzee Joseph Nyerere akiwa na Kulwa Milonge na Hamis Mnyupe, picha ya pili wapiga trumpet marehemu Chondoma, Hamis Mnyupe, na Kulwa Milonge. Picha ya chini ni kundi zima la Vijana Jazz wakiwa na Mheshmiwa Seif Khatib, hapa wanaonekana akina Shaaban Dogodogo, Hemed Maneti,Shaaban Wanted, Abou Semhando na wengine wengi.Kama unavyoona alama za x wengi hawapo tena nasi duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Naikubali hii awamu ya Vijana Jazz. Pale kulikuwa na muziki wa kutosha. Lakini pia marehemu Jerry Nashon alileta uhai mzito alipojiunga na Vijana. Vibao kama Top Queen hadi leo ni moto wa kuotea mbali. Pengine huo ndio ulikuwa mwisho wa Vijana Jazz ya ukweli. Siku izi wanaimba kwaya kama TOT wala wanachopiga hakieleweki ingawa naona wamejaruibu kurudia baadhi ya nyimbo studio. Vijana Jazz na Washirika Tanzania Stars walikuwa mwisho wa matatizo. Nilipendelea sana hawa maana walikuwa kwenye utoto wangu. Hii haimaanishi JUWATA, DDC, OSS na marquis hawakuwa vyema, ila nyakati zangu hao ndo walikuwa juu.
ReplyDeleteNaikubali hii awamu ya Vijana Jazz. Pale kulikuwa na muziki wa kutosha. Lakini pia marehemu Jerry Nashon alileta uhai mzito alipojiunga na Vijana. Vibao kama Top Queen hadi leo ni moto wa kuotea mbali. Pengine huo ndio ulikuwa mwisho wa Vijana Jazz ya ukweli. Siku izi wanaimba kwaya kama TOT wala wanachopiga hakieleweki ingawa naona wamejaruibu kurudia baadhi ya nyimbo studio. Vijana Jazz na Washirika Tanzania Stars walikuwa mwisho wa matatizo. Nilipendelea sana hawa maana walikuwa kwenye utoto wangu. Hii haimaanishi JUWATA, DDC, OSS na marquis hawakuwa vyema, ila nyakati zangu hao ndo walikuwa juu.
ReplyDeleteMimi naomba msaada kwa yoyote ajuaye, Hivi huu wimbo wa Ngapulila aliutunga nani? na pili ukiusikiliza huu wimbo mwanzoni kuna muimbaji anasema hey ngapulila;Namkumbuka vizuri sana alikuwa ana cheza ile mbaya hivi ni nani kwa jina na yuko wapi hivi sasa, Maana hakukaa sana Vijana jazz I have no idea why, Help please,
ReplyDeleteBig fan,Lilian,Orlando,Fl.
Nadhani unamuongelea Adam Bakari aka Sauti ya zege. Yeye ndie alikuwa mwimbaji wa wimbo huu wakishirikiana na Eddy Sheggy, na ndie alikuwa anacheza sana. Bahati mbaya kwa sasa ni marehemu
ReplyDeleteHivi Kitime yule jamaa alikuwa anapuliza trumpet Everist Bitto yupo wapi nakumbuka mara ya mwisho nilimwona Vijana jazz akitokea Dar international
ReplyDeleteKwa bahati mbaya Evarist Bitto alikwishafariki miaka mingi iliyopita
ReplyDeleteMtu ambaye sikutegemea kabisa kumuona humu ni Mzee Joseph Nyerere. Lakini inaonyesha jinsi gani muziki unagusa watu wote, wa kila rika.
ReplyDeleteNa Mzee wetu tunamkumbuka alikuwa mpenzi mkubwa wa muziki.
Ile picha ya Patrick Balisidya nimeipata, nitakutumia punde.
Hii group ilikuwa na nguvu ya aina yake, nakumbuka walikuwa wanaweka libeneke pale kinondoni vijana hostel siku ya jumapili mchana, halafu mwimbo wa mwisho wakati bado unapigwa, nusu ya vyombo vya muziki vimeshapakiwa katika fuso au canter ile? Halafu saa tatu,nne hivi, wapo African stereo bar na kuanza show nyigine upyaaa!!!! Hiyo ilikuwa ni energy ya Kitime & co. Au unasemaje Bro?
ReplyDeleteEnzi za Vijana kupiga Kinondoni Stereo Kitime alikuwa bado hajajiunga na bendi hii. Kitime kajiunga mara baada ya recordig ya Ngapulila ambapo Adam Bakari, Eddy Sheggy na Hamza Kalala walikuwa wamehamia Washirika Tanzania Stars.
ReplyDeleteNashukuru kwa kunisahihisha unajua tena ni miaka mingi imepita kwa hiyo ni rahisi kuchanganya mambo kidogo.Unajua kwa zaidi ya miaka 20 nimeweka makazi katika nchi za skandinavia, na mazungumzo haya huku hakuna kwa hiyo hii blog inanikumbusha sana vile vijiwe ambapo maongezi haya ni kawaida. Kuna wakati Hamza Kalala ilikuwa arudi Vijana Jazz na kuendelea na Pamba moto awamu ya tatu. Iliishia vipi?
ReplyDeleteKurudia bendi ya zamani huwa ni ngumu maana watu wapya, muziki umeshakuwa mwingine, alikaa siku chache akaacha
ReplyDeleteBig Up John. ningependa pia ujaribu kutukumbusha mashindani ya kumi bora enzi zile za miaka ya 80's na kuna vibendi vidogo vidogo ambavyo navyo vilitikisa kwa muda kama vile Salna Five Brothers N.k. pale nakumbuka kulikuwa na akina Kapelembe Kokoo na Binki Binsalim sijui wapo wapi kwa sasa hawa jamaa. kama una taarifa zao na wengine wengi wadau tungependa kuzijua.
ReplyDeleteEnter your comment...Vijana JAZZ kwa sasa inapiga Muziki wake wapi na kitu kingine ambacho wazee wetu mlikosea hamkuwa na Foundation ya kuandaaa Vijana Ambao leo hiii wangewez kuukuza huu Muziki wenye asili ya TZ mim ni kijana ila nimejikuta naumia moyoni kwanini sikuzaliwa Zama zenu roho huwa inaniuma kwasababu nasikiliz hizi nyimbo kisha najaribu kurejesha Fikra zangu nyuma Naumia kwasababu huuu Muziki umekufa siusikiii tena wala records mpya hazisikik ila yote haya mliyasababisha wenyewe yamkini mnfekuwa km na Chuo cha kuandaaa Vijana ninauhakika mpk Leo Muziki wa Bandi ungekuwa juuu kuliko Bongo flavor mimi pia Mpaka Leo nataman kuimba Huuu Muziki cha ajabu sijawah kujua na sijui naanzia wapi
ReplyDeleteWananikumbusha Vijana Jazz ilipoasisi mtindo mpya wa "Sagarhumba" wakiwa na nyimbo kama Top Queen, Lumbesa, na nyinginezo nyingi. Sina hakika kama katika kikosi kile kuna aliyebaki tena Vijana Jazz ukiacha Shomari Ally. Wengi wamefariki na wengine walishaondoka kwenye bendi hiyo kama John Kitime, Rashid Pembe na Kulwa Milonge.
ReplyDelete