YOUTUBE PLAYLIST

Tuesday, August 3, 2010

Lister Elia














Huyu ni mwanamuziki mpiga keyboards, zao la Dodoma, kule alikotoka Patrick Balisdya, Anania Ngoliga, Rahma Shally na wengi wengine. Lister mtoto wa mchungaji atakumbukwa sana kwa kazi yake katika bendi ya Sambulumaa lakini baada ya hapo alipitia Afriso Ngoma ya Lovy Longomba na Orchestra Safari Sound wale vijana wa Kimara, na hatimae akatua MK Sound(Ngoma za Magorofani). Hiyo ilikuwa baada ya wanamuziki akina Andy Swebe, Mafumu Bilali, na Asia Darwesh kuhamia Bicco Sound, alitua huko wakati mmoja na Ally Makunguru, Rahma Shally na hivyo kujiunga na Joseph Mulenga , Makuka, Matei Joseph na wengineo. Lister pia ni mtunzi wa vitabu na mwanamuziki ambae amesoma vizuri muziki kwa sasa yuko Japan habari zake za sasa zinapatikana kwenye website yake http://www.listerelia.com/

(Pichani Sambulumaa katika picha kabla tu ya uzinduzi wa bendi hiyo, picha ya pili Lista akiwa OSS)

19 comments:

  1. Anonymous11:50

    Vitu adimu sana hivi, huyu jamaa nilikuwa namfagilia ile mbaya kweenye keyboard. Wa saizi yake alikuwa Father Kidevu. Katika ule wimbo wa MK Group wa Yaliyopita si Ndwele na MAUMIVU MAKALI amekamua ile mbaya. Yaani unamsikia Kasongo Mpinda na kinanda cha Lister tu vikahanikiza. "kwani maisha yana maana kubwa sana kwetu eh..yaliyopita si ndwele tugange yajayo". Kuna wakati palikuwa namadai kipindi kile cha 90 kwamba Lister alinyakuliwa MK Group kutoka kwa Nguza lakini Nguza alikanusha. Nakumbuka kichwa cha habari cha habari cha gazet la Uhuru kilisomeka: "Lister hakuwa wangu - Nguza".

    ReplyDelete
  2. Anonymous00:42

    Huyu jamaa ni inspirational kwa new generation ya musicians. Lister katoka mbali na kikubwa haachi kujifunza! He always learns new things;something many of today's Bongo Flava musicians don't want to DO!

    Bro Lister, endeleza libeneke! Mimi siyo mwanamuziki lakini ni mdau wa muziki and a friend and no doubt, I have learned a few things from you since I knew you!

    Keep up good work.

    Mdau UK.

    ReplyDelete
  3. Anonymous11:55

    Sio kuwa namsifu ila kwa Lister ameprove kuwa kipaji hutoka moyoni.

    Yeye anaweza kupiga kila chombo nadhani hata kuimba.

    Vijana changamkeni, those days Lister anajifunza magitaa, vinanda etc vyombo vya mziki vilikuwa vichache mno....pengine hata magitaa ya kuchonga kwa mafundi seremala, nyuzi za waya break ya baskeli.

    Leo vifaa kila kona kuna duka cha ajabu katika wanamuziki wa sasa kumi labda mmoja anataka kujua zaidi anachokijua katika muziki kwa sasa...........kama mnavyoiga kuvaa kwa wanamuziki wakubwa....chimbeni na undani wa vipaji vyao hasa katika kutanua uigo wa ufahamu wenu wa muziki.

    ReplyDelete
  4. Anonymous12:14

    Lister Elia ni mwanamuziki msomi na kiwango chake ni cha kimataifa,hapigi miziki ya kibongo pekee.Ukifuatilia vitu vyake kwenye tovuti yake utamkuta kila mahali kuanzia kwenye miziki ya kigeni ya jazz hadi kwenye miziki ya kawaida ya kibongo.

    Uandishi wake wa vitabu vya muziki kuisaidia jamii ya wanamuziki wa ki-Tanzania unaonyesha nia yake njema ya kufanya mapinduzi ya ki-muziki kwa wamuziki ambao hawakubahatika kupata elimu ya muziki.

    Ni mwamuziki aliyetulia na hata anapohojiwa na wanahabari hapa nyumbani anaporudi kupumnzika, majibu ya maswali anayoulizwa huonyesha upeo wake wa kujua mambo.

    Bwana Lister endelea kutoa mchango wako wa kitaaluma kwa wanamuziki wenzako,ni wengi wanaofaidika na mafunzo yaliyo kwenye vitabu vyako mimi nikiwa mmoja wao. 

    ReplyDelete
  5. Anonymous16:28

    Hivi huyu Lister Elia si ndio yule Lister Nkuhuwala? Au sio mzee Mwakitime?

    Maselepa "Kama Zamani"
    Zamani Sports Club
    Kimara Suka

    ReplyDelete
  6. Anonymous17:15

    Picha ya juu kulia kabisa namuona Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kikii', lakini sikumbuki kama aliwahi kupigia Sambulumaa. Labda kumbukumbu zangu hazinitendei haki. Naomba Balozi unielimishe katika hili.

    ReplyDelete
  7. Macho yako hayakudanganyi, ni King Kiki alipitia Sambulumaa

    ReplyDelete
  8. Anonymous18:35

    Hapo Lister ananikumbusha mavazi yetu tulipokuwa vijana wadogo miaka ya 80. Ulikuwa unapiga shati lako jeupe, suruali nyeusi, soksi nyeupe na viatu vyeusi. Suruali ilikuwa shati iwe fupi kidogo ili soksi zionekane. Those were the days.

    ReplyDelete
  9. Anonymous12:24

    Kwa umri wangu na kumbukumbu zangu ambazo ninaamini ni sahihi Lister Elia alikuwa anatupigia kinanda wakiti tukiimbia kwaya ya UVUKE pale dodoma. Ilikuwa siku ya masikitiko sana na kumlaani shetani enzi hizo pale tulipoambiwa ati lister ameamua kwenda kupiga muziki wa dansi. apakutosha . Lakini kumbe mungu alikuwa anamuandalia bright future. Mwaha lister uwalamsee woseeee kuko!

    ReplyDelete
  10. Mashaka06:21

    swali langu ni la kimuziki halihusiani na lister ,Linahusiana na marehemu Moshi williamu nimesikiliza vizuri pamoja, na kumtaja katika nyimbo nyingine lakini ktk hii albam ya mwisho wimbo kama nimebadilika nini wa karama marehemu amemtaja mtu anaitwa majaliwa mara nyingi na kama anasisitiza ukisikiliza kama anahuzunika pia huyu majaliwa ni nani ?na kama unaufahamu alikua na ukaribu gani? na marehemu asante mzee kitime kazi nzuri.

    ReplyDelete
  11. Majaliwa kamtaja katika nimbo nyingi sana. Huyu alikuwa rafiki yake aliyekuwa akifanya kazi Nzega na kuhamia Ifakara. Yeye ndiye aliyewezesha kuweko kwa kundi la Bana Mwambe. Pia ana mdogo wake ambae ni mwanamuziki anaeendeleza Bana Mwambe baada ya kifo cha Moshi William

    ReplyDelete
  12. Mashaka09:21

    ASANTE SANA MZEE KITIME KILA LA HERI

    ReplyDelete
  13. Anonymous17:14

    Nilibahatika kumuona huyu kijana Lister Elia akifanya vitu jukwaani hapa Zanzibar wakati wa tamasha la muziki la SAUTI ZA BUSARA.
    Nilivutiwa na upigaji wake wa kinanda pamoja na uchaguzi wa sound alizokuwa anazitumia.

    Ana spidi ya hali ya juu vidoleni na ubonyezaji wake wa vipande vya kinanda unaleta mlio au sound iliyo tajiri na isiyofanana na wapigaji wa kinanda tuliowazoea hapa bongo.

    Anajiamini jukwaani,anajituma na pia anaimba kusaidia safu ya waimbaji.Kwa hakika kijana huyu ni role model kwa wanamuziki wapiga vinanda wa hapa nyumbani.

    Lister usilewe sifa,kaza buti katika shughuli zako....tuko nyuma yako kaka.

    ReplyDelete
  14. Anonymous17:30

    Balozi,ni kweli Lister alipitia Afriso? nimemfuatilia miaka mingi lakini sikumbuki kama alipitia Afriso.

    ReplyDelete
  15. Anonymous17:42

    Huyo wa nne kulia aliyeweka gitaa begani ni Nguza Viking kama sijakosea.

    ReplyDelete
  16. Kwataarifa nilizo nazo alipitia huko kwa muda mfupi. Nitajaribu kukutana na wanamuziki aliokuwa nao wakati huo nipate uhakika

    ReplyDelete
  17. Anonymous19:53

    Anony wa hapo juu ya balozi,hujakosea.Aliyeweka gitaa begani si mwingine ni Nguza Viking.

    Ikumbukwe kwamba wakati Sambulumaa inazinduliwa Diamond Jubilee,ilikuwa chini ya uongozi wa Nguza Viking.

    Mdau,Finland.

    ReplyDelete
  18. Anonymous13:31

    Ama kweli nimefurahi sana kupata habari hizi kuhusu waimbaji kama Lista. Mi ni fan mkubwa sana wa waimbaji wa Tanzania. Ni mkaaji wa Malindi, Kenya.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...