YOUTUBE PLAYLIST

Tuesday, May 18, 2010

Afro 70

Afro 70 wakati wako juu. Waimbaji Monte Gomes na Steven Balisdya (alikuwa pia anapiga drums), Dick Unga,Shabby Mbotoni(alikuwa pia anapiga saxophone na bass). Magitaa Patrick balisdya, Owen Liganga(second solo), Salim Willis(second solo), Jack Matte (rythm guitar),Charle Matonya(Bass guitar), Paul Mdasias (drums), Didi Musekeni(Hayuko pichani mwimbaji).

7 comments:

  1. Anonymous23:47

    Je, kuna mtu anajua Dick, Shabby na Salim wako wapi.? Nadhani sijawaona tangu mwisho ya miaka ya 80. Jimmy.

    ReplyDelete
  2. Salim yuko Chang'ombe Bora mtaa wa Majimaji na bado anapiga gitaa siku akifurahi,Dick yuko Mtwara, Shaby yuko Dodoma

    ReplyDelete
  3. Anonymous10:58

    Ahsante sana mkuu kwa update hii ya watu niliokuwa ninafahamiana nao katika ujana na kwa kazi nzuri ya blog hii. Jimmy.

    ReplyDelete
  4. Anonymous12:01

    Kwanyongeza tu Shebby Mbotoni alipata kuwa mheshimiwa diwani wa kata ya moja huko dodoma. Bado ni mtanashati sana japo inasadikiwa kwa sasa ni Babu wa wajukuu watatu wazuri sana ila mustach na suruwali zake za juu ya kitovu bado hajasahau huyu kijana mwenzetu wa zamani

    ReplyDelete
  5. Perez14:35

    "...Nambie kweli kaka mzigo huu sasa nitauweka wapi...,

    Nikijiua leo naua roho mbili, ee eee.."

    Yaani. We acha tu. Zamani tulifaidi bwana!

    ReplyDelete
  6. Anonymous18:20

    Dk.John,
    ahsante,hiki ndicho kilikuwa kikosi cha Afro 70kilichopendwa na kila mtanzania,walikuwepo kila pahali hata vijiharusi vya mitaa ya uchochoroni wakiitwa watakuja kutupa furaha kwa mziki wa Afrosa
    Mickey Jones

    ReplyDelete
  7. Anonymous22:20

    Balozi, sasa naachana na mablogu yote feki ya bongo nakufuatilia wewe tu. We ndiyo balozi wetu kweli, tuletee miziki balozi. Je umeshapata ujanja wa kutuwekea baadhi ya nyimbo tuzisikilize jamani, tupo mbali na home.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...