YOUTUBE PLAYLIST
Sunday, May 9, 2010
Abdalla Gama
Kwa wapenzi wa DDC Mlimani Park, jina la Abdallah Gama ni jina muhimu katika historia ya bendi hiyo. Mwanamuziki huyu mpigaji wa gitaa la rythm alipata umaarufu zaidi baada ya wimbo wa uliotungwa na Assossa -Gama, ambao mpaka leo bado unafurahisha sana. Gama na wenzie kama Joseph Mulenga, Abel Balthazar, Cosmas Chidumule chini ya King Michael Enoch waliweza kutunga na kutengeza nyimbo ambazo bado zinaleta burudani miaka thelathini baada ya kutungwa. Abdallah Gama tena atakumbukwa kwa kazi zake alipokuwa BimaLee wakiwa na watunzi kama Jerry Nashon, Shaaban Dede, solo la Mulenga , nba besi la Mwanyiro, hapo ilikuwa utamu kolea. Pichani Gama(mbele)akiwa na mpiga gitaa mwingine Huruka Uvuruge ambae sasa yuko Msondo, na mpiga drum Matei Joseph ambae kwa sasa anendesha bendi yake African Minofu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Asante sana Kitime,kumbe ni Assosa ndiye katunga nyimbo Gama amakweli muziki hauna mipaka.
ReplyDeleteMzee Minofu Matei Joseph kachangia kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la Muziki wa Dansi na Drums yake...
God bless you Matei and Kitime
"Gama na wenzie kama Joseph Mulenga, Abel Balthazar, Cosmas Chidumule chini ya King Michael Enoch" This is like an All-Stars Team. No wonder waliandika / kutunga na kurekodi nyimbo bora kabisa.
ReplyDeleteSwali nililonalo ni kuwa NI KWELI KUWA MAMBO YANABADILIKA KUELEKEA KUBAYA AMA NI SISI MASHABIKI TUNAONG'ANG'ANIA YA KALE?
Tazama Muziki. Licha ya kuonekana kuwepo kwa teknolojia, kuwepo kwa zana saidizi na mambo mengine meeengi, bado wengi wanakubali kuwa muziki wa zamani ulkikuwa bora. Iwe ni Dansi ya Tanzania, Reggae n.k
Na tunapoelekea kwenye World Cup, watu wanawaona wachezaji bora na vijana wanaofanya ambayo hayakuweza kufanywa na weengi zamani, lakini bado hawawaweki kundi moja na kina Pele.
Kila nisomapo hapa, nakumbuka BURUDANI MURUA NA YA HAKIKA iliyotolewa na na wanamuziki hawa na kisha nawaza "ni lipi ambalo wasanii wetu wa sasa wanaweza kuunganisha ama kuchanganyana wale wa kale kupata UHONDO ambao twaonekana kuukosa?"
ASANTE SAANA Uncle Kitime kwa kumbukumbu hizi
John!
ReplyDeleteHivi string master Abdalah Gama yupo hai mpaka leo? na anafanya nini na wapi??
Binafsi naona tofauti kubwa iliopo kati ya muziki wa zamani na wa sasa inakuja katika utunzi. Ni kweli muziki wa zamani ni mtamu sana ila muziki ule ule una itilafu yake pia. Utakuta kama ukisiliza nyimbo za zamani, kuna kipengele (beats in a song) midomo ya bata ama trumpets hazistahili kuwepo lakini bendi inatia tu kisa bendi zingine zote zinafanya hivyo, matokeo yake mtu unabaki kufikiri hawa watu walikuwa wanafikiria nini hapa?
ReplyDeleteTungo za sasa, kwa kweli nyingi ni za ngumbalu, ila beats tuko juu sana kulinganisha na zamani. Ninachowashauri wanamuziki wetu ni kuwa makini katika tungo, watunge nyimbo tamu kama za miaka ile ya 47 ila beats za kisasa kama tulivyo.
Nataka ni mjibu anonymous 14:42 namba 4,mbona unavungavunga vitu ambavyo hujui?jaribu kuuliza ujue ukweli...
ReplyDeleteBeats:Muziki wa zamani ulikua unarekodiwa katika Tracks 2 ya Studio RTD,Bendi zilikua zinatumia vyombo vyao(vingine vibovu ao vizuri)angalau Sound ilikua nzuri.
Muziki wa leo(Bongo Fleva) mmebahatika kutumia Teknolojia ya kisasa, yaani mnachukua Sampo za Beats za Kimarekani kutoka program za computer kama vite Kyubesi n.k...
Ushauri:Vijana wa leo mjifunze kupiga vyombo kama Drums,Congas,Sax,Tompett,Guitar,Keyboard,acheni programation za computer,pigeni LIVE katika Studios ili Muziki wenu uvuke mipaka...
Muziki wa zamani ulivuka mipaka,mfano:Remmy,Mbaraka,3-8...
Ahsanteni
GAMA NASIKIA YUPO KAMA SIKOSEI MBAGALA,LAKINI KACHAKAA KIMAISHA NA HUO MUZIKI HANA MPANGO NAO KWA MAANA YA KUTOLISOGELEA KABISA JUKWAA LA SIKINDE PALE DDC KARIAKOO AMBAPO HUWA NAPITAPITA SIKU ZA JPILI,HUWA NAENDA HAPO DDC AMA MSONDO SANASANA AMBAKO NDIPO YALIPO MAPENZI YANGU,WENYE DATA ZAIDI ZA GAMA MSAADA TUTANI,
ReplyDeletesayz HAJI SENETA WA MSONDO
Huyo mdau wa juu aliyeyazungumza ni ya kweli. Nakubali kuwa zamani kulikuwa hakuna technology kama ya leo, lakini pia ikumbukwe, kuwa ni kweli bendi nyingi zilitumia midomo ya bata ama trumpets hata sehemu isiyostahili. Tungo za zamani ni kiboko kweli, yaani kiboko ile mbaya. Kinachosikitisha hapa TZ ni kule kubezwa muziki wa fleva kujifanya sisi ni wamarekani weusi. Kwa kweli huu ni ujinga, ebu angalieni vijana wenyewe wa fleva. Utakuta mtu anaimba wimbo (hauna maana) anatia lafudhi ya kiingereza ili aonekane mmarekani ama mgeni kwa hiyo lugha. Muziki wa fleva ni ulostishaji vipaji na ndiyo maana utakuta wasanii wake hawadumu na hata ile ladha ya muziki wao baada ya muda uisha kabisa. Bongo dansi ni muziki wetu wa kujivunia na ni kitambulisho chetu nje ya TZ ila si fleva!
ReplyDeleteNaungana na anonymous 23:01 na 09:31 Ukweli ni kwamba vijana wa sasa hawana moyo wala nia y akujifunza muziki wa kina sababu ya utandawazi. Zamani wanamuziki walilazimika kuwa wabunifu sana na wajuzi sana vyombo hasa kwa sababu ya technology ndogo. kila unachokisikia katika muziki wa zamani ni kazi halisi iliyofanywa na mkono wa mtu. hakuna msaada computer wala kazi za copy and paste. Nachelea kusema maendeleo ya technology yasipotumiwa kwa maarifa yanashusha ubora wa kazi za muziki.
ReplyDeleteGama yupo, anaishi maeneo ya Pile Temeke lakini hali yake inasikitisha amekuwa mlevi wa kupindukia na inaelekea hana mwelekeo kabisa wa muziki inasikitisha kupoteza kifaa kama Gama. watu wa councelling labda jaribuni kumuokoa.
ReplyDeletenionavyo mimi tunakoelekea ndio kubaya. mie si wa zamani lakini sio wa kisasa hihivyo. wimbi la teknolojia la sasa lingewakuwa wanamuziki wa zamani na spirit yao ya kutunga na kupiga muzika pangekua hapatoshi. muziki wa siku hizi ni wa kibiashara zaidi kuliko burudani. nia ya wanamuziki wa zamani ilikuwa ni kuburudisha tofauti na dhima ya wa sasa (to be precise waimbaji, sio wanamuziki) ambayo ni pesa. ndio maana leo tunaambiwa na anon wa saa 05:24 kuwa gama kachoka ile mbaya.
ReplyDeletekasoro ndogo zinazojitokeza za muziki wa zamani ni vyombo na ubinafsishaji wa recording kwa kituo kimoja
SASA KWANINI MIZIKI YA BONGO FLEVA(Uganda,Kenya na Tanzania) HAIPIGWI KATIKA REDIO ZA KIMATAIFA?
ReplyDelete1.NI KWAMBA SAMPO ZA BEATS,INSTRUMENTAL,WANA ZI DOWNLOAD KATIKA MTANDAO WA KIMAREKANI.
2.HAUWEZI KUPIGWA SABABU WATADAIWA HAKIMILIKI(mfano wa nyimbo Bullet)
3.WAZUNGU YAANI REDIO ZA KIMATAIFA WANAPENDA KUSIKIA KITU ORIGINAL SIO CHAKU IGA