Mzee Joseph Nyerere alikuwa mpenzi sana wa Vijana Jazz Band. Nakumbuka siku za Jumapili ambapo Bendi ilikuwa na onyesho lake lililoitwa Vijana Day mara nyingi ungemkuta pembeni akisikiliza muziki na pengine akiomba special request. Ilikuwa ni burudani pale ambapo aliamua siku hiyo kucheza maana alikuwa na staili ya peke yake iliyofanya mtu apende kumuangalia. Historia inasema alisoma Tabora Boys na alikuwa Band Master wa bendi ya shule na alipendwa sana kutokana na mbwembwe zake alipokuwa akiongoza na kifimbo cha Band Leader. Mzee Joseph aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa TANU Youth League. Pichani akiwa jukwaani na Marehemu Hemedi Maneti katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni, kwa mbali nyuma anaonekana Aggrey Ndumbalo akiwa ameshika gitaa na Said Hamisi muimbaji wa Vijana akiwa napiga makofi, wote wamekwisha tangulia mbele ya haki.
YOUTUBE PLAYLIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Yaani wote uliowataja wametangulia mbele za haki, najua Joseph Nyerere na Maneti sikua Aggrey Ndumbalo na Saidi Hamisi pia.
ReplyDeleteHivi Said Hamisi si ndio alikuwa anaweza kuiga vizuri sauti ya Maneti?
RIP Hamisi Saidi aka Misukosuko!
Ndiye huyo haswa misukosuko
ReplyDeleteHivi Balozi, ulitoka lini Vijana Jazz?
ReplyDeleteNiliacha Vijana Jazz mwaka 1995
ReplyDeleteBW.KITIME,NAOMBA KUULIZA. HIVI ULE WIMBO WA VIJANA 'MAANA YA TANGA'....TANGA NI LA MSIBA ..AU KUTANGATANGA. NANI HASA ALIYEANZA KUUPIGA? KWANI KUNA WIMBO EXACTLY KAMA HUO ILA KWA KILINGALA, ULIOPIGWA NA ORCHESTRE VEVE, BENDI YA YULE MTAALAM WA KUPULIZA SAX, VERKEYS KIAMUANGANA MATETA!!
ReplyDeleteKwa kweli nimeshasahau hata melody ya wimbo huo wa Tanga ngoja niusikilize. Huo wimbo wa Verckys unaitwaje?
ReplyDeleteJINA LA WIMBO WA VERKEYS LIMENITOKA KIDOGO...NITAJARIBU KUWASILIANA NA NDUGU YANGU ALIYEKO MWANZA YEYE ANAYO HIYO ALBUM YA VERKEYS YENYE HUO WIMBO..
ReplyDelete