YOUTUBE PLAYLIST
Sunday, April 25, 2010
Akina mama nao- Asia Darwesh
Asia Darwesh ni miongoni mwa wanamuziki wanaoheshimika sana katika jamii ya wanamuziki na wapenzi wa muziki waliowahi kusikia au kufurahia kazi zake. Katika picha hapo juu Asia ambae alikuwa mpiga Keyboards wa kutumainiwa anaoneka picha ya juu akiwa na King Kiki enzi za Double O, na chini akiwa Mk Sound. Asia aliwahi pia kupigia Bicco Stars ambapo yeye pamoja na Andy Swebe na Mafumu Bilali na wenzao (waliihama MK sound), waliweza kuipandisha sana chati bendi hii. Hatimae Asia aliweza kumiliki bendi yake na alipatwa na umauti akiwa na bendi yake ambayo ilifanya vizuri sana huko Uarabuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Nakumbuka nyimbo zake za Bicco zaidi. Nakumbuka walivyokuwa wakitajwa pamoja na Any Swebe "Ambassador" na Mafumu.
ReplyDeleteLakini hata MK Group nako aliacha kumbukumbu nzuuri saana.
Itabidi kufanya mpango wa kuunganisha makala hizi na Audios zake.
Asante kwa mara ya Tena Uncle Kitime
BW.KITIME, HIYO PICHA YA JUU,HUYO MWIMBAJI WA KWANZA KUSHOTO SIYO KAPELEMBE KOKO? ALIYEIMBA WIMBO WA JEAN PIERRE...'WATOTO WA JEAN PIERRE MUNAWAONA VILE WANATESEKA YOYO...' NAMFANANISHA VILE! NA HUYO ALIYENYUMA YA KIKKI KAMA MOHAMED IDD VILE..HEBU NIKUMBUSHE BW. KITIME.
ReplyDeleteNdiye mwenyewe
ReplyDeleteHIVYO HIYO 'X' MAANA YAKE KISHATANGULIA? OH! ALALE PEMA.
ReplyDeleteAnonymous 22:44
ReplyDeleteYule aliyenyuma ya King Kiki nadhani ni Zahoro Bangwe ambaye sasa yupo Msondo.
-Muarubaini
Ni kweli Zahoro Bangwe kwa sasa yuko Msondo, kwenye Bass yuko Mohammed Iddi , Drums Matei Joseph, waimbaji ni King Kiki na Kapelembe koko, kinanda Asia Darwesh, hizi zilikuwa enzi za nyimbo kama Kitoto chaanza tambaa, Lamanda na kadhalika.
ReplyDeleteNi kweli Zahoro Bangwe kwa sasa yuko Msondo, kwenye Bass yuko Mohammed Iddi , Drums Matei Joseph, waimbaji ni King Kiki na Kapelembe koko, kinanda Asia Darwesh, hizi zilikuwa enzi za nyimbo kama Kitoto chaanza tambaa, Lamanda na kadhalika.
ReplyDeleteMachozi yananilengalenga nikiwakumbuka wanamuziki mahiri wa kike waliotamba miaka ya 80 na 90 kama Asia Darwesh (RIP), Rahma Shally (RIP), Kida Waziri na Tabia Mwanjelwa. Kuondoka kwao katika anga la muziki kumetuacha wapweke
ReplyDeleteHivi Anna Mwaole yuko wapi?
ReplyDeleteJohn,kwa kweli unaleta raha mkuu....Asia kwa kweli nilikuwa namkubali mnooo...Naukumbuka wimbo wa Muuza Chipsi wa Bicc Stars wanakindumbwendumbwe ulioimbwa zaidi na Kinguti System(last tyme nilisikia yuko uarabuni na bendi ya Jambo Survisors akiwa na mwanamama Mlasi Feruzi wakatoa kibao kitamu cha Maproso)
ReplyDeleteOmbi maalum kwako John;je unaweza ukaanza angalau kutuwekea vipande vya nyimbo mlizotamba nazo miaka hiyo(hasa za vijana Jazz),kama yawezekana tusaidie tafadhali...Binafsi napenda kusikiliza nyimbo ambazo ni utunzi wako9kama sikosei) kama Malaine na Nyongise......Pia naomba ukiweza niwekee nyimbo au mashairi ya nyimbo za Mfitini na Mvuvi Kinda..
Natanguliza shukrani
Mdau Balantanda
Mkuu,mimi ninaomba utupe machache kuhusu malkia hawa wengine wa Muziki wa Tanzania wa miaka hiyo
ReplyDelete1.Tabia Mwanjelwa
2.Kida Waziri
3.Rahma Shally
4.Nanah Njige
5.Emma Mkelo 'Lady Champion'
Balantanda
JM, je Stella Amri yuko wapi siku hizi? namkumbuka from late 60's na early 70's nilipokuwa nikisoma.
ReplyDeleteBalantanda,
ReplyDeleteNadhani Tabia Mwanjela yupo Ujerumani na bado yupo kwenye fani ya muziki hali kadhalika Kida Waziri ambaye yuko Arusha.
Rahma Shalli, Nana Mjige 'Mzuri' na Emma Mkelo wote wameishatungulia mbele ya Haki.