YOUTUBE PLAYLIST

Saturday, April 24, 2010

Akina mama nao


Ni jambo lisilopingika kuwa akina mama wamekuwa sambamba na wanaume katika kuendeleza gurudumu la muziki wa nchi hii. Kumekuwa na tatizo la mtizamo na hivyo kufanya akina mama kutokuonekana sana katika fani hii kwa vile siyo siri imekua ikipigwa vita katika miaka yote. Pamoja na kuwa hakuna anaetamka hadharani kuwa wanamuziki ni wahuni, lakini taratibu na sheria zinaongea lugha ya kimya kuwa hivyo ndivyo. Nitoe mifano
1. Pamoja na kuwa kuna syllabus ya muziki kuanzia darasa la kwanza, kumekua hakuna jitihada kubwa ya kuhakikisha waalimu wanapatikana. Chuo cha Butimba ndio kimekua chanzo cha waalimu wa muziki lakini akishafika mashuleni hupangiwa vipindi vingine, na muziki huacha kama ulivyo.
2. Leo hii akiingia mwanamuziki kutoka nje ya nchi huhitajika kuwa na work permit, lakini kwa wanamuziki wa nyumbani hakuna taratibu zozote za ajira inayotambulika, hata wahudumu wa ndani wanatetewa bungeni lakini si wanamuziki. Angalia hata Waziri anaeshughulika na Vijana wa Tanzania na Kazi haoni soni kutoa ajira kwa vijana kutoka nje ya nchi yake katika fani ya muziki. Idadi ya wanawake katika muziki imekua kubwa sana kwa sasa ikilinganishwa na zamani lakini bado kuna wanawake wengi waliotikisa anga hizi zamani. Pichani ni muimbaji wa kike wa Afro 70 kutoka South Africa ambaye alisaidia sana kufanya muziki wa Afro kuwa na vionjo tofauti na bendi nyingine. Muimbaji huyu aliitwa Nini, na alirekodi nyimbo moja na Afro70, Mayele. Nini alikua na kaka yake aliyeitwa Vuli ambaye alipiga pia muziki hapa Tanzania na kutunga nyimbo ambayo bado inapiga na bendi kadhaa Tanzania'Lonely Child'. Vuli aliendelea na hatimaye kuwa manamuziki wa Lucky Dube.

8 comments:

  1. Anonymous13:48

    NAKUMBUKA PIA KULIKUWAKO DADA KUTOKA SOUTH KATIKA BENDI YA KING KIKI DOUBLE O NDIYE ALIYEIMBA WIMBO 'KACHELE'. WIMBO MAKINI,SAUTI SAFI, UJUMBE...(UTAJAZA)! NILIWAHI KUMUONA DADA HUYO LIVE PALE KEKO BAA FULANI NADHANI DIMAX KAMA SIYO OMAX (JINA LIMENITOKA KIDOGO). WAKATI HUO BWANA MKUBWA AKIWA BWANA MKUBWA KWELI(BODYGUARD PEMBENI)! ALIKUWAPO PIA MAREHEMU ASIA DARWESH NA DA TABIA MWANJELWA, PALIKUWA HAPATOSHI HAPO!

    ReplyDelete
  2. Sammy Mnkande07:26

    I remember both Nini and Vuli. Nini also sang "Sele Mwana" another Afro 70 hit. Vuli used to play the organ at Margots for Sunburst. He also sang vocals on Osibisa songs with the Nigerian guy who also used to play the Sax

    ReplyDelete
  3. Anonymous15:23

    KINA MAMA KATIKA GENERATION YA 70`s

    Kulikuwepo kina mama katika band kama The Rifters na Judy akiwa na kaka zake Nkulu na Freedom Hadebe kutoka South africa,Afro 70 na dada yake Vuli,The Comets na STELLA akiwa na Virda Amri na Alice Mhuto.
    Vulli alikuwa mwanamuziki wa kila chombo "piano,saxaphone,drums na vocal" nakumbuka kulikuwa na "buggy" Splendid Hotel katika mtaa wa "Independece Avenue" siku hizi Samora Avenue,aliimba wimbo wa kuigiza "Green Green Grass of Home"-Tom Jones.Kulikuwepo na band zingine zilizopata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kama The Groove Makkers,The BarKeys na The Heroes.
    Virda Amri,Alice Mhuto,Gershom Chihota,na mimi tulikuwepo kama "back-up" sitowasahau hawa kina mama walichangia "Generation" yetu katika mziki wa Tanzania.

    Mickey Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  4. Mickey kuna mtu ananiuliza ndiye wewe ulikuwa incharge wa Police Officers Mess Oysterbay?

    ReplyDelete
  5. Samahani Mr Kitime, naomba email address yako.

    ReplyDelete
  6. jkitime@gmail.com

    ReplyDelete
  7. Anonymous15:41

    Mkuu,

    Mickey,

    Umewataja wanamuziki kadhaa wa Afrika ya Kusini waliowahi kupiga muziki Tanzania wakiwemo "..The Rifters na Judy akiwa na kaka zake Nkulu na Freedom Hadebe kutoka South africa,Afro 70 na dada yake Vuli.." Hii inaashiria kwamba wanamuziki wa Kizaire na Kisouth Africa wamechangia kwa kiasi fulani katika muziki wa dansi wa Tanzania.

    Katika safu ya wanamuziki wa Kiafrika ya Kusini ambao waliishia mwishoni mwa miaka ya miaka ya themanini ni pamoja na kina Ritz, Mambazo, Thami The Dynamite na Veronica Farasi.

    Judy Hadebe mara ya mwisho kumuona ilikuwa miaka 1980s alikuwa anamiliki "a famous hideout spot" iliyokuwa inaitwa Lady Madonna Bar kule sehemu za Mikocheni inayopakana na Mwenge Satelite. Kuna mchangiaji mmoja humu alipiga gitaa kwenye harusi ya kaka yake Judy iliyofanyika kwenye hiyo "famous hideout"!

    Tunawakumbuka na kuwafahamu wanamuziki wengi wa Kizaire waliovuma kwenye muziki wa dansi wa Tanzania. Hebu tukumbushane na wengine toka nje ya Tanzania kama kina Marehemu King Enock na Joseph Mulenga waliotokea Zambia na kuchangia sana katika muziki wa dansi wa Tanzania. Kiki wa TX Seleleka, Watafiti na TatuNane toka Uholanzi na wanamuziki wengineo toka nje ya Tanzania waliovuma katika muziki wa dansi Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Anonymous15:02

    Ndugu John Mwakitime,

    Hauyo aliyekuuliza amekisia sawa kabisa nilikuwa meneja msaidizi katika bwawa la maofisa wa Polisi(POLICE OFFICER`S MESS
    Oysterbay/masaki tulipelekwa kuianzisha kutoka wizara ya utalii,wakati ule nikiwa New Africa Hotel mara tuu baada ya kumaliza masomo ya utalii,nikaondoka nchini 1977 mpaka hii leo nipo Scandinavien.

    Mickey Jones
    OLD BOYS GENARATION OF 70`s

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...