Mkongwe mwingine


Wengi tutakuwa tunamfahamu sana marehemu Ndala kasheba alieko kulia, je unamfahamu huyo anaesalimiana nae. Subiri usikie mchango wake katika muziki wa Tanzania

Comments

Anonymous said…
Balozi,
Huyo kushoto ktk picha ni Mh.Balozi Maharage.

Mdau
BabaJunior
Anonymous said…
Huyu ni Mh. Balozi M. Maharage Juma (ex-collegemate wangu mlimani). Katika burdani - enzi hizooo - alikuwa ni mwimbaji wa "soul music", hasa wa nyimbo za James Brown (early 70's). Inkishafi.
Perez said…
Eee Bwana Kitime Huyo Kasheba ananikumbusha jinsi walivyokuwa wanajibishana kwa kutumia ma Solo gitaa yao yeye na Nguza katika wimbo wa MAMA MARIA.
Masolo gitaa yanaongea yenyewe kwa yenyewe Mwanangu! Daa!

"...mama mariaa twakutakia kila la heri mamaa..."
Anonymous said…
Huyo ni balozi mhs Mohamed Maharage
alitikisa saana miaka ya 70`s aliitwa "James Brown" wa Tanzania akiwa na mkongwe Ndala Kasheba.

Mickey Jones
Denmark
Anonymous said…
Mkuu,

Muheshimiwa Balozi ana mdogo wake mwishoni mwa miaka ya 70 alikuwa ni booongeeee la disco dancer! Alishinda mashindano kadhaa ya dansi jijini Dar es Salaam. Yeye na partner wake walikuwa ni kivutio kikubwa sana cha uchezaji disco. Ninaweza kusema mdogo wa Muheshimiwa Balozi alikuwa ni outstanding choreographer and dancer.

Huyo mdogo wake Muheshimiwa Balozi alikuwa pia mlimbwende na mchekeshaji mzuri sana mwenye ufasaha wa hali juu wa lugha ya Kiswahili. Kwa jina la utani tulikuwa tukimuita Kamanyola au Nyolakama

Popular posts from this blog

Marijani Rajabu

SITI BINTI SAAD

Western Jazz Band

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika

Mlimani Park Orchestra

Super Kamanyola ya Mwanza