Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, May 19, 2010

Kitendawili tena

Naleta picha nyingine ya wanamuziki wa zamani, bahati mbaya kuna mmoja katika picha hii amekwisha tangulia mbele ya haki, wa kwanza kushoto ni Salim Willis, drummer, na baadae mpiga gitaa wa Afro70, wa kwanza kulia ni mwanamuziki wa toka enzi hizo na mpaka leo bado yuko jukwaani je unamfahamu ameshiriki katika miziki mingi inayopendwa sana. Unakumbuka bendi alizopitia?

8 comments:

Anonymous said...

hapa namkumbuka Salim Willis na marehemu Belino,huyu dada mrembo na mwanamuziki wa enzi mpaka leo siwakumbuki.
Mickey Jones

John Mwakitime said...

Willis yupo lakini Belino hayupo hapa.

SamMnkande said...

Mickey,Balozi M are you guys in facebook ? If so look me up

http://www.facebook.com/SamMnkande?ref=profile

Anonymous said...

Mickey
Huyo dada ni dada yake Salum Willis, sikumbuki nani mkubwa kati yao, mara ya mwisho 1999 nilikutana naye Arusha Int Conference Center, Sam Mkande huko face book sijaingia bado
Balozi

Anonymous said...

mwakitime naomba unisaidie kitu kimoja napenda sana wimbo wa jojina lakini sijuii mtu aliyeimba tafadhali naomba jina la mtu aliye imba na namna ya kupata huu wimbo niweze kuzikiliza hapa ktk computer tafadhali naomba unisaidie ubarikiwe sana

John Mwakitime said...

Sina uhakika ni wimbo gani wa Jojina unaoutaka,uliomaarufu ni ule ambao umepigwa na Safari Trippers, ukaimbwa na Marijani Rajabu. jaribu

Anonymous said...

Huyu wa kwanza kulia ni Jeff those days alikuwa ni drummer boy wa the groove makers pamoja the late Herbet lukindo, the jengo brothers and ofcourse the one and only one our James brown s(atchmo)

Kitime J said...

Wa kwanza ni Jeff, kwa sasa yuko Sikinde,Na wa mwisho ni Salim Willis alikuwa Afro70

Adbox