Mazoezini katika ukumbi wa Amana katika uhai wake |
Moshi
William alizaliwa mwaka 1958 hale Mwakinyumbi Korogwe. Pale palikuwa na Mzee
mwanamuziki maarufu aliyekuwa akiitwa Mzee Masongi na bendi yake ilikuwa chnzo
cha wanamuziki wengi maarufu akiwemo Moshi William. Jina halisi la Moshi
William lilikuwa Shaaban Ally Mhoja lakini alikuja kubadili na kuitwa Moshi
William kutokana na kuja kulelewa na baba mwingine. Alipewa kisifa cha TX, na Julius
Nyaisanga.
Moshi
alifariki siku ya tarehe 29 March 2006 katika wodi ya Sewa Haji baada ya
operesheni ya kuondoa chuma katika mguu wake uliovunjika kwenye ajali.
Alifariki saa tatu kasoro robo asubuhi na kuzikwa siku hiyohiyo katika makaburi
ya Keko Machungwa. Moshi lipitia bendi kadhaa baada ya kutoka Hale zikiwemo UDA
Jazz, Safari Trippers, Polisi Jazz na hatimae kutua JUWATA 1982. Ambapo aliweza
kutuacha na album 13. Na pia alishinda tuzo la mtunzi bora kuanzia mwaka 2003
hadi 2005.
Kaburi la Moshi William |
Mungu
amlaze pema Shaaban Ally Manongi, TX Moshi William