YOUTUBE PLAYLIST

Saturday, September 4, 2010

The Upanga Story-Autographs

Utamaduni wa Autograph ulikuwa maarufu sana kwa vijana wa enzi hizo, kwa bahati tuu niliweza kupata kurasa chache za Autograph za vijana wa Upanga sitayataja majina ya wahusika kwa sababu nyingi sana chini ni maelezo yaliyokuwa kwenye autograph hizo, ukizisoma zina eleza mengi kuhusu hali ya wakati huo;
Drink: Coke
Food: Ugali
Clothes:boo-ga-loo
Singers: James Brown
Showbiz Personalities:Guliano Gemma
Records: The Chicken
Girl: "X"
Boy:Groove Maker
Place: Mchikichi
Best Ambition: Music (Drumer)

Drink: Babycham
Food: Tambi + Rice
Clothes: Pecos(bell-bottom)
Singers: James Brown, Clarence Carter,Otis Redding
Showbiz Personalities:Sidney Poitier,Elvis Presley,Franco Nero
Records: If I ruled the world,Thats how strong my love is, Take time to know her,
Girl: The one who loves me
Boy:Groove Maker
Place: Soulville Upanga
Best Ambition: Secret Agent

Drink: Fanta
Food: Chapati
Clothes:boo-ga-loo
Singers: Percy Sledge,James Brown
Showbiz Personalities:Fernando Sancho, Lee Marvin
Records: Take time to know her, Sex Machine Blue Transistor Radio
Girl: Fikirini
Boy:Groove Maker
Place: Soulville Upanga
Best Ambition: Electrician

10 comments:

  1. Anonymous11:48

    John Mwakitime
    Hii kali maana hata kazi imenishinda kufanya mara baada ya kuona chapisho hilo.
    Ninaenda kutafuta yakwangu nione kama nitaipata maana hii ndio ilikuwa FACEBOOK ya wakati ule. Very very MANUAL

    ReplyDelete
  2. Anonymous17:10

    Mkuu,

    Kulikuwa na wanandugu wawili waliokuwa mabingwa wa kutengeneza hizi autographes kwa kutumia manilla paper halafu wanazichora kwa crayon au colour pencils ule upande wa kuweka picha. Sikuwahi kuona autograph nzuri zaidi ya zile.

    Mmoja wa wanandugu hawa alisoma Tambaza na alikuwa bonge la muigizaji kwenye kile kikundi cha waigizaji wa Tambaza. Mwana ndugu mwingine in the early 80s wakati Space 1900 Disco Mbowe Hotel alikuwa doorman.

    Autograph langu analo pedejee mmoja ngoja nianze kumdai.

    Mkuu, Asante sana kwa hii post. Babu kubwa!!!

    ReplyDelete
  3. mdau USA21:24

    Kumbe Ubishoo wa watoto wa upanga haukuanza leo ..wemerithi toka kwa baba zao..

    ReplyDelete
  4. Anonymous11:47

    Mimi favorite yangu ni ya wale watu waliokuwa wakisaini ukurasa wa mwisho kabisa wa autograph book: "By hook or by crook, I am the last in your book, the last to be remembered and the last to be forgotten". Eddy.

    ReplyDelete
  5. Roses are red
    Violets are blue
    Sugar is sweet
    And so are you

    ReplyDelete
  6. Anonymous12:12

    John!
    Kama nakuona wakati unapost mambo haya unachekaaaaaa! namiss sana nyumbani. Vipi ratiba ya Eid kwani band yenu haina web page tujue ili kama yawezekana tuje tumfukuze nyokaa!

    ReplyDelete
  7. Hahahahaha Njenje watakuwa Salender Bridge.Kuhusu web ngoja tufufue japo blog leo jioni

    ReplyDelete
  8. Anonymous17:04

    Utabiri wangu ni kwamba hizi autographs ni za katikati ya miaka ya sabini kwa kuwa ni enzi hizo watu kama James Brown, Elvis Presley na Sidney Poitier walikuwa wakitamba bila ya kusahau mavazi kama pecos na mashati ya slim-fit.

    ReplyDelete
  9. Anonymous20:28

    Tufahamishe ni blog gani ili tuwe tunapata matukio yooote yanayoihusu bendi yetu inayopiga miziki wa kitanzania tafadhali

    ReplyDelete
  10. Anonymous11:28

    Anon wa 07:28, Mimi naona hizo autographs ni za early 1970's (1972-1975) kwa sababu hizo hizo ulizozitoa na kutajwa kwa Groovy makers na soulville.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...