YOUTUBE PLAYLIST

Friday, July 30, 2010

Mwanamuziki Mheshimiwa Paul Kimiti


Kwa muda mrefu nilikuwa na nia ya kuweka taarifa kuhusu wimbo wa kumsifu Nyerere ambao uliimbwa na Mheshmiwa Paul Kimiti. Nilijitahidi kutaka kupata taarifa kutoka kwake ikawa haikuwezekana lakini karibuni nilisoma maelezo ya Mheshmiwa mwenyewe kuhusu kazi hiyo, ambayo alisema walifanya akiwa Mwenyekiti wa wanafunzi kutoka Tanganyika katika chuo kikuu cha Netherlands kati ya mwaka 1962 na 1965. Akiwa na wanamuziki wenzake wakiwa na kundi waliloliita Safari Brothers walirekodi nyimbo hii nzuri sana kuhusu Mwalimu Nyerere. Mheshimiwa alisema walitoa dola 20,000 walizozipata kutoka Philips records kwa Mwalimu alipotembelea Netherlands April 1965, pesa hizo walitoa ili kuchangia maendeleo ya nchi yetu, na huo ndio ulikuwa mwanzao wa uhusiano wake na Mwalimu.

9 comments:

  1. Uncle JK sikuwahi kufahamu kuwa mheshimiwa Paul Kimiti alipata kuwa mwanamuziki. Ama kwa hakika, ninayo shukrani ya dhati kwako kwa kutufahamisha jambo hili.

    Pia nampongeza sana mheshimiwa Kimiti kwa kuamua kupumzika siasa. Natumia jukwaa hili kumshukuru kwa mchango wake kama kiongozi wa taifa na kumtakia kila la heri katika ustaafu wake.

    ReplyDelete
  2. nataka kuandika kama alivyoandika fadhy mtanga hapo juu.

    je kibao hiki chapatikana wapi?

    ReplyDelete
  3. Najua RTD wana kibao hicho na nimewahi kukisikia mara kadhaa miaka iliyopita

    ReplyDelete
  4. Anonymous21:44

    Huu wimbo wa 'Tumsifu Kambarage' ktk http://mwanasimba.online.fr/E_bands_tumsifu.htm ndio huo Balozi?

    ReplyDelete
  5. Si huo mkuu but thats a nice song hizi ni nyimbo zilizotolewa na Tanzania Film Company

    ReplyDelete
  6. Si huo mkuu but thats a nice song hizi ni nyimbo zilizotolewa na Tanzania Film Company

    ReplyDelete
  7. Si huo mkuu but thats a nice song hizi ni nyimbo zilizotolewa na Tanzania Film Company

    ReplyDelete
  8. Si huo mkuu but thats a nice song hizi ni nyimbo zilizotolewa na Tanzania Film Company

    ReplyDelete
  9. Si huo mkuu but thats a nice song hizi ni nyimbo zilizotolewa na Tanzania Film Company

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...