YOUTUBE PLAYLIST
Thursday, July 15, 2010
Lutumba Simaro wa Ok Jazz
BANNING EYRE ni mwandishi Mmarekani aliyefanya mazungumzo na mwanamuziki Lutumba Simaro mpiga gitaa wa kundi la OK Jazz, kuna mengi ya kujifunza kwa wanamuziki wa Tanzania
SWALI: Nini kinaendelea katika muziki wa Kongo siku hizi?
SIMARO: Kinachoendelea sasa sikipingi, mi ndio baba yao, hawa vijana kuna kitu walichoingiza katika muziki. Wameleta damu mpya na ujana kweli lakini,kuna monotony mno, Huwezi kutofautisha bendi moja na nyingine. Wanavyoimba, wanavyocheza na wanavyopiga mgitaa katika kile wanachoita seben. Kuna mtangazaji mmoja anaitwa Gaspar wa Studio Maximum, ana kipindi kimoja ambapo nilikuwa nasikia wimbo wa Werrason lakini alikuwa JB anecheza na wimbo wa JB ukichezwa show na Werra, kwa kweli huwezi kuona tofauti ya muziki wa hawa wawili.
Enzi za OK Jazz, Franco alikuwa mtunzi mzuri sana, mimi nikajiunga nikaleta style yangu, Josky alipokuja nae akaleta staili yake. Ndombe nae pia akaja na staili yake. Wote tulikuwa OK Jazz, gitaa la Franco ndilo lilitawala na kuweka nembo ya staili zetu mbalimbali. Papa Wemba akiimba najua ni Papa Wemba ana staili yake. Mdogo wangu Kofi nae anastaili yake, Zaiko ya Nyoka Longo pia wana staili yao
Kama wangeweza kunisikiliza ningewaambia hivi hawa vijana wanajitoa Wenge na kuanzisha makundi yao, ni muhimu kuja na utofauti, wana waimbaji wazuri sana, watunzi wazuri na wamepata bahati kuweza kurekodi katika studio za kisasa wana jukumu la kuendeleza ubunifu. Wakati wetu wa enzi za Vicky Longomba, Mujos na Kabasele, kama we ni mwimbaji ulilazimika kuimba aina mbalimbali za muziki. Muziki wa Ulaya au Marekan na kwa staili mbalimbali. Mtu akiomba Tango, unapiga Tango , ukitakiwa kuimba Waltz uliimba style hiyo, lakini waimbaji wetu wa sasa, hakuna kitu. Na wapiga magitaa pia, tulikuwa na wapiga magitaa wakali kama Papa Noel, na Tino Baroza, na hata Franco. Wapiga magitaa siku hizi ukiwauliza unamfahamu Nico Kasanda? Tuno Baroza? Kimya kinatawala. Muhimu kujua staili zao ili kujitafutia stail mpya. Nina mpiga gitaa ana miaka 20, wiki iliyopita nilimpa sanduku zima la santuri akafanye mazoezi, nashukuru ameanza kuniuliza maswali mengi kuhusu upigaji mbalimbali. Utunzi nao unapwaya pia utakuta wimbo unataja majina ya watu 200, wanaita “mabanga”, nawauliza majina mengi ya nini wananiambia hawa huwa wanawalipa vizuri.
Vijana wana bahati wana teknolojia nzuri, wana TV nyingi na nzuri za kuweza kuwafanyia promotion, Wakati wetu tulikuwa na radio moja tu, hivyo ililazimu kufanya kazi nzuri ili ujulikane. Nawakumbuka Soki Dianzenza na Soki Vangu walikuja na kitu kipya, Nyboma, Pepe Kalle wote watakumbukwa kwa aina yao ya uimbaji.
Nimeitafsiri kwa ruksa ya Banning Eyre. Kwa habari nyingi zaidi angalia www.afropop.org
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Asante Kitime kwa interview ya Mzee Mzima Lutumba Simaro...nafkiri hii ni fundisho pia hata kwa Bendi za Tanzania, Twanga,Akudo,Academia,Extra Bongo n.k...wanao kopi miziki ya akina kizazi kipya cha Kongo.
ReplyDeleteVijana wa sasa hawapendi kuvunja kichawa kwa kubuni chao...hata ukienda kwa hao Bongo Fleva utasikia kasumba hiihii...wanataka kutengeneza pesa haraka bila kufikiria kesho waache historia ya kuenziwa...kweli muziki wa Kongo ulaya hauna soko kama wa Senegal ao Mali...!muziki wa Kongo ni makelele nakukata mauno tu,wanao nunua CD's ni Wazungu wana Mashule ya Miziki wanajua huu ni Muziki wa kelele na uliotulia...
Namuunga mkono Simaro kwa asilimia 100. Niliwahi kuandika katika blog hii kuwa muziki wa siku hizi wa Congo ni makelele matupu. Nilisema pia kuwa ni vigumu kutofautisha muziki wa wanamuziki tofauti wa nchi hiyo. Nashukuru kuwa mawazo yangu yanashabihiana na mwanamuziki huyo mkongwe anayeheshimika nchini DRC na nje ya nchi hiyo. Hebu sikiliza baadhi ya tungo za Simaro (Bisalela na Mbongo) alipokuwa na TP OK Jazz katika link zifuatazo na ulinganishe na haya makelele tunayosikia sasa:
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=QJHulsjzR2Q
http://www.youtube.com/watch?v=9D164ZJDnSE
Jamani muziki wa leo umepoteza ladha kwasababu hakuna vipaji vya kweli. Watu wanaishi kwa kukopikopi tu hadi mwisho. Na kwasababu bendi zinaweka steji shoo walionusu uchi (ambavyo haikuwepo) na kwakuwa mara nyingi watu wanakuwa wameshalewa wakati wa mziki hakuna anaelalamika.
ReplyDeleteJana nilikuwa najiuliza hivi mtu kama Marijani Rajabu aliwezaje kutoa hits mfululizo? Hebu jaribu kufikiri, Masudi, Siwema, Uke wenza, Mwanameka, Zuena, Mayasa yaani ningekuwa na mda ningeendelea kuzitaja hizi hits ambazo zote zilikuwa original. Leo hii ukisikiliza mziki hasa kwenye chorus huwezi kutofautisha kama ni Twanga pepeta, Akudo au FM Academia. Wote wanapiga sawa tofauti ni kwamba wakongo wananogeshea kidogo vyombo vyao maana sebene ni miziki yao. Vinginevyo hakuna tofauti. Hivi hawa watu kama Twanga pepeta wanajua kwamba zamani wakongo walikuwa wanakopi miziki ya TAnzania? Nasikia Tabu Ley alikopi Asha wa Tabora Jazz. Na mimi nilikuwa na akili zangu miaka ile wakati sijui Yondo Sister au Tshala Muana alipokopi wimbo wa "Dezo dezo" wa maestro Ndala Kasheba. Tena nasikia enzi za akina Mbaraka Mwishehe majabali ya muziki kama Franco walikuwa wanakaa meza moja na wanamuziki wa Tanzania kwasababu ya heshima ya muziki tuliyokuwa nayo wakati huo.
Ukienda bongo fleva kwa sababu maproducers ni wachache nyimbo nyingi zina music arrangements zinazofanana. Kwanini zisifanane wakati wanamuziki 200 wanategemea kupigiwa muziki na mtu mmoja? Halafu nyimbo zenyewe hazina currency (ukisasa). Zamani (nina miaka 32 jamani niwieni radhi)wakati wa mambo ya kuzamia meli Vijana wakatoa Ngapulila. Mandela alipokuwa jela washirika wakatoa Mandela must be free. Juwata walileta ule wimbo unasema "wakati wa ujana wangu shati shilingi sita unapata kwa hivi sasa hata soda hupati". DDC nafikiri ikawaona mafisadi wa mapenzi ikatoa "usitumie pesa kama fimbo". Yaani kila wimbo ulikuwa na currency. Leo hii ni "pedejee x, pedejee y" mpaka wimbo unaisha. HEbu akina Mzee Mwakitime leteni mziki wa kweli Tanzania. Mziki ambao hauhitaji mabinti kucheza uchi ili watu wajae ukumbini. Nilikuwa nasikiliza wimbo wa "kadiri Kansimba" wa Tuncat au Sambulumaa? Ziki lililopigwa humo wala hakukuwa na sababu ya akina Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga kuimba maana music arrangement hadi leo hii ni 100% international. Hata ukimpa mkongo hawezi kupiga zaidi ya hapo. Sikiliza "Mundinde" wa vija jazz halafu niambie kuna wimbo gani mwingine unapiga drums kama vile, unique. Kwa mawazo yangu, wimbo wa mwisho kupigwa vyombo vizuri na sauti kupangiliwa ni ni "Msafiri Kafiri" wa Msondo. Pale unakuta bass limepigwa kipekee, saxaphone kipekee na sauti zimepangiliwa sio kelele. Walikosea na wao kuanza kutaja taja majina ya watu. Yani sipendi hiyo tabia kuliko.
Enyi vijana mnaotaka kuingia au ambao tayari mpo kwenye tasnia ya muziki, jaribuni kutafuta kujifunza sio kukurupuka tu. Enzi zile (miaka ya mwishoni mwa 80 hadi katika ya 90) vijana walipikwa wakaiva. Nambie kijana gani anakipaji cha kuimba kama alivyokuwa kijana Jerry Nashon? Nasikia hata gita alikuwa napiga. NAni ana stereo ya Eddy Shegy? Yupi ana sauti mvuto kama akina Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga? Nambie nani anapiga kinanda kwa ustadi wa Abdul Salvador au hata mama Asia Daruweshi? Ni mdada gani leo ataimba kama akina Kida Waziri na Nana Njige? Sifuri sifuri sifuri.
Nazilaumu redio stesheni na vituo vya tv tanzania. Wangetoa mwanya kwa muziki wa kweli kusikika, pengine vijana wangeacha uvivu wa kibunifu. Wizara husika nayo inastahili lawama. Pengine itabadilika siku wakimweka mtu anaejua mziki badala ya Akina Professa KApuya ambao wanauweza wa kuunda bendi nzuri ila wameamua ku-promote ukongo kwa kuunda Akudo bendi ambayo ina wakongo asilimia 99. Nakilaumu Chama tawala pia maana kama wapo serious na muziki wa kweli wangewaita nyie wazee kutumbuiza kwenye mkutano wao wa kitaifa Dodoma na badala yake wamepeleka bongo fleva. hivi kweli wazee wale hawaoni aibu kutingisha matumbo kwa kucheza uchafu wa Bongo fleva jamani? Hivi kama hawaoni aibu kucheza miziki ya kihuni hadharani, wataonaje aibu kuwa MAFISADI? Acha kwa leo niishie hapa ila nina kilio kikubwa cha muziki nchini Tanzania.
ReplyDeleteAnonymous 23:48 & 23:49 machambuzi yenu ni ya ukweli,Muziki halisi wa Tanzania umeKUFA... kwa sababu SERIKALI umeupa mgongo,Medias za Tanzania yaani Tv's,Magazeti na Radio's zina promoti tu Hip-Hop ya USA aka Bongo Fleva...naomba nikwambieni nyinyi msio fahamu maana ya "Musician" ni yule anaepiga ao kupuliza chombo kama: Guitar,Saxophone,Trompett ,Trombone,Keyboad,Drums...sasa utakuta Medias za Tanzania zina promoti mtu kajiita Mfokaji(Rap) eti Musician na hajui hata KEY ya Music ao kupiga CHOMBO. Dr.Remmy Ongala na Orchestra Matimila katika miaka ya 80-90 walisafiri Dunia mzima kuutangaza Muziki halisi wa Tanzania. Walirekodi na kusaini mkataba na Recording company ya kimataifa Real World ya Peter Gabriel.Hiyo Hip-Hop mnayo promoti sijue kama ita tanganza Tanzania ki Muziki Nchi za nje... sababu ni utamaduni wa Marekani.
ReplyDeleteMdau wa 23:48 tembelea Msondo ngoma pale Sigara kila jumamosi au Africenter jumapili usiku ni balaa. Hayo yanayokosekana kwa bendi nyingine utayakuta. Msondo bado wanajitahidi albamu yao mpya kuna nyimbo zimechekecha vizuri kama Cheo ni Dhamana wa Eddo Sanga. Lakini ukienda Twanga, Extra, Bwagamoyo, Akudo, FM na Diamond hakuna tofauti ubunifu sifuri kuanzia vyombo hadi uimbaji.
ReplyDeleteNiongeze pia toka kwa anony wa 04:58 kwamba muziki wa Remy ulikuwa wa kipekee na kuwa na hits kadhaa mfano Kifo, Siku ya Kufa, Sauti ya Mnyonge, Kilio cha Samaki, Narudi Songea, Mwanza n.k. Tena kwa wale msiojua, wimbo wa Remy wa "Kipenda Roho" ulitumiwa kama background sound track ya cinema maarufu ya Hollywood ya mwaka 1996 iitwayo "Natural Born Killers". Hii iliwashirikisha wanasinema maarufu duniani kama Tommy Lee na Robert Downey Junior ambao hadi leo wanavuma Hollywood. Haya niambie ni mziki gani leo utafikia hivi viwango?
ReplyDeleteJK kaendelea kuniudhi alipokuwa anafunga bunge kwa kusifia mafanikio ya Bongo fleva na kwamba amewanunulia mtambo wa kyurekodi. Wanarekodi nini hasa? Wanachokijua ninini? Muziki wao ni wa utamaduni upi? Nini tunajifunza kutoka kwenye nyimbo zao? Jamani akili ni nywele ila wengine wanatenda kana kwamba wanavipara toka utotoni.
Anonymous 01:56 Nakuunga mkono JK kazunguukwa na JAMAA fulani wa Redio na sasa wana Tv nia na madhumuni yake ni kuuzima Muziki wa Dansi.
ReplyDeleteKuna wakati JK aliomba akutane na Wanamuziki,JAMAA akavungavunga akawaleta WanaHip-Hop aka Bongo Fleva.JK kaomba aletewe Mkongwe Zahir Ally(Zorro)...
Studio ya mastering imeletwa imesimamiwa na JAMAA,baada ya malalamiko ya Wanamuziki wa Dansi ndio kakubali bendi zaweza kurekodi,yeye mwenyewe atagaramia ili nyimbo zipigwe katika Station Radio yao.Nakuombeni nyinyi Wakereketwa wa MUZIKI HALISI WA TANZANIA mlio nje na ndani tujaribu kumwandikia Rais ateuwe mwakilishili wa Muziki wa Dansi,kama akina Kitime,Waziri,Juma Ubao,Mafumu,King Kiki ao Matei JAMAA awe mwakilishi wa Hip-Hop yao
Kizazi cha sasa kuna sehemu nyingi za kupatia ujuzi, mfano ktk upigaji gitaa wapo watu wameweka demo za upigaji wa muziki wa dansi ktk youtube nenda halafu search:
ReplyDelete-African soukous demo 4 (sina makosa lead)
- African soukous guitar demo 6 (6ths & 10 ths solo guitar) hapa ni jinsi wa kula na kian Franco au Mose sengo fan fan
Uwanja wa kujiendeleza ni mpana sana, ila inatakiwa kizazi cha muziki wa dansi wa sasa kuwa na moyo wa kujiendeleza kwa kutumia wazee wa zamani, madarasa, youtube n.k