Hawa wanamuziki kama unavyowaona wanapiga saxophone , walikuwa na mengi zaidi wanafanana walikuwa pia wanaweza kupiga vizuri vyombo vingine, japo hawakuwahi kuwa bendi moja lakini wote waliwahi kuwa katika bendi zilizorekodi muziki ambao unapendwa mpaka leo ni akina nani na walipiga vyombo gani na walipitia bendi gani?
YOUTUBE PLAYLIST
Wednesday, May 19, 2010
Magwiji wa kweli
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Huyu kwenye picha ya chini ni marehemu Abel Balthazar. Huyo mwingine wadau wengine wasaidie kutukumbusha.
ReplyDeleteLile solo la Balthazar katika Msondo ya miaka ya 1970 lilikuwa si mchezo. Ni solo ambalo liliipa Msondo utambulisho kiasi kwamba hata ukisikia kibao cha bendi hiyo kwa mara ya kwanza unajua huo ni Msondo. RIP Abel Balthazar.
ReplyDeleteSina uhakika lakini nafikiri huyu ni Shabby Mbotoni mwana Afrosa na Abel Balthazar mwana msondo
ReplyDeleteMickey Jones
Solo la Balthazar liliitambulisha Msondo kama gitaa la Luambo lilivyoitambulisha TP OK Jazz miaka hiyo. Hata leo hii, solo la Msondo bado lina mirindimo ya Balthazar, zaidi ya miaka 30 baada ya yeye kuondoka katika bendi hiyo.
ReplyDeleteHapa nimeshinda mimi: Huyu wa juu ni Shabby yule wa Afro 70, na huyu wa chini bila kufuta tongotongo zangu ni Baltazar wa Nginde ambaye alikuwa Msondo enzi hizoooooooooo!
ReplyDeleteDuh, ndugu yangu Mickey Jones, kumbe wewe sio mwenzangu. Wewe ni wale wazee wa mjini ambao hawakupenda kupitwa na mambo.
ReplyDeleteMickey Jones, wewe ni wale wazee wanaoenda na wakati, kwa sababu kuna mambo mengi ya "kileo" unayachanganua vizuri kuliko hata vijana wa kileo tunaowategemea kutuelimisha.
Mickey Jones, hata akina "Mtakatifu Simon Kitururu", vijana wa kisasa umewafunika.
Mickey Jones, nimekutana na wewe kwa mara ya kwanza "Bongocelebrity". Umekuwa ukinivutia katika utoaji maoni yako yaliyoenda shule.
Mickey Jones pamoja na Mzee John Kitime, mchango wenu kwetu sisi Watanzania ni mkubwa sana, japo kila mmoja wenu ana nafasi yake katika hilo.
Tunawashukuru sana na tunawaomba msichoke kutuendeleza kwa kutufungua masikio kwa yale ambayo hatukuwa tunayajua zamani.
It's Great To Be Black=Blackmannen
Mdau hapo juu utakuwa umepatia...nimeangalia kwa makini picha ya kwanza huyo ni kaka Shebby Mbotoni hahahahaaaaaaaaa!
ReplyDeleteHapo ni Shabby Mbotoni na Abel Balthazar
ReplyDelete@BLACKMANENN: :-)