YOUTUBE PLAYLIST

Monday, April 19, 2010

Usimkwae mtu likwae chua


Chakachua ndio ulikuwa mtindo wao, walikuwa na mpiga solo ambae wapiga magitaa wote waliomjua wanamheshimu kwa upigaji wake. Kuna mwanamuziki Mtanzania aliyeko Japan aliwahi kunambia kuna siku aliwahi kumsikilizisha muziki wa Chakachua mpiga gitaa mahiri George Benson, George Benson alisikitika sana kusikia aliepiga gitaa vile ameshafariki kwani alitaka wakutane watengeneza kitu cha pamoja, huyu si mwingine bali ni Michael Vicent. Na bendi ilikuwa Urafiki Jazz iliyokuwa chini ya Kiwanda cha nguo cha Urafiki Dar Es Salaam

10 comments:

  1. Anonymous16:52

    kidogo kidogo unatuumiza!

    ReplyDelete
  2. Anonymous22:51

    Ukitaka kujuwa umahiri wa Michael Vincent sikilizeni ule wimbo wa "Mtoto wa mjomba." Jamaa alilipuliza solo katika ule wimbo, yaani ni raha ya pekee. Huyu jamaa naweza kumfananisha na Shaaban wanted kwa ukun'gutaji maana hana mchezo.

    ReplyDelete
  3. Anonymous22:51

    Michael Vincent alifariki lini jamani? Mungu amrehemu mahala pema peponi amen.

    ReplyDelete
  4. Anonymous22:52

    '.....utampata wako mwingine utakaye mpenda, rudisha roho dunia hii ni pana sana kijana.' Mambo ya mtoto wa mjomba hayo. Hivi kweli TZ tuna ma-dj wa redio? Kwanini wasikae chini siku moja hao ma-dj wasilize vigongo vya muziki wa dansi kisha wafananishe na fleva, waone nani ana ujumbe mkali.

    ReplyDelete
  5. Anonymous22:54

    Ma-dj wa TZ wote ni wajinga tu, wao wameweka mchongo mbele badala ya kuweka vitu vya uhakika. Kwa miaka kumi ijayo kama bado tutakuwa na hii tabia ya kuajiri waandishi feki basi hata watu hawatasoma magazeti tutakuwa tunapata habari kwa kina Kitime, Michuzi na wengineo.

    ReplyDelete
  6. Anonymous16:46

    Huyu Michael Vincent nadhani bado hatujampata guitarist kama yeye,watu wajaribu kusikiliza vizuri zile nyimbo za geza ulole,mauaji soweto,asmaha nk.kama wewe ni mpiga gita,utakuta humo scales za kutisha,kama pentatonic scales na minor zake nk.na amezitumia katika muziki wetu wa dansi wa kiafrica,jribuni kuzizfuatilia nyimbo hizo hasa wanamuziki au wapiga magita mtaona
    ukweli wa huyu bwana,he was the great guitarist among East African
    guitarists.mungu amuweke pahali pema peponi.mwanamuziki wa ki tanzania niishie Japan.Abbu Omar

    ReplyDelete
  7. Hello Abbu vipi Japan? Nilimpa Ben nyimbo kama kumi za Michael Vicent nategemea ulizipata. Ni kweli Michael alikuwa kitu kingine, namuweka daraja moja na Juma Ubao

    ReplyDelete
  8. Anonymous19:37

    Asante sana mkuu J.Kitime kwa kuwa na idea hii ya kuanzisha blog hii ihusuyo mambo ya muziki wetu hasa wa dansi huko nyumbani Tz.nimefurahi kuona kwa ujumbe wangu nilioutoa kuhusu Michael Vincent umefika na nimeusoma,NYImbo zote ulizompa bwana mdogo Ben nimezipata nadhani nitangu last year mwishoni,asante sana kwa msaada wako,huwa nazisikiliza karibu kila siku,kuhusu bwana Michael Vincent nadhani watu hawamjui vizuri,hasa wanamuziki wa kizazi kipya,pia mashabiki hushabikia tu mwanamuziki wanaempenda huo ni uhuru wao,Lkini swala la Michael V.
    litabaki pale pale hata marehemu Joseph Mulenga niliwahi kumuuliza aakasema yaani kwa Tanzania ndio wapo wapigaji solo wakali pamoja na yeye,lakini kwa Michael Vincent
    ni mwisho.Mpiga gita mwingine ambaye sasa ni marehemu na alikuwa na stali hiyo hiyo ya Michael ni mzee mmoja nae alitoka huko huko Tanga kwenye bendi moja ilikuwa inapiga nadhanai ni klabu ya Mwangoennae alipotelaea Mombasa siku nyingi,na tuliwahi kuongelea habari za huyu Michael Vincent akasema yula alikuwa junior wake lakini akamkubali kuwa ni mkali,tena huyu bwana katika kuhangaiaka na kazi yetu ya miziki aliwahi kuishi Uganda nako aliacha jina kubwa tu,asante mkuunaandaa profile yangu ya miaka 11 kwa Simba Wanyika nitakuletea mkuu,na pia nyimbo nyingi nilizoshiriki.asante
    Abbu Omar,Prof Junior.Tokyo Japan.

    ReplyDelete
  9. Anonymous19:45

    Nilizipata mkuu,nashukuru pia kwa jmambo juhudi zako za kuweza kuwaelewesha
    wadau mbali mbali mambo ya kuhusu miziki yetu ya enzi hizo,itasaidia sana kuwapa watu habari zenye ukweli na siyo ubabaishaji,maana nimefuatilia hii blog yako naona kuwa huwa unafanya research ya kutosha na ndipo unatoa habari,karibu asilimia 100 ya habari za blog hii ihusuyo muziki ni za ukweli.Nami najiandaa kukuletea profile yangu katika Simba Wanyika kwa miaka 11 hivi,na nyimbo au album nilizoshiriki kwa
    kipindi chote hicho.asante
    Abbu Omar,Prof.Junior,Tokyo Japan.

    ReplyDelete
  10. chesi.com17:10


    Kitime, Abbu Omar mimi sina utaalamu sana wa chords za muziki lakini kwangu mimi ninaona solo iliyopigwa kwenye wimbo wa Urafiki wa 1976 wa 'Rukia uliambiwa hukusikia', yule mpigaji ambaye nilidhani ni Mzee Ngulimba wa Ngulimba ulikuwa ni Mkono usiokuwa wa kawaida.
    Nilipenda pia wimbo wa mwaka nadhani 1972 wa 'Eddah wanipa Machungu'

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...