Miaka michache iliyopita kulianza hadithi moja ambayo vyombo vya habari vikaishikia bango, na baadae wanamuziki kadhaa nao wakashika bango nakutoa ushauri nasaha wa tatizo hilo. Tatizo hilo lililkuwa kwanini muziki wa bendi Tanzania hauwi maarufu. Kwa utafiti ambao washika bango waliufanya wakatangaza kuwa Tanzania tuna tatizo la kuwa tunapiga aina nyingi mno za muziki ndio maana haujulikani. Kwa hiyo wataalamu hawa wakiwa wanalinganisha na muziki wa Kikongo wakasema Mkongo mmoja akianzisha Kwasakwasa wote wanapiga Kwasakwasa , ikija Kibinda Nkoy wote wanapiga hivyo hivyo , kwa hiyo nasi tuwe na staili moja, tena ikapewa jina Achimenengule. Utafiti huu ni wa ajabu sana, tuanze na nchi yetu ina makabila zaidi ya 110,yenye mila mbalimbali na muziki mbalimbali, inashangaza kujaribu kufikiri wote hawa wapende aina moja tu ya muziki. Huko Kongo ambako kulitolewa mfano hata wakati wa kile kipindi kinachoitwa the Golden Age of Congolese Music, ndipo haswa upigaji wa aina mbalimbali ulipokuwepo. Huku kulikuwa na Dr Nico, Franco, John Bokello,African Fiesta, bendi za vijana kama Lipualipua , Belabela, Orchestra Kiam, Empire Bakuba, Veve, kila moja ilikuwa na aina yake ya muziki,wapi ilikuja kupatikana hiyo theory ya kupiga staili moja ni kitendawili. Tatizo la kudumaa kwa muziki wa Tanzania si kutokupiga staili moja.
YOUTUBE PLAYLIST
Thursday, April 8, 2010
Muziki wa staili moja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Ndiyo mkuu ,bwana kitime.sasa nafikiri hoja yako najinsi ulivyo ichambua sihaba.muziki wa staili moja hakika ni neno pana sana na linahitaji upeo mkubwa wa kuelewa na kujadili kwa mapanayake.mimi binafsi yangu nahusudu muziki vibaya sana.ila kuhusu hili la staili moja ya muziki,niuvivu wa ubunifu, nakutotilia maanani taaluma nzima ya muziki.yawezekana kukawa na stili au mtindo sina hakika kama vyote ni sawa(kiswahili)lakini kunakuwa na vionjo mbalimbali vinavyo nogesha muziki huo katika staili hiyo au mtindo huo.kwahiyo waweza kutumia staili rumba au rock music vionjo vikawa ni vya mdumange,nk.kwahiyo nivizuri kujadili hii hoja na wenda tukafika mahali tukaelewana kiswahili. mdau uk.
ReplyDeleteMze Kitime, ni kweli unayosema. Mimi nipo hapa Kinshasa huu mwaka wa 9 sasa, kwa kifupi ngoja nikupe historia ya bendi za hapa na mitindo yao. Hapa kila bendi inatumia mtindo wake kama huko nyumbani, na kila bendi inafanya chini juu ili mtindo wake uwe maarufu shinda wa mwenziwe hivyo utakuta ushindani wa kucheza na uporomotaji wake uwa wa juu sana shinda hapo nyumbani. Huko nyumbani mnajali sana ujumbe katika muziki huku sivyo, na ndiyo maana utakuta nyimbo nyingi za kilingala hazina tungo nzito ukiondoa Franco, tabu Ley, na wazee wa zamani waliotangulia mbele ya haki. Huku kila bendi inakuwa na mtindo wake kama hapo TZ (Sikinde, Sagha rhumba, msondo, zembwela, n.k) ila sasa utakuta ije kutokea labda tuseme msondo imetoa wimbo wa asha mwana seif na ule wimbo umekuwa ndiyo kipenzi cha watu mjini dar, basi kila mtu mtaani utasikia anauimba na kutumia maneno kama cheza msondo na kuonyesha jinsi msondo unavyochezwa, n.k. Na hapa utakuta bendi zingine nazo zinatoa nyimbo kwa kutumia mtindo huo cheza msondo kwani kila mmoja anaupenda. Sasa utakuta wimbo wa asha mwana seif unafifia halafu inakuja zaiko na wimbo utakaopendwa na jamii wakitumia mtindo wa 'madiaba' then pia kila bendi itafuata hivyo hivyo, na ndiyo maana huku utakuta kila mwaka kuna mtindo mpya. Kwa sasa kuna techno malewa, ni mtindo wa kijinga lakini unapendwa na watu wengi haswa watoto wa mitaani, kwa hiyo bendi nyingi za vijana nao wanaiga techno malewa. TZ tukae na mitindo yetu kwani tuko unique na muziki wetu ni mzuri sana. Hapa nina albamu za Vijana, Sikinde, msondo, Tancut alimasi, Kimulimuli, Mwenge, Super rainbow, na nyingine nyingi tu. Kuna wakati naimiss sana TZ hivyo nikipiga nyimbo za nyumbani marafiki zangu wanashangaa kusikia TZ tuna muziki mzuri hivi. Cha kushangaza huko nyumbani mnadharau muziki wenu huku unapendwa, jamani si ujinga huu? kumbukeni miaka ya nyuma haswa ya themanini wakati bendi zilikuwa nyingi na utundu wa upigaji ulifana sana. Kipindi kile kwa kweli kulikuwa na upinzani sana, watunzi waliweza kutupiana madongo ya hapa na pale na wapigaji wa ala kama nyie mlikuwa mna kazi ya ziada kupikuana ki-mapigo, kweli ilikuwa uhondo kwetu mashabiki. nakumbuka Vijana Jazz mlikuwa mnapiga muziki wa aina yake hata zembwela, sikinde ama msondo walikuwa hawasogelei japo wanajiita baba ya muziki na babu ya miziki TZ. Sagha rhumba chini ya solo la Wanted (hana mpinzani mpaka leo hii TZ) na utunzi mnene mlikuwa mbali sana na watu tulichanganikiwa na ujuzi wenu. Maana nakumbuka kule Ilala pale mtaani kila mtu alikuwa na bendi yake aipendayo na wimbo wa bendi yako ukipigwa tu, utawatambia wenzio kwa kuimba kwa sauti ya juu, yaani ilikuwa ni furaha sana. Mwanzoni ya miaka ya tisini ndipo muziki wa TZ ulianza kufifia siyo kwa sababu haukuwa mzuri, lahasha. Kipindi kile kulikuwa na homa ya kupenda kina Yondo sister, Lokasa ya mbongo, na wanamuziki feki wengi tu wa Congo ambao hata huku kin hawatambuliki. Na Ma-dj wengi wa bongo walihamua kuuchuna makusudi tu kwa kuuacha muziki wa kwetu na kuupa upeo muziki wa kigeni. Kingine, Bw. Kitime, ebu angalia kipindi kile Maquis ilipokuja TZ, walikuwa wanapiga muziki lakini si wa kutisha, kwani kipindi kile kulikuwa na wataalam kama kina Dar jazz, Urafiki, Msondo, Western, Afro 70, na bendi nyingi tu ambazo hata maquis walikuwa hawaoni ndani ila ma dj wetu waliibeza maquis redioni kisa walikuwa wanaimba kwa kutumia broken kiswahili, si ni kasumba hii? Na kasumba ama ujinga huu ndio upo sasa kwa ma dj wetu kwani nina rafiki yangu wa karibu sana katika station moja ya redio hapo bongo, yeye hakunificha kaniambia kabisa kuna vijana (wa flava) uenda pale ofisini na dau kutaka nyimbo zao zipigwe redioni na hawa vijana wanashindana kuonga, kwa hiyo hii imekuwa kama ajira nyingine ya wale ma-dj pale station na ndiyo maana utakuta nyimbo nyingi wanazoweka kupigwa ni za kijinga halafu unabaki kujiuliza huyu kijana kaimba nini hapa? Kwa kweli muziki wa kwetu bado ni mzuri mno na tumeendelea sana kwani kuna ushindani wa aina ya pekee kwa sasa na hata tungo si duni, sasa sijui wenzangu mnasikiliza nyimbo za nani?
ReplyDeleteMdau wa Kinshasha ahsante sana kwa ufafanuzi wako, huku bongo naona hilo jambo la uvamiaji vitu visivyo na sababu umeshamiri sana. Ni kweli kuwa vijana wa flava wanaonga ma-dj redioni ili nyimbo zao zipigwe mara kwa mara; na cha kusikitisha zaidi ni kwamba hawa vijana ma-dj wanakusudia kuua muziki wetu wa asili na kuubeza muziki wa nje kwani flava si muziki wetu. Kingine cha kusikitisha zaidi eti utakuta hata magazeti nayo wanaandika fulani kuwa ni mkali ama mfalme/malkia wa mtindo wa muziki fulani wa nje hapa TZ. Hivi najiuliza hapa TZ kweli tuna waandishi wa habari ama ubabaishaji tu. Kumbuka muziki wa Zouk, ni muziki wa asili wa Guadeloupe, Reunion, na Martinique pamoja na nchi nyingi tu za visiwa zilizotawaliwa na ufaransa lakini TZ leo tunaambiwa fulani ni king ama queen wa huo muziki wakati wao wamezaliwa wameukuta, wanachofanya ni kuiga. Kuna muziki wa kwaito pia ambao ni wa south, leo TZ Mr. Nice anaitwa mfalme wa huo muziki. Mr. Nice si mtunzi na si mwana muziki na ndiyo maana hana nyimbo za maana zaidi ya kuimba mapipi pipi tu. Kwa nini TZ tunakuwa wajinga wa kuiga na kuthamini vya nje visivyokuwa na faida kwetu?
ReplyDeleteMze wa Kinshasa ahsante kwa ufafanuzi wako na pia hongera kwa kupenda muziki wako wa asili na wenye tungo za maana. Mimi kila siku nilikuwa nawaambia wenzangu kuwa muziki wa congo hauna maana nzuri kama muziki wetu. Na ndiyo maana kila wimbo wa kikongo utakaosikia redioni lazima watie neno la bolingo kumaanisha mpenzi ama mapenzi. Ile nchi ina taabu kibao badala ya wasanii wake kukaa chini na kuamasisha umma kwa kutunga nyimbo za maana wao wanakilia mapenzi tu, utaimba mapenzi mpaka lini? Kweli kimapigo wako juu sana kutokana na utundu wao wa kutaka kushindana lakini hata sisi tukiamua kufanya hivyo tutakuwa mbali sana na hii tutafanikiwa endapo tutawakalisha chini hawa ma-dj njaa wa kwetu na kuwapa somo juu ya kuheshimu jadi yetu na si kubeza ujinga huu wa flava.
ReplyDeleteMkuu wetu Bw. Kitime ahsante kwa kuanzisha mada hii. Binafsi naona cha msingi hapa ni kwa kila bendi kupiga mitindo yao kama ilivyo sasa. Mbona hapa Bongo kuna ushindani mkubwa tu ila isipokuwa ma dj wetu ni feki sana na wanakatisha tamaa wanamuziki wetu nguli. Ebu angalia nyimbo zinazopigwa redioni hizi za fleva zina uzuri gani? Nyingi hazina maana, utunzi wa ngumbalu, mapigo yenyewe feki hata wasanii wake ni feki. Nakumbuka siku moja nilikuwa marekani (North carolina) na mwenyeji wangu alikuwa anaangalia video za flava, basi yule demu wake (mmarekani mweusi) alikasirika na akataka zitolewe. Mimi sikuelewa nini kinaendelea, nilipomuuliza jamaa yangu akaniambia kuwa demu wake hapendi kuona waafrika wanaiga wamarekani. Nilishangaa sana wakati anatoka n mwaafrika. Siku iliyofuata walikuja wenzake pale nyumbani na tulikuwa tunasikiliza hizo fleva. Haki ya Mungu walitucheka na kutusanifu kama vile wajinga yaani mpaka mimi mwenyewe mgeni niliona haibu kwa nini nilimpelekea jamaa yangu zile fleva. Kumbe huku TZ tunaona fleva ni issue wakati wenzetu hawazimaindi hata kidogo. Kwa kweli ma dj wetu wafikirie hii kitu, tusikuze muziki usio na akili, watu wengi wa nje wanapenda muziki wetu wa asili na si fleva!
ReplyDeleteDanstan,
ReplyDeleteNimefurahishwa sana na maelezo ya ndugu yetu wa kinshasa. Kwa kuwa yuko huko, naamini asemayo kuhusu muziki wetu ni kweli kabisa.
Nami niwaongezeeni ushuhuda kidogo ili kuunga mkono maelezo ya bwana wa kinshasa. Hapa mimi niko Brussels, Ubelgiji, basi ndugu wa Rwanda na Burundi hushinda kwangu jioni kusikiliza nyimbo za Tz ambazo ninazo kwenye laptop yangu. Wanazipenda mno. Na issue kubwa ni ujumbe na upigaji (ingawa hauko mbali sana na wakongo).
Pia kuna bendi moja hapa ya wanamuziki wakongwe wa Kongo ambao nimeunda nao urafiki na huwa napenda kuhudhuria maonyesho yao kwa ajili ya kujiburudisha. Lakini nikikaa nao, wao huzungumzia muziki Tanzania tu. Yaani wanaupenda mno. Kuna mmojawao ananiambia kila siku kuwa huwa anachanganyikiwa akimsikia Rose Mhando na nyimbo zake za Injili. Pia kiongozi wao wa bendi na mkewe ambaye ni mzungu, wananishangaza kwani wanaimba sana nyimbo za Kurugenzi jazz ya Arusha, nyimbo za Twanga pepeta, Dar Jazz, n.k., na wawapo jukwaani, muziki ukikolea wao huweka rap za kiswahili...hasa za twanga pepeta.
Wanasema nyimbo zetu ni tamu sana. kwa hiyo mdau wa Kongo nakubaliana na wewe. Niliwaeleza jinsi Fally Ipupa alivyokuja na kupagawisha hapo dar, wakanishangaa. Yaani wakasema mbona yule sio maarufu kwao, na kwamba hafahamiki sana. Kwa hiyo radio zetu ndio zimemkuza sana, kwani zaidi ya kukata viuno na kuliza sana magitaa...kuna nini katika muziki wake?
Nimeona wanzetu wa Netherlands wamemualika Fally Ipupa kwenda kuwapa burudani. Nilitamani sana wangekuwa wameialika bendi toka Tz. Lakini hawakuweza kwa sababu matangazo yamemkuza sana Fally Ipupa na hakuna matangazo ya kuwakuza wanamuziki wetu huku na muziki wao.
Wale wenye nafasi kama magazeti na ma-Dj wa Radio ni kati ya wale wanaotakiwa kuukuza muziki wetu kati yetu. Wakiu-promote utarudi kwenye chat kwenye anga zetu hapo. Na sisi wenyewe tukishaufurahia, basi na watu wa nje wataupenda, na tutagundua kwamba tuko juu bwana Kitime.
Style tunayopiga sio mbaya ila tuongeze ubunifu, na ushindani, vitasaidia tuzidi kuwa juu. Pia wanamuziki wetu watafute mialiko katika nchi ambazo zinauzimia muziki wetu, kama vila Rwanda, Burundi, n.k.
NB: Bahati mbaya ni kwamba humu tunajadili mambo mengi mazuri lakini hayafiki huko nje kwa walengwa. Ni wanamuziki wangapi wanashughulika na mitandao kama hii? Au basi wanaojua ipo?
Ni kweli wenzangu hapo juu, muziki wa TZ uko juu na unapendwa na watu wengi wa nchi za nje wakati sie wenyewe tunaudharau. Wacongo wanumaindi sana muziki wetu na tungo zake za maana. Mtanisamehe lakini hapa Canada nilashamtafsilia mwanamuziki mmoja nyimbo kadhaa za dk. Remmy na Urafiki (Mtoto wa mjomba na Paulina) ili arekodi kwenye albam yake. Alirekodi na wanamuziki wa Koffi olomid miaka ya nyuma wakati koffi alipokuwa hapa. Ma-dj wetu bwana kwa kweli hawana maana na pengine ni njaa inawasumbua. Pia nasikia ni kweli wamarekani wengi haweapendi kuigwa nasi waafrika, lakini sie tunaona ujiko kuwaiga wao, kwa nini?
ReplyDeleteKaka Kitime, Nakubaliana nawe kwa 100% Katika utafu=iti wangu niliofanya mwaka 2004/05 nilibaini mambo kama hayo, ni kweli kabisa waandishi wenzangu hivi sasa ni wavivu sana, hawataki kujishughulisha kabisa na mbaya zaidi wanajidai ndiyo wako juu kwa kuwa wanamajina kwenye magazeti au vipindi kwenye redio au TV. kweli ukiona makala ya sanaa siku hizi ni braabraa tu, habari sanaa na muziki ni za kupagawisha, kuzindua albam nk. hii inaniumiza sana na mbaya zaidi waandishi wa utashi kama akina Francis Chirwa, Rashid Kejo, Ken Manara, Issa Michuzi.. hawapati muda kutokana na majukumu. Waandishi wetu wa sasa ni wale wa wanaosubiri penalty yaani press conference tu hata uchambuzi wao juu ya mambo ni mwepesi sana hauna tija katika maendeleo ya fani. kibaya zaidi suala la kile wanachoita mshiko linawasukuma kuandika makala ambazo ahazina kichwa wala minguu. utakuta mtu anamsifia mtu kwamba ni muziki mahiri wakati ana nyimbo moja tu tena bado iko studio jamani!!!!! Kuna kitu kinaitwa SANAA PRESTALK, kimeanzishwa ili kuwapa fursa mahsushi waandishi kupata habari za kina na kuwapanua mawazo kwa kuwakutanisha na wataalam, lakini wapi hawaendi kwa sababu hakuna bahasha na wanasema kabisa. Nata wakienda wanachoandika kitu kisichokuwa na tija kwa sababu wanakosa maswali ya kuhoji kutokana na hizo pupa na haraka zao. Sijui lakini naomba tusaidiane...
ReplyDeleteTZ ni nchi isiyo na muelekeo, nasema hivyo kwa sababu hawa waandishi feki inabidi vyombo ama idara ya habari iwatenge. Sawa ndiyo tuna kitu tunaiita freedom of speech lakini siyo kama hivi, utakuta mtu anaandika kitu akieleweki au wala hana uhakika wowote juu ya iko kitu kisha anaitwa mwandishi wa habari. Sasa kuna maana gani mtu unakaa kwenye internet masaa na masaa kunakili maisha ya msanii wa nje wakati hapo nyumbani wasanii wetu kibao wamejaa.
ReplyDelete