Hatimae inataka kuwa. Kama ambavyo wapenzi wengi wa Blog hii wamekuwa wanaomba,mwanga umeanza kuonekana kuwa itawezekana. Wenye afro zao wazitimue au wakachome tena nywele hahahaha, wenye raizon zao, wenye slimfit zao,(kama zitawatosha na hivyo vitambi), wenye superfly, pekos, maxi, midi, mini wazitoe vumbi maana wanamuziki wa zamani wameamua kuwa watafanya show moja kubwa ambapo wanamuziki wa toka enzi za buggy watapanda tena stejeni na kujikumbusha yalivyokuwa. Onyesho hilo ambalo pia litahusisha Madjs wa enzi hizo linategemea kufanyika mwezi July. Tayari Kilimanjaro bendi wametoa vyombo na eneo la mazoezi na wanamuziki kadhaa wamekwisha jitokeza kukubali kushiriki. Fuatilia katika blog hii upate kujua nani na nani watakuwepo. Mapato ya onyesho hilo yataenda kwenye huduma ambayo itatajwa baada ya siku chache.
YOUTUBE PLAYLIST
Sunday, April 4, 2010
Hayawi hayawi.........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Hatimaye.
ReplyDeleteAsanteni kwa hili. Naamini hii ni hatua ya kwanza katika kile ambacho wapenzi wa MUZIKI HALISI tumekuwa "tukililia" kwa mda mrefu.
Natumai hatua itakayofuata itahusisha KUWAENZI wasanii wengi walioifikisha sanaa ya muziki hapa ilipo na ambao wanaanza kusahaulika kwa kuwa tu hawakumbukwi na jamii.
Niliwahi andika kuwa NATAMANI KUONA SIKU YA MUZIKI WA DANSI NCHINI ambao utaenzi watu hawa na kazi zao. Kisha kuona HALL OF FAME wa muziki wa Dansi na wakithaminiwa vema
(http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/02/natamani-kuona.html)
Natamani kuona siku hizi
Mkuu,
ReplyDeleteNaomba utoe ruhusu wadau watoe listi ya magwiji waifikiriayo kuwemo katika zoezi hili. Unasemaje?
Toa mapendekezo
ReplyDeleteMkuu,
ReplyDeleteKwa heshima na taadhima naomba urejeshe hii mada kuleni mwanzoni na utoe ruksa kwa wadau kuanza kutoa mapendekezo. Asante.