YOUTUBE PLAYLIST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
John,
ReplyDeletemwishoni mwaka 69 na mwanzoni 70`s Dynamites walikuwepo walitikisa miji mingi,lakini kama ujuwavyo miaka ile ingawaje tulikuwa na vipaji vya kuzaliwa wengi katika fani ya mziki wa Tanzania,kulikuwepo na matatizo ya band nyingi kutokuwa na uwezo wa vyombo vya mziki ni band chache zilikuwa na vyombo nyingi za wakongo,Salim Willis alijiunga Afro 70 na wengine wakajiunga bendi zingine.
kujibu swali ulioulizwa:
Hauyo aliyekuuliza amekumbuka sawa kabisa,mimi nilikuwa meneja msaidizi katika bwawa la maofisa wa Polisi(POLICE OFFICER`S MESS)
Oysterbay/masaki.
Baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere na hayati Abeid Karume na mzee Rashid M. Kawawa walilifungua katika sherehe iliyofikia kileleni kwa maofisa wetu wa polisi.
Sisi tulipelekwa kulianzisha tulitokea wizara ya utalii wakati ule nilikuwa front office adminstration New Africa Hotel mara tuu baada ya kumaliza masomo ya utalii,nikiwepo New Africa Hotel na Police Oficers Mess nilibahatika kupata nafasi ya kuwa karibu na wanamziki wengi kutoka band tofauti starehe za zamani zilikuwa mahotelini kwa watalii.
Niliondoka nchini 1977 mpaka sasa bado nipo Scandinavien.
Mickey Jones
OLD BOYS-GENARATION OF 70`s
Namkumbuka Otis "Hey Jude dont make it bad take your...and make it better, remember....
ReplyDeleteMkuu Hey Jude ulikuwa wimbo wa Beatles, lakini katika kipindi cha Soul, Wilson Picket nae alitoa version yake
ReplyDeleteHuyo ambaye ame kneel down kulia ni Abdul Abubakar. Tulisoma wote Forodhani
ReplyDeleteJe, aliyesimama wa pili kulia ni Bashir aliyekuwa Sunbursts???
ReplyDeleteJohn yeah ur right ulikuwa Beatles. Nimeuchanganya na "Direct Me".
ReplyDeleteKatika hawa Dynamites alikuwemo pia Cyril Kabarole alisoma Saint Josephs sasa Forodhani akiimba na kupiga rhythim, Mohamed Nyamka akipiga bass, Godfrey Manoni pia wa Saint Josephs akiimba
ReplyDeleteMohamed Maharage Juma
Wakuu,
ReplyDeleteMpaka mwishoni mwa miaka ya 70 ilikuwa bado ni rahisi kwenda muziki na kuwakuta wanafunzi wa shule za sekondari na wachache wengine wa shule za msingi wakiwa wapigaji.
Siku hizi siyo rahisi kukuta wanafunzi wa sekondari au vyuo wakiwa wanamuziki. Kuna maswali mawili ambayo yamenijia:
Swali la Kwanza, nini kilichokuwa kinawafanya wanafunzi wa miaka ya 60 na 70 kuweza kuwa wanamuziki?
Swali la Pili, kilitokea nini katika miaka ya 80 na kuendelea hata wanafunzi wakatoweka katika anga za muziki? Naomba katika hili swali la pili nifanunue ninaposema wanamuziki ninamaanisha waimbaji na wapiga ala na siyo Bongo Fleva au Muziki wa Kizazi Kipya kwa sababu hata kwenye Bongo Fleva na Mziki wa Kizazi Kipya wapo wanafunzi wanaorap na kutengeneza miziki kwenye kompyuta na synthesizer.