YOUTUBE PLAYLIST

Monday, March 29, 2010

Miaka minne toka kifo cha Moshi WIlliam


Tunakukumbuka Moshi. Mola akulaze pema peponi

8 comments:

  1. Moshi William.
    Kwanza niseme ASANTE kwako Uncle Kitime kwa kuonesha umakini wa fikra kwa kumuenzi mwanamuziki mwenzako ambaye (kama ulivyo wewe) amefanya mengi mema ndani ya sanaa hii ya muziki.
    Pili ninaomba ukiweza utujuvye juu ya hiztoria yake kwa ufupi (ama kadri utakavyoweza).
    Nilikuwa na bado ni mpenzi wa nyimbo zake.
    KAZI ZAKE ZITAENDELEA KUKUMBUKWA DAIMA

    ReplyDelete
  2. Kwanza kabisa tunakubali kwa moyo mmoja kwamba Moshi William (Shaaban Mhoja...jina lake la awali) alikuwa mwanamuziki mahiri hapa nchini. Maudhui ya tungo zake, ubunifu wa melody za nyimbo na sauti yake mwenyewe, tutavikumbuka daima.
    Bendi yake inaendelea kusonga mbele na mungu awajalie mafanikio, ila sauti yake inakosekana katika ile safu ya uimbaji kama tulivyoizoea.

    ReplyDelete
  3. Moshi William ni mmoja wa wanamuzuki wanaoongoza kwa kuwa na nyimbo nyingi katika studio ya TBC

    ReplyDelete
  4. Kamaka18:20

    Uncle KITINE nilikuwa na swali ambalo linanisumbua kwa Muda mrefu kuhusu wapiga gitaa la solo.Kuna kundi la wapiga solo mimi nawaita wanapiga solo kavu mfano,marehemu Rwambo,Hamza Kalala na Saidi Mabela.Kuna kundi jingine nawaita wapiga solo laini mfano,Kawelee mutimwana,Jah mangelesange(alikuwa mpigaji wa Bantu group),marehemu joseph Mulenga.Swali hivi ni kitu gani wanakifanya kwenye gitaa mpaka likatoa mlio wa kutofautiana kati ya wapiga solo laini na Kavu.

    ReplyDelete
  5. Mkuu kwanza naitwa KITIME, haya hao wapigaji watatu uliowataja Franco,Hamza Kalala, Said Mabela wamekuwa wanapiga style moja ambayo ilitumiwa sana na Franco, wanamuziki huuita Kent(sijajua kwanini),ambapo mpigaji hushika nyuzi aidha ya kwanza na ya nne au ya pili na ya sita. Jina kuwa solo kavu lilianza pale ambapo Franco alirekodi nyimbo kwa kutumia gitaa lisilo la umeme (accoustic) akiwa anapiga style hii ya kent, kuna wimbo mwimbaji mmoja wa wakati huo wa OK Jazz/ alikuwa anasikika mwimbaji mmoja akisema " aaa mama sikia muziki inalia kama iko ndani ya mayi" muziki unalia kama uko kwenye maji. Wapiga solo hao wengine walijulikana zaidi kwa staili niite ya upigaji wa kawaida japo sijawahi kusikia mtindo huu ukiitwa kwa hilo jina 'solo laini'.

    ReplyDelete
  6. Anonymous23:41

    Shukran sana kaka Kitime kwa kutukumbusha Mkongwe wetu TX,actually wengi wanamlinganisha na Marijani au Mbaraka. Mwingine mwenye solo laini ni Ridhiwan Pangamawe wa Msondo. Kaka Kitime, Shaban Yohana "Wanted' tunamuweka kundi gani humu? Kwa nini aliitwa "Wanted" na yuko wapi? Najua mlikua nae Vijana.

    ReplyDelete
  7. Anonymous22:09

    Tuache ubishi usio na sababu. Katika TZ hajawahi kutokea mpiga solo imara kama shube wanted. japo shakashia alijitahidi kuziba pengo lake pale vijana lakini wanted kwa kweli hana mpinzani, kwa kule congo naweza kusema anafananishwa na beniko popolipo yule wa koffi, ila kwa sasa nasikia yuko na werrason.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...