YOUTUBE PLAYLIST
Sunday, February 7, 2010
Wanamuziki kutoka Kongo
Huwezi kuongea kuhusu muziki wa bendi Tanzania bila kutaja wanamuziki kutoka Kongo. Kuna sababu kadha wa kadha. Kwanza historia. 1945 kwa sababu za kipropaganda Wamarikani walianzisha kituo cha radio kikubwa katika mji unaoitwa sasa Kinshasa hii iliwezesha muziki wa Wakongo kusikika katika eneo kubwa la Afrika ya kati na mashariki, 1947 ndugu wawili wa Kigiriki walianzisha record company katika mji unaoitwa sasa Kinshasa na santuri za wanamuziki kama Wendo Kolosay na nyimbo kama Akili ya bibi sawasawa mtoto mdogo zilisambazwa chini ya label ya Ngoma na Loningisa na kusambaa sana nchini kwetu, mambo haya mawili yaliweza kuusambaza muziki wa Kikongo katika maeneo yaliyoizunguka na kufanya wanamuziki kuanza kuiga mipigo ya Wakongo. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilianzisha kuhama kwa wanamuziki kutoka Kongo na kuja Afrika Mashariki. Kati ya wanamuziki wa kwanza kuja huku ni Paschal Onema. Lakini baada ya hapo zilikuja Bendi nyingi. Nakumbuka Super Bocca na wimbo wao Suzana mwana Tanzanie, Maquiz du Zaire, Fauvette haya jamani karibu tuendelee .........Pichani ni Mzee Makassy mara tu baada ya kuingia nchini kutoka Uganda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.
TANCUT ALMASI ORCHESTRA wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...
-
Mara baada ya kutoa ule wimbo maarufu wa Kisambaa Shakaza, Eddy Sheggy mwenyewe na Wasambaa wengine wakaanza kuitwa Shakaza. Eddy Sheggy ali...
-
Suleiman Mbwembwe, aliyekuwa anajulikana pia kwa jina la Electronic Voice, alikuwa mwimbaji na mtunzi aliyeng'ara katika enzi zake. Aki...
-
Maneno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili...
Hapa kitine umenikumbusha kitu kimoja, ingawa umri wangu si mkubwa sana lakini nimebahatika kusoma kidogo kuhusu historia ya muziki wa Congo, Huyu jamaa uliyemuelezea humu ndani WENDO COLOSAY wenyewe walikuwa wakimwita jina la utani WENDOSOR ndio alikuwa mmoja wa waasisi wa muziki wa Congo.
ReplyDeleteNi kweli Marehemu Mzee Wendo anachukuliwa kwa umuhimu wa juu na wanaoijua historia ya muziki wa Kongo. Yeye na kundi lake ndo walikuwa watu wa kwanza kuanza kutoa santuri katika label ya Loningisa kwenye mwaka 1947.
ReplyDeleteKaka Kitime hongera sana kwa kutupa vitu kama hivi.Pia na wengine wanaotoa maoni nawapongeza maana wanaongeza katika jungu hili la ufahamu wetu wa muziki
ReplyDeleteMoses Gasana
City University London
John Kitine unaweza kutufafanulia 'bifu' la kimuziki baina ya mzee wa dazani ndala kasheba na nguza viking. story za uswahilini sasa hazina nafasi tena.
ReplyDeletetafadhali.
Kwanza nisahihishe naitwa KITIME,huwa nakosa raha kuitwa Kitine. Sikumbuki Bif kati ya watu hao wawili, ninachokumbuka ni ushindani mkali wa bendi zao. Bendi ya Maquis ya Nguza,makao yake makuu yalikuwa White House Ubungo, wakati Kasheba na Orchestra Safari Sound walikuwa Safari Resort Kimara, ukaribu huo uliwafanya kila mmoja ajitahidi ili apate watu. Hivyo basi wakati Maquis walipoanza mtindo wao wa Ogelea Piga Mbizi, OSS wakanzisha mtindo wa chunusi,kuwa ukiogelea utakamatwa na chunusi, wapenzi wao walikuwa wa ukweli kwani hata muziki wa bendi hizi ulikuwa tofauti. Na Ndala Kasheba aliwahi kupigia Maquis wakati wa Nguza
ReplyDeleteJFK naomba unikumbushie enzi za Santa Fe pale juu Gateaways. Je wale si ndio walikuwa wanamuziki wa kwanza kuja Tanzania toka Kongo?
ReplyDeleteKitime,
ReplyDeleteahsante sana kazi nzuri unayotupa juu ya muziki 'halisi' wa Tanzania, ni elimu tosha tunayopata toka kwako na kwa wachangiaji.
...Leo nina swali dogo; hivi wimbo wa FANTA WANGU(original) uliimbwa nchi gani? kama unaweza tafadhali sana tuwekee clip yake tufaidike!
Fanta wangu ulikuwa utunzi wa Kalala Mbwebwe, aliurekodi mara ya kwanza Kenya na baadae akawa anaupiga Tancut almasi na mara ya mwisho ulirekodiwa na Papy Nguza. Kalala alihamia Tancut Iringa na hata baada ya Bendi hiyo kufa aliendelea na endi za Iringa kama VICO Stars na Ruaha International hadi alipofariki.
ReplyDeleteMichuzi unashtua mioyo ya wengi ukianza kutaja Gateaways. Sina uhakika kama Santa Fe walikuwa ndiyo bendi ya kwanza ya Wakongo kuja nchini, japo ntatoa jibu la uhakika zaidi muda si mrefu, lakini ikumbukwe kuwa wanamuziki kutoka Kongo walianza kuja upande huu mara baada ya mauaji ya Lumumba mwanzoni mwa miaka ya 60. Japo kwa mwanzo walianza kwa kuja mmoja mmoja na si kama bendi.
ReplyDelete