Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Saturday, June 19, 2010

Disco

Haya djs walikuwa, na bado ni watu muhimu katika shughuli za muziki Tanzania, labda nikupe maelezo mafupi. Baada ya Biribi kupumzika, akazuka kijana huyu, kwanza kwenye parties maeneo ya Upanga, na baadae kuwa dj maarufu aliyejulikana kama Dj Emperor, akiburudisha sana pale Agip Motel na kisha kuhamia ghorofa ya saba New Africa Hotel, alifanya mambo makubwa Arusha pia wapenzi wa disco mnamkumbuka? na disko lake liliitwaje?
2 comments:

Anonymous said...

Huyu ni Bwana Joseph Kusaga mkurugenzi wa Clouds Media Group. Kweli ametoka mbali maana ninamkumbuka dakika za mwisho mwisho pale 77 hotel tulikuwa tunagombania kumsukuma katika gari yake ya enzi hizoo VW ili atambue uwepo wetu na kisha kutupatia namna ya kuishi kwa siku hiyo. Mungu akubariki sana Joseph

Anonymous said...

Haswa ni Joseph Kusaga katika enzi hizo,ukianzia kwenye parties mpaka kufikia New Africa na kutawanya disco lake sehemu mbalimali ikiwemo Arusha na Morogoro Hotel.Mungu akuzidishie kwa uatafutaji toka huko ulikoanzia.

Adbox