Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, April 14, 2010

Vyombo vya habari

Katika kusoma magazeti ya zamani,(nitazitoa baadhi ya makala hapa), imeniijia kuwa tunatatizo kubwa la uandishi na utoaji wa habari za shughuli za muziki. Makala za muziki za siku hizi, nyingi ni kuhusu nani kapagawisha wapi au mcheza show gani alikaa vibaya au ana uhusiano na nani. Kimsingi ni kama vile taarifa kuhusu muziki ni gossips zinazoendelea katika uwanda wa wanamuziki. Hakuna taarifa ya taaluma katika muziki huo. Unaweza kupata taarifa nzuri kuhusu Beyonce lakini ukakosa taarifa kuhusu Anna Mwaole ambaye yuko jijini Dar es Salaam. hili liko hata kwenye vituo vya redio vya wilayani, ambako huko nako watangazaji wengi wanaiga kuanzia uongeaji, mpangilio wa vipindi, maadili na kadhalika kutoka redio maarufu za Dar es Salaam.
Huko wilayani nako wanadai hawana taarifa za wasanii wa hapo wilayani kwa kuwa wasanii hawaleti taarifa zao, lakini mtu huyohuyo atakaa masaa kadhaa kwenye internet akitafuta taarifa zote kuhusu msanii wa nje. Napata taabu kujua aina ya mafunzo wanayopata waandishi katika vyuo vya uandishi siku hizi. Na tena nakumbuka kuwa wandishi wengi wa zamani hawakupitia vyuo kama vilivyo siku hizi kwanini hakuna ubora wa uandishi sasa? Kwanini tunakosa ufanisi zaidi siku hizi ? au ni mimi ndio mwenye kuona kuna tatizo ambalo halipo? katika makala nitakazoziposti hapa ambazo ni za miaka ya sabini naona kuna maelezo ambayo nayakosa katika uandishi wa siku hizi.

6 comments:

Anonymous said...

Kazikwelikweli,Mwakitime.unajuwa sasa hivi biashara imetawala maeneo mengi,kwa hiyo mwandishi anaona ni heri akiandika habari ya Akon italipa kuliko kuandika habari ya mtoto wamarehemu mzee mwinamila,na hiyari ya moyo.Hivyo basi ya wezekana kabisa uko sahihi ama la unapingana na wakati.kuhusu taaluma ya uandishi ni pana sana,sas sina uhakika na elimu waipatayo kama wana uwezo na hamasa ya kuandikia ambo ya sanaa kwa mapenzi ya hali yajuu, bila kupotosha uma wa wasomaji.badala ya kuandika amekoga nyoyo za watu aandike kwa undani mapungufu ya msanii yule ili kumjenga,ama kumpongeza kwa kazi nzuri aliyo ifanya nahapa nikiwa na maana kufaya uchambuzi wa kina unao shabihiana na taaluma husika ya sanaa,ama ya maonyesho au kuchora nk.pia kuna kitu nafikiri nita kuja kuwasiliana nawewe sikumoja,lina husiana na hili la uandishi,kuhusu ziara za wana muziki wa kitanzania nje ya nchi,na jinsi ukweli unavyo pndishwa. kwa maneno yaleyalw ,"fulani amekoga nyoyo za mashabiki uk".haya naomba kuishia hapa kwa leo,kaka s

Anonymous said...

Bw. Kitime uyasemayo ni kweli kabisa. Unajuwa siku hizi hapa TZ kuna ile kitu kinaitwa kuiga ili uonekane nawe umesoma. Utakuta mtu anaongea english yaani ile broken mbele ya kadamnasi ili naye aonekane anajuwa kuonge english. Na pia mtu atajitahidi kuimba wimbo wa beyonce huku akitumia broken english apate sifa. Na waandishi wetu hujitahidi sana hata kutafsiri makala ili wajuwe tu msanii wa nje anafanya nini, yaani mtu anapoteza muda wake kutaka kujuwa msanii wa marekani ana nini nyumbani kwake na alianzaje kimuziki ili awasumulie wenziwe uswahili si ujinga huu? Hali halisi, mmarekani mweusi tupende tusipende hana mpango nasi waafrika, hao wanaokuja bongo wanakuja tu kwa misingi ya kibiashara ama wameishiwa kule marekani wanakuja kusafisha image zao tu. Hivi kwanini hatuelewi hili? Utakuta dj anaongea kiswahili huku akichanganya kiingereza broken kisha anatia fleva kulinganisha na miziki ya kimarekani, si ni ushenzi huu?

Blackmannen said...

Mzee Mwakitine,

Uandishi wa wanahabari wetu ni mbovu saaana tena haufai na haulengi katika kuelimisha, bali ni umbea mtupu.

Kwa kuileta mada hii hapa, hapo ndipo uliponigusa kabisa. Magazeti ya siku hizi yana ajiri waandishi kwa ajira ya chini, watu wenye elimu ya darasa la saba, wanapelekwa kozi miezi miwili mitatu, mtu anapewa nafasi ya kuandika gazetini au kutangaza redioni.

Je, unadhani mtu mwenye elimu kama hiyo anawezaje kuchambua mambo ya kiuandishi ili kuwapasha wasomaji wenye upeo mkubwa wa kuelewa mambo?

Ili kuzidi kuficha magugu ya uandishi mbovu, waandishi wa siku hizi wanajazilizia habari waandikazo kwa picha na kuweka video. Hapo mtu anaona katoa habari kamili.

Wasanii wetu ndiyo kabisaaa wamechanganyikiwa. Mtu unakuta anaongea kiswahili chenye lafudhi ya kiingereza cha Kimarekani weusi. Tangu lini kiswahili kikawa na lafudhi ya Kiingereza cha Kimarekani????

Mimi ninapokutana na Msanii wa Kitanzania mwenye tabia hiyo, huniisha hamu ya kupenda miziki yake au filamu zake.

It's Great To Be Black=Blackmannen

Mliakuvana said...

Mnoge? Uandishi wa habari wote ni mbovu, sio muziki tu! Hata ukiangalia uandishi wa habari za kibiashara nao ni mbovu sana na inaonekana hakuna waandishi wa aina hii. Wakiandika kwa kiingereza unategemea wanatumia MS Word but why spelling na gramatical errors kibao? Nadhani wanaignore spell and grammer checker!
Hata uandishi wa TV una makosa tele! Iweje hizi draw za makampuni ya simu, vinywaji etc habari zake zitokee kwenye michezo na sio kwenye biashara? Eti kwa sababu wanasema mchezo wa bahati nasibu (au promotion yeyote) utachezwa siku fulani! Labda hiyo kucheza ndio imekwenda michezo lakini muandishi wa kweli wa mambo ya biashara angeelewa kwamba hiyo ni promotion au marketing na iende kwenye biashara instead of michezo. TBC1, ITV are guilty of this.

Patrick Tsere said...

Thank you very much John. President Mkapa has been vindicated at last. Sasa mnaelewa kwa nini Rais Mstaafu anawadharau waandishi wa habari wa Tanzania. Sasa mmeelewa?

I can tell you viongozi na wanasiasa wa Tanzania wana raha sana kwa sababu waandishi wa habari wa nchi hii hawajui udadisi na they are not informed hata kidogo.

Ila kwa udaku aah ai ndilo walijualo.

Anonymous said...

we umeona wapi mwandishi wa habari anakaa kwenye internet masaa kibao kupoteza muda wake kunakili mambo ya jay z ama beyonce kisha anakiri kwenye Nipashe. Eti anaacha kutembelea walengwa hapo TZ anaenda kwenye internet kutafsiri vitu visivyo na msingi katika jamii yetu, hivi inakuja akilini hii kweli? Utaona mwandishi wa habari kaandika mwana fleva fulani ni msanii wa ngfuvu ama mwana muziki mashuhuri, hivi hapa TZ kuna mwanamuziki gani wa fleva ambaye ni mwanamuziki kweli? wote ni feki tu, kuimba hawajuwi ila wanauza sura tu videoni. Katika muziki wa fleva hakuna mwanamuziki anayejuwa kuimba zaidi ya lady jay dee, nasema hakuna woooooooote si wanaume si nani ni feki.

Adbox