Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Saturday, April 24, 2010

Maquis Original


Maquis Original wakiwa katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. Mwenye nyeusi tupu akiwa na gitaa ni Dekula Kahanga Vumbi, wa pili toka kushoto na suruali nyeusi ni Issa Nundu haya tuwataje wengine hapa.

11 comments:

Anonymous said...

BW.KITIME, HAPA NAWAKUMBUKA, L-R: WA KWANZA (IN BLUE) NI MUKUNA WA MUKUNA ROY, WA TATU(IN WHITE) NI MULENGA KALONDJI, HUYU NDIYE ALIKUWA MWANZILISHI NA MMILIKI WA BENDI YA MULE MUVA, WA NNE NI MUTOMBO AUDAX,NA WA TANO NI MUKUMBULE PARASH, HUYU ALIIMBA WIMBO BANGUNGI, NA MWAKA WA WATOTO AKIWA NA BENDI YA KYAURI VOICE...

Anonymous said...

Nampongeza sana Vumbi kwa kukumbuka atokako na kuitembelea Tanzania mwaka jana, takriban miaka 18 tangu aondoke nchini na kuhamia Sweden. Natarajia wanamuziki wengine waliowahi kuishi Tanzania kabla ya kutimkia ng'ambo watafuata nyayo zake.

John Mwakitime said...

Hata sasa hivi Vumbi yuko Dar anaondoka kurudi Sweden wiki ijayo.

Anonymous said...

Kama sikosei hizi zilikuwa ni enzi za 'super sendema' mwaka 1990, baada ya Assosa kuondoka na kujiunga na Legho Stars. Kipindi kifupi baadae kulikuwa na mabadiliko mengine ambapo walikuja watu kama Kivukutu, Freddy Butamu na Bobo Sukari.

Anonymous said...

Mdau wa kwanza shukrani kwa kutukumbusha majina ya wana Maquis. Julius Nyaisanga alivyokuwa akiyataja majina ya hawa jamaa kwenye Club Raha Leo Show ilikuwa burudi kwelix2. Kulikuwa kuna Banza Mchafu, nafikiri alikuwa akipiga gitaa la bass kwenye hii bendi.

Anonymous said...

HATA KEPI WA NJENJE NAYE ALIPIGA BASS MARQUIS WAKATI FULANI.

Anonymous said...

Keppy Kiombile kapigia Maquis 1986-1987,kisha kahamia Afriso Ngoma,ila hakukaa akarudi tena Maquis ndio kachukuliwa na Kilimanjaro...

Kutoka kushoto ni Roy Mukuna,Issa Nundu,Mutombo Audax,Parash Mukumbule,Kwempa Rissasi,kaumba kalemba.Wapiga Magitaa ni Mulenga Kalonji,Steven Kaingilila na Vumbi Dekula.Drums ni Matei Joseph.Hii ilikua jamuhuri Stadium Dodoma baada ya safari ya pili kutoka Muscat Oman,Maquis ilikua bendi ya kwanza kutoka Tanzania kufungua safari za Oman.

Anonymous said...

huyo nyuma mwenye white suti anayepiga gitaa ni nani?

Anonymous said...

Huyo mwenye suti nyeupe ni Marehemu Mulenga Kalonji "Vata" mpiga rythm guitar, alikua akimiliki bendi ya Mule Muva katika miaka ya 86 huko Lusaka Zambia baada ya bendi kufa... akarudi tena Maquis 1988

Anonymous said...

Huyu wa kwanza kulia ni mmoja wa wale mapacha Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa. Mmoja wao nasikia ni marehemu.
Hongera kaka kwa kutukumbusha muziki wa enzi hizoooooo.

Anonymous said...

Huyu wa kwanza kulia ni mpiga Tarumbeta, Marehemu Kaumba Kalemba yeye ndiye katunga Nyimbo ya Makumbele.

Wale Mapacha,mmoja wao ni Marehemu yaani Kyanga Songa ila Kasaloo Kyanga yuko hai...na bado anaimba katika Bendi fulani Dar-Es-Salaam.

Kwa kweli tuzidi kumpongeza Mr. John Kitime kwa kazi nzuri anayoifanya...
Sababu Muziki wa Rumba ao Bongo dance umesaulika Tanzania.
Vyombo vya Habari havitangazi ipasavyo Muziki huu...

Adbox