Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Tuesday, February 16, 2010

Kwa heri Juma Mwendapole

Kwa masikitiko makubwa nimepata taarifa ya kifo cha mdau muhimu wa muziki wa dansi Juma Mwendapole. Amefariki Ijumaa tarehe 12 February 2010 na kuzikwa kesho yake. Mwendapole ndiye aliyekuwa mmiliki wa Bendi ya Afriso Ngoma iliyokuwa na wanamuziki maarufu kama Lovy Longomba. Kwa miaka ya karibuni wanamuziki wengi wamekuwa wakimtegemea kwa kukodi vyombo vya muziki toka kwake. Bendi nyingi zisingekuweko kama si msaada wa Juma Mwendapole.
Mungu Amlaze pema peponi Amin

9 comments:

Danielle said...

Please can you tell me if this is Baba-Issa of Msasani district?

John F Kitime said...

Unfortunately I have to say Yes. Pole sana

Mzee wa Changamoto said...

Uncle John.
Naomba unikumbushe / unisaidie kuweka kumbukumbu sawa. Afriso Ngoma ndiko alikoibukia Ally Choki ama Eddy Sheggy? Ni bendi hii iliyoimba Milima ya kwetu? Najaribu kuweka picha sawasawa lakini naona nahitaji msaada wako.
Asante

SIMON KITURURU said...

R.I.P Juma Mwendapole!

John F Kitime said...

Hapana Choky aliibukia Bantu kwa Hamza Kalala, bendi iliyoimba Milima Ya Kwetu ilikuwa ni Super Rainbow,bendi ya Mwananyamala, waimbaji wakiwa Eddy Sheggy na Emma Mkelo

Danielle said...

Ndiyo pole sana :( I lived at their home in 2007 and they treated me like family. Please send my sympathy to mama, Issa, Saidi and my little toto Salima.

Mzee wa Changamoto said...

Asante saana Uncle
Naendelea kujifunza na kuboresha kumbukumbu zangu.

Anonymous said...

KWANZA NATOA POLE KWA FAMILIA YA MWENDAPOLE KWA MSIBA,MOLA AILAZE ROHO YAKE PEPONI.

DEKULA KAHANGA SWEDEN

Anonymous said...

pole kwa familia na wadau wa muziki hapa africa na ulimwenguni kote tuko pamoja kaka Kitime naamini kwa pamoja tunaweza kufikisha ujumbe na kutangaza muzkiki wetu mbali zaidi

Adbox