YOUTUBE PLAYLIST

Thursday, September 30, 2010

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika


Wengi tunaufahamu wimbo Sikujua Kama Utabadilika, wenye maneno yafuatayo....
Ohhh Sikujua kama utabadilika
Ohhh Ulimwengu kweli una mambo mengi
Baki salama oo kuonana nawe ni majaliwa
Chorus
Utalia utalia ooo usinione, Mombasa mbali, Kakamega mbaali......................
Wimbo huu ulitungwa na Wilson Peter kama kijembe, baada ya mpiga rythm wa Simba Wa Nyika, Prof. Omar Shaaban kwenye mwaka 1978 kuondoka na karibu kundi zima la Simba wa Nyika na kwenda kuanzisha Les Wanyika ambao nao waliokuja na vibao vikali sana katika album yao ya Sina Makosa.

14 comments:

  1. Anonymous01:03

    Kusema ukweli bwana kitime sijui niseme nini au nianzihe wapi sabababu unikumbusha mblali na hiyo nyimbi niko nayo kwenye cd nakumbuka vizuri sana nyimbo hiyo irirudiwa upya uku ulaya na mzee koko kayinda mwanzilishi wa mangelepa akapiga tumba ni safi sana,mziki wa hawa wakongoman wa leo ni kelele tuu na wanapiga staili moja kama wera son jb mpiana au koffi au ferre gola zamani muziki wa kitanzania ulikuwa ni mtamu mno ukisikia bima lee ni moto na mziki wao no tofauti na wa msondo au sikinde au makassy au vijana jazz ,Tan cut alimasi,uda jazz band ,au jamuhuri jazaz au tabora jazz,oss bwana kitime hongeara kwa kazi ya kuelimisha jamaa kuhusu mziki wa Tanzania,leo hii utasikia eti akudo ndio wazee wa masauti sauti gani?ukisikia nyimbi za ddc za miaka ya 80 mpaka 95 hawa jamaaa hawifiki hata nusu au nyimbo za kina oss au maquiz au tan cut alimasi,au dr remmy ongara naomba watanzania tuanza kupenda vyetu ,ukienda congo autasikia wanapiga nyimbo za kiswahili au kuimba kiswahil naomba sana serikali iangalia sana kuhusu muziki unaopigwa tanzania kwenye radio asilimia 60 au 70 uwe mziki wakitanzania na wenye lugha ya kiswahili au mziki wa asili.Ezi za mwalimu rtd ndio alikuwa championi wa kupromoti muziki wa tanzania pia nyimbo za tanzania zifadhiwe kama hawa wenzetu wa uku,kwa mfano nyimbi za jimmy reeves,peter tosh.la mwisho naomba watanzania tuupende mziki wetu na lugha.
    asante mzee kitime
    yusef france

    ReplyDelete
  2. Anonymous08:47

    Balozi JK,

    Watu hawa walipiga muziki mzuri sana....tafadhali nisaidie line up yao ilikuwaje? nina tabia ya kutaka kuwajua wapigaji wa nyimbo ninazosikiliza..sasa nyimbo za band zetu hatupati taarifa za kutosha..tofauti na wenzetu ambao huwa wanaweka wazi wachangiaji wote ktk kuandaa nyimbo zao....pia hapo juu kwenye picha naona magitaa manne, nimekuwa nikihudhulia maonyesho ya band nyingi lakini siku hizi naona magitaa matatu tu..huko nyuma band kama Afro 70, Mlimani Park, Bima lee niliwahi kushuhudia wakiungurumisha magitaa manne na kweli ukisikiliza kwa makini unayasikia jinsi yanavyojaza muziki.....nadhani upigaji huu unahitaji umahiri wa hali ya juu hasa katika kuandaa na kupiga wimbo bila kuingiliana.

    Hata Muziki wa Congo ukisikiliza nyimbo za zamani unasikia magitaa manne.....sasa sijui kama ujio wa organ/key board umeua gitaa moja? ukipata muda tafadhali tuchambilie hili.

    Nashukuru sana kwa hisani yako ya kutugawia ulicho nacho hasa sisi walevi wa muziki.

    -Muarubaini

    ReplyDelete
  3. Anonymous10:32

    Mkuu,

    Album hii iliitwa Pepea! Ina vibao 7:

    1: Mwongele

    2: Wenzako

    3: Pamela

    4: Sikujua Utabadilika

    5: Nakupenda Cherie

    6: Pole Pole na

    8: Maria

    Les Wanyika walikuja na Album ya Amigo iliyokuwa na na vibao 8:

    1: Amigo

    2: Sina Makosa

    3: Afro

    4: Nimaru

    5: Pamela

    6: Tamaa Mbaya

    7: Maisha na Mapambano

    8: Paulina

    _________________________________-

    Mkuu,

    Kuhusu Wanyika weave naoamba tumrejee mtafiti Doug Patterson!

    ReplyDelete
  4. Anonymous14:15

    Ndugu Kitime,asante kwa kutupatia
    uhondo na kutuamsha kutoka kwenye usingizi mzito ambapo habari nyingi kuhusu muziki wetu wa miaka michache tu iliyopita unaanza kusahaulika,matokeo yake watu wanashabikia mara Fm muzika mara akudo,kusema ukweli kama alivyosema mtoa maoni wa kwanza miziki hiyo ni makelele tu hata saauti za waimbaji hazina utamu wowote ukilinganisha na hao Simba Wanyika,Sikinde,OTTU,Dar int.Marquiz,Tancut,Dr.Remmy na bendi nyingi za zamani hakukuwa na makelele na kutaja majina ya watu mwanzo hadi mwisho.Hata tukirudi upande wa Congo pia akina Fraco,Tabu Ley,Pepa Kalle nk.waliimba nyimbo nzuri ingawa hatukuwa tunaelewa maana,na hawakuwa na makelele kama wakongo wa siku hizi.pia natoa ushauri wanamuziki wa ki tanzania tuache kuiga miziki ya aina hii na tuudumishe muziki wetu kama ulivyokuwa awali.Mini nilikuwa na hadi sasa ni mpenzi mkubwa wabendi ya Simba Wanyika kule Nairobi miaka hiyo,Pia mwana muziki mmoja kati ya hao Simba Wanyika Abbu Omar nilisoma nae Sekondari Songea Boys.naomba niwajulishe majina ya hawa wanamuziki kama waanavyoonekana kwenye hiyo cover ya Album yao.Juu toka kushoto ni George Peter,Joseph Just,Wilson Peter na chini toka kushoto ni JOhn
    Olwenyo-rasta man(mkenya)Maneno Shabani(tangu enzi za Morogoro jazz)Abbu Omar,Prof.Jnr huyu Abbu Omar kwa sasa anafanya shughuli zake za muziki nchini Japan pamoja na Fresh Jumbe,hilo ndili kundi lililorudisha hadhi ya Simba Wanyika,baada ya Prof.Omari Shabani
    kuchomoka na wanamuziki wote kwenda kuunda Les Wanyika.
    J.Mdoe,Washington Dc.Usa.

    ReplyDelete
  5. Baada ya muda mfupi tutapata mengi kuhusu Simba wa Nyika na clan zilizozaliwa toka kwanke, nimeweza kupata mengi toka kwa mwanamuziki ambae alikaa Simba wa Nyika kwa miaka 10. Nasubiri picha kabla ya kuleta habari hizo hapa.

    ReplyDelete
  6. Anonymous13:09

    Anony 15:03 umezungumza maneno ya busara,muziki wa Kongo umekuwa monotone hata Lutumba Simaro kasema katika interview moja hapa...haya mabendi yamekuja na staili ya Kikongo sioni kipya wameleta TZ bali ni kopi za akina J.P na Werra...Kinshasa kwenyewe ukiimba Nyimbo ya Kiswahili inakuwa Siasa hawapendi...kwangu Wazee wamasauti ni Msondo Ngoma na Sikinde.Medisas za Tz lazima wa Promoti Muziki wa Kiswahili...asante John kitime

    ReplyDelete
  7. Anonymous17:54

    George Peter Kinyonga (RIP), anayeonekana juu kabisa kushoto, ni miongoni mwa wanamuziki waliompa hamasa kubwa Moshi William (RIP) alipokuwa anachipukia katika muziki. Hili hata Moshi mwenyewe alikuwa akilisema wakati wa uhai wake.

    ReplyDelete
  8. Perez03:00

    Ooo hoo hoho,
    Sikujua kama utabadilika... x2

    ...Najuta kupoteza aa, wakati waangu, nyumbani kwako...,

    ...Baki salamaaa, kuonana nawe, ni majaliwa....,

    Ooo hoo hoho,
    Ulimwengu kweli una mambo mengii.

    Yaani! We acha tu

    ReplyDelete
  9. Anonymous18:09

    Ukweli ni nikwamba muziki wa tanzania na congo unatokea kwa baba moja na mama moja ,cuba katika historia ya muziki wetu ni kwamba miaka 1930 mpaka 1940 Tanganyika ilikuwa na bendi za muziki wa dansi ambao ulikuwa ukipigwa kwa staili ya cuban chacha au rumba,muziki huu miaka nenda rudi ndio wakauperak mbele na kuanza kupiga swahili rumba sawa sawa na cuban rumba,ndio ukwa mwanzo wa au msingi wa muziki wa dansi na huu msingi tunao useema nikuanzia kwenye mpangilio wa vyombo na kwenye uimbaji pia,kwa mfano ukisikia nyimbo za Tanzania za zamani utasikia hakuna tofauti na nyimbo zilizokuwa zinapigwa na kina franco au tabu ley au wendo kolosy the GOD FATHER OF CONGOLIES RUMBA au Dr Niko,huu msingi uliendeleza muziki wa dansi ndio maaan ukisikia nyimbo za zamani za Tanzania ni tamu si kwa maneno tuu bali hata upiga wa vyombo au kuimba kwenyE key au note zile za kimuziki ni tofauti na leo kabisa wasomaji popete pale mlipo naomba msikia nyimboya ddc mlimani park ubaya ulianza zamani waimbaji wakiwa bitchuka, mzee wa busara mzee nguruma wakina mkanyia utasikia kweli hawa ni wanamuziki sio bongo flava au fm academia au nyimbo ya marehemu mbaraka mtaa wa saba alipiga gita ya soro katika mahazai ya jazz lakini akaifanya na stairi ya muziki wa dansi au sikiliza nyimbo ya mzee kiki jk kikwete au mimi na wewe tuu. kwa hiyo maoni yangu ni kwamba bwana kitime razima turudisishe azai ya muziki wa kiTanzania na siyo muziki wa kicongo man hatukatai muziki wa kicongo ila tuna taka muziki wa kitanzania uwe namba moja bendi zinazo piga muzuki wa kitanzania zipewe nafasi kubwa katika burudani muziki tz.
    many thanks next time
    yesf paris

    ReplyDelete
  10. Anonymous01:59

    JK
    WEWE MWENYEWE UKIWA KAMA MWANA MUZIKI NIKITU GANI HASA KILICHOPELEKEA KIZAZI CHA SASA KUTOKUWA NA WAIMBAJI WENYE UWEZO KUIMBA,KUTUNGA NA KUFIKISHA UJUMBE KWA JAMII.WAIMBAJI KAMA SALUM ABDALAH,GEORGE NA WILSON PETER,MBARAKA MWISHEHE,JOHN SIMON,JUMA KILAZA,MOHAMEDI KIPANDE MUHIDINI GURUMO.WAKARITHISHA MIKOBA KWA KIZAZI KIPYA MARIJANI RAJABU,PATRICK BALISIDYA,JAMES MKUMBO,HEMEDI MANETI EDDY SHEGY,HASSAN BICHUKA,COSMAS CHIDUMULE MOSHY WILLIAM,MAX BUSHOKE,SELEMANI MBWEMBWE NK,NINI KILICHOPUNGUA MPAKA WANAMUZIKI WETU WA LEO WANAIMBA UKUTII UKUTIII,YANI MI BADO SIJAELEWA KIMETUKUTA NINI KATIKA MIZIKI YETU,HONGERA SANA KWA KAZI NZURI.

    ReplyDelete
  11. Anonymous14:51

    Jamani we Kitime hizi raha mbona tunafaidi...sikujua kama utabadilika oooh".

    Maselepa a.k.a "Kama Zamani"
    Zamani Sports Club,
    Kimara Suka

    ReplyDelete
  12. Anonymous15:24

    Naomba ufafanuzi kidogo.mimi habari niliyo nayo huo wimbo wa sikujua kama utabadilika alitunga wilson peter kama kijembe kwa mwanamke tajili alie kua akishi nae na walipotengana na wilison peter kinyonga akuamua kuondoka ndipo akamtungia wimbo huo na ilipofika wakati huyo mwanamke ana mtafuta akamkuta tayali hali yake ni mbaya sana hospital na alishindwa hata kuongea nae akakata roho je ipi ni kweli

    ReplyDelete
  13. Nami ni miongoni mwa wapenzi wa wa muziki qa dansi, wimbo Sikujua kama utabadilika umekuwa ukinigusa sana kila ninapousikia ukipigwa. Kwakweli mtunzi pamoja na kwamba alikuwa anazungumzia kisa cha kweli cha kuondokewa na wanamuziki wake lakini wimbo huu unatufundisha mengi hata kwenye maisha ya kawaida. Tuendelee kushikiana kuweka habri nyingi kadri tuwezavyo kuhusu muziki wa dansi maana ni chakula na burudani kwa qengi. Asante sana John Kitime kwa kuwa mstari wa mbele katika simulizi za muziki wa dansi. Mungu akubariki sana na wengine tutafuata nyayo zako.

    ReplyDelete
  14. Nami ni miongoni mwa wapenzi wa wa muziki qa dansi, wimbo Sikujua kama utabadilika umekuwa ukinigusa sana kila ninapousikia ukipigwa. Kwakweli mtunzi pamoja na kwamba alikuwa anazungumzia kisa cha kweli cha kuondokewa na wanamuziki wake lakini wimbo huu unatufundisha mengi hata kwenye maisha ya kawaida. Tuendelee kushikiana kuweka habri nyingi kadri tuwezavyo kuhusu muziki wa dansi maana ni chakula na burudani kwa qengi. Asante sana John Kitime kwa kuwa mstari wa mbele katika simulizi za muziki wa dansi. Mungu akubariki sana na wengine tutafuata nyayo zako.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...