Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Saturday, September 11, 2010

Maneno UvurugeManeno Uvuruge ni moja ya wanamuziki waliotoka katika familia ya wanamuziki ya ukoo wa Uvuruge. Kaka zake Jumanne, Stamili, na Huluka ni kati ya wapiga magitaa walioheshimika sana katika jamii ya wanamuziki wa bendi Tanzania.

Jumanne Uvuruge ambae alikuwa mkubwa wa akina Uvuruge wote, ndie aliyetunga kibao maarufu cha Georgina, kilichopigwa na Safari Trippers na kuimbwa na Marijani Rajabu. Siku zake za mwisho za maisha Jumanne alikuwa anajishughulisha na kupata riziki yake kwa kuzunguka katika mabaa mbalimbali na gitaa na kupiga maombi mbalimbali ya wanywaji, na kisha kuhama na kuelekea baa nyingine. Hayakuwa maisha rahisi.

Maneno Uvuruge hana kumbukumbu ya jinsi gani Jumanne alijifunza gitaa, lakini anajuwa kuwa Stamili alifundishwa na Jumanne. Anakumbuka zaidi jinsi Huluka alivyojifunza kwani ndie alikuwa kaka yake waliefuatana kuzaliwa. Huluka alijifunza gitaa kwa kuanza kuchonga gitaa lake mwenyewe, aliiba mishipi ya kuvulia ya baba yake na ndio zikawa nyuzi za gitaa lake, siku babake alipogundua wizi huo alivunja vunja gitaa na kumkataza asiguse mishipi yake tena, lakini akamwelekeza inakonunuliwa, Huluka alitafuta pesa na kwenda kununua mishipi na kuendelea na gitaa lake la kopo. Wakati huo Huluka alikuwa anasoma, naye Maneno akaanza hamu ya kutaka kujua kupiga gitaa akawa anaiba gitaa la kaka yake kila alipoenda shule, ilikuwa ni ugomvi kila alipokata nyuzi kwani alikuwa bado anajifunza. Jumanne na Stamili wakaanza rasmi kumfundisha gitaa Huluka nae akalijua vizuri sana. Si muda mrefu baadae nae akaanza rasmi kumfundisha mdogo wake. Maneno anasema wimbo wa kwanza kakake kumfundisha ni ile rhythm ya wimbo Novelle Geneation wa Orchestra Lipualipua, wimbo huu ulikuwa ni kipimo muhimu kwa wapiga rythm enzi hizo. Freddy Benjamin ndie aliyemshauri kujiunga na Bendi. Alimkaribisha UDA Jazz ambako alikuwa akiimbia na pamoja na kuweza kupiga gitaa alifanyiwa mizengwe na mpiga rhythm aliyekuweko na ambae pia alikuwa katibu wa bendi. Freddy alimuombea kazi Super Rainbow iliyokuwa na makao yake makuu pale Sunlight Bar Mwananyamala B. Na hapo akakutana na wanamuziki kama Hatibu Iteytey, Nuzi Ndoli, Rocky, Mzee Bebe, Akina Eddy Sheggy walikuwa bado hawajajiunga na bendi hii wakati huo.(Picha ya juu akiwa na Mohamed Shaweji, ya chini akiwa na Mawazo Hunja)

17 comments:

Anonymous said...

Kitime umemsahau Khalfan Uvuruge katika list yako. Huyu namkumbuka sana jinsi alivyocharaza solo katika kibao 'Zenaba' cha Bima Lee.

Anonymous said...

namkumbuka Nuzi ndoli wakati akiwa nairobi miaka ya 80 alikuja kilimanjaro na mke wake na sanduku kubwaaa la nguo zao na wakapokewa na mzee makassy wakati huo wakiwa moshi kwenye ziara ambayo siku hiyo remmy alipigana na Nuzi. Nuzi nilimuona akiimba clasic ila sijui kama ndio alijiunga na makassy ama vipi kabla ya kuja na kuingia rain bow. Inasemeka alikuwa jasusi wa mobutu japo hakuna uthibitisho.

Kitime J said...

Khalfani na Stamili ni mtu mmoja. Asante kwa kukumbusha hilo

Kisondella, A.A said...

Mzee Kitime kuna huyu Bwana mdogo Fadhili Uvuruge, alipiga muda mrefu Sikinde (alikuwa anapiga gita la rithim vizuri sana)sambamba na nduguye Huruka Uvuruge,Fadhili alipata uzito kidodgo kutokana maisha yake binafsi (???), kinidhamu yalikuwa yanamsumbua sana ndani ya Sikinde.

Huyu si mmoja ya Uvuruge Family??, japokuwa kuna mtu alining'ata sikio kuwa si Uvuruge Familiy as such bali alitumia jina la Uvuruge kuvuta attention ya wapenzi, bali ukweli halisi ni binamu ya akina Uvuruge

Anonymous said...

Maneno ni hodari sana......namkumbuka sana kwa rythm yake kwenye wimbo wa Msondo.......'mwana mkiwa'.........kuna vipande vya kufa mtu nadhani wimbo ule ulimpandisha sana Maneno.

emu-three said...

Aisee, sisi wengine tunapenda kusikia wimbo na kuishia kusema wimbo huu mzuri nimeupenda, lakini ni nani na nani waliouwezesha kupendeka kwa wimbo huo hatutaki kujua. Ahsante sana ndugu yetu Kitine kwa kutupa hili na blog yako inatupa mambo ambayo wengi tulikuwa tukijiuliza...hivi yule alikuwa nani?

Kitime J said...

Kisondela... Marehemu Fadhili alikuwa mtoto wa mjomba wa hawa akina Uvuruge, akina Uvuruge wanaamini kuwa muziki kwao ulitoka kwa babu yao aliyemzaa mama yao kwani alikuwa akipiga ngoma pia na zeze la Kizaramo, mama yao pia alikuwa akipiga aina ya zeze linalobanwa kwa mdomo akawa akilipiga huku dada zake wakiimba. Kwa maana hiyo hata wao waliona kipaji cha Fadhili kilikuwa ni kutokana na urithi huo.

Anonymous said...

Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati Maneno Uvuruge alivyokuwa akituvuruga mashabiki wa Msondo pale Amana Social Hall kwa umahiri wake wa kukung'uta solo na rhythm. Msondo ya enzi hizo iliyowajumuisha akina Moshi William (RIP), Hassan Bichuka, Maalim Gurumo, Athumani Momba (RIP), Uvuruge, Said Mabera na Abdi Ridhiwani ilikuwa ni balaa. Jamaa namkubali. Ana kipaji. Hivi kwa sasa yuko bendi gani?

Anonymous said...

Ningependa mdau emu-three aelewe kwamba si vibaya kujua nani alifanya nini kwa sababu kuna ala za muziki ambazo zimekun`gutwa isivyo kawaida,sauti 1-3 zimepangiliwa kiaina yake.Mimi ni mmoja wa walio wengi ambao ningependa kujua nani alifanya nini,haswa nyimbo za kizazi cha zamani,kwa hiyo hii blog inaweza kukukera sana, kwa sababu humu atachambuliwa mwanamuziki mmoja mmoja kwa mchango wake katika fani ya muziki.Ni huu mziki wa kizazi kipya ambao hakuna anayejali nani kapiga chombo gani kwa sababu wamejipanga upande wa biashara zaidi ya burudani. Mwisho namuomba Kitime, au mdau anayejua,ile solo na rythm katika nyimbo ya Zahir Ali Zorro,photo album zilipigwa na kina nani?

Kisondella, A.A said...

Mzee Kitime shukurani pia kuni-update; sikujua kuwa Fadhili Uvuruge alifariki. Kwa kweli zisipofanyika juhudi za makusudi wanamuziki na wasanii kujifunza upigaji wa vyombo vya muziki, tutakuwa tunaua kabisa muziki wetu wa kitanzania.

Proffessional music si ile ya kuimba halafu unasindikizwa na recorded beats. Dunia ya leo mtu anatoa pesa yake kuona muziki ambapo kama muziki una ala ya saxphone, basi mtu angependa kuona saxphone inapigwa na mtu, vivyo hivyo kwa vyombo vingine kama trumpets, tumba, drums, n.k. Hii music computer techonology isitudanganye sana. Wenzetu nje ndio wanatumia music computer techonology, lakini mkazo mkubwa ni kujifunza vyombo vya muziki.

Wasiwasi wangu ni pale ninapoona wanamuziki wazuri, ambao bidii yao katika kupiga ala za muziki ilijidhihiri wanapofariki hakuna replacement of the same

Kisondella - From Mafinga - Iringa

Anonymous said...

Namuunga mkono Kisondella,muziki unahitaji full squad kuanzia sauti mpaka vyombo. Hata kwenye concert kuna muda anaachiwa mmoja mmoja afanye vitu vyake,kuanzia magitaa,saxaphone,trumpet,drums,mpaka tumba!!!! Hiyo ni burudani,lakini huu mziki sasa unaelekea pabaya.Nikiwa kama mpenzi wa muzuki wa kizazi cha zamani,ningependa kusikia tofauti angalau si chini ya vitano vikipigwa live na binadamu. Sasa brother John,ukiwa ni mmoja wa wakongwe wa muziki, mna mpango gani wa kuufufua muziki wa tanzania? Nimeshaiona show yako na vijana jazz pale vijana hostel ukaimba ile nyimbo ya Nyongise,safi sana ina ladha ya carribean, unajua tena soca muzic, kwa hiyo nina imani mtafanikiwa, kusanya wote hao, kuanzia kina Bitchuka,Mabera,Kalala,Dede,Zahir mpaka kina Juma Ubao kaeni chini muangalie mtafanya nini,la sivyo baada ya nyinyi ndio hakuna kitu!!!

Kisondella, A.A said...

Wenzetu wazaire wamekuwa na utamaduni wa kufanya concert ambazo zimekuwa zikihusisha vikundi mbali mbali. Hivi karibuni kulifanyika onyesho kubwa ambalo waliliita 50th Celebaration. Likiwakutanisha wanamuziki wakongwe ambalo waliwahi kupiga na Marehemu Lwambo Makiadi "Franco" na bendi ya TP OK Jazz, kwa nyakati tofauti, ulikuwa wakati mzuri sana wa wanamuziki kubalishana mawazo nakukumbushia enzi zao. Wapo wale ambao wapo Ulaya na wanafanya kazi zao kule, wapo wale wapo nyumbani (DRC), aidha wamestaafu muziki au wanapiga muziki wa nyumbani

Hii imenikumbusha tamasha la wanamuziki wakongwe ambalo walilifanya hivi karibuni hapa Tanzania. Hii safi sana. Huu utamaduni ni vyema ukaendelezwa usiwe wa "kubip". niliufuatilia kwa karibu japokuwa nilikosa ushiriki. Nafikiri vijana wa leo watakuwa walijifunza mengi sana kutoka kwenye concert ile na hasa matumizi halisia ya vyombo. Kwa siye tuliopo mikoani tulikoa kitu fulani muhimu sana.

Hivi Mzee Kitime kulikuwa na production ya DVD kwenye ile concert ili tuunge mkono ile concert na kuchangia kwa namna fulani kwa kununua DVD au VCD.

Njia mojawapo ya kuwanyenyua wasanii/wanamuziki ni kununua kazi zao halisia

Kisondella - From Mafinga (Iringa)

Kitime J said...

Bahati mbaya watu wanao controll music industry Tanzania c wale waliopitia phase mbalimbali za muziki hivyo hawana imani kuwa kuna chochote kina maana katika muziki wa zamani, wakitaka kushiriki katika muziki wa zamani hutoa masharti kuwa ni lazima waubadili ndio watatoa support

Anonymous said...

Kitime
Sii kwamba wanao endesha muziki ni vijana wasio na upeo wala ubunifu wa kufuatilia mambo mbali mbali ya nyuma,ni wavivu wa kufukiria mambo mapya yenye kuleta maana na yatakayo dumu kwa muendelezo wa kizazi chao.
Mbaya zaidi hawajitambui so ni ngumu sana kuweza kuwasaidia.

Anonymous said...

Lakini tusiwalaumu saana hawa vijana, kwa sababu,chukulia kule kwenye industry ya muziki ambayo ni Marekani,wana matatizo hayo hayo.Ndio,vijana wanatoa ngoma nzuri,ambazo zinaisha utamu kwa muda mfupi sana,tofauti ni kuwa wao wanatengeneza noti!!! Kama wakizungumzia mziki utasikia kuanzia kina THE TEMPTETIONS,OTIS,FOUR TOPS,THE COMMODORES,ARETHA,MARVIN GAYE,STEVIE WONDER,LUTHER VANDROSS,TINA,WHITNEY ETC...hao watu walikuwa wanakaa chini na kutoa vitu si vya kawaida, mnakumbuka Nightshift? Pappa was? Sexual healing? Have you seen her? Listi ni ndefu,na zinawafanya watu kama Usher na Chriss Brown kuonekana matapeli tu!! Pia msifikiri nilimsahau King of Pop, the man himself, MJ RIP Huyu ndiye aliyewafungulia milango ma artist wote hususan weusi katika MTV.

elvan stambuli said...

TUPE HABARI YA DAVID MUSA WA TRIPPERS ALIKUWA MPIGA SOLO

Twaha Mtumbi said...

Si mchezo tunaishiwa

Adbox