Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Monday, May 3, 2010

Wanamuziki ndugu


Katika kila nyakati kunatokea ndugu ambao ni wanamuziki. Pengine hii inatokea kwa kuwa mtu anakulia katika mazingira ya nduguze kupiga muziki hivyo inakuwa rahisi kwake kuwa mwanamuziki, na nduguze wakiwa wanamuziki inamrahisishia njia, lakini hilo si jibu sahihi kwa kweli kuna mengi zaidi ya hilo. Katika picha hii ni wanamuziki ambao ukoo wao wako wanamuziki wengi na hii imekuwa inaendelea kwa vizazi vitatu sasa jina la ukoo huu kila mara likiwemo katika historia ya muziki. Ni akina nani hawa?

34 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kwa kweli nitahisi tuuu. Kwa kuwa nimeona gitaa, ntasema ni kina UVURUGE.
Just guessing

John Mwakitime said...

Hapana , kumbuka nimesema katika ukoo huu kumekuwa na historia ya muziki ambayo imekuwa katika kizazi zaidi ya kimoja

Anonymous said...

Me too, just guessing (they look too young): Kina Mhuto???

John Mwakitime said...

Picha ya miaka ya mwanzo mwa 70s

Anonymous said...

Kina Issa Juma wale ndugu ambao walikuwa Les Wanyika?

Anonymous said...

Lakini siyo Marijan Rajab na kaka zake hawa?

Anonymous said...

Balozi John,
hawa nimeshindwa kabisa kuwajuwa ingawaje nilikuwa mmojawapo wa wapenda mziki tokea mwishoni 69 mpaka mwishoni 70`s hawa vijana wanaonekana walikuwa wadogo sana,
tupe mwelekeo kidogo labda utasaidia,walikuwa wanaishi wapi tutajaribu kupata mwanzo wa kuwakumbuka hawa siyo kabisa kina mhuto,sabuni au barkeys.
Mickey Jones
Denmark

Mzee wa Changamoto said...

Nasubiri "kutoa mji". Hahahahaaaaaaaaaaaaa

John Mwakitime said...

Bado sitaki mji clues zote nimezitoa, ukoo wao washiriki wa music wameingia generation ya 3

Anonymous said...

Huu ni ukoo wa mwinshehe na hiyo picha ni yeye hapo

Anonymous said...

ukoo wa kina Mze Zahir Ally Zoro

John Mwakitime said...

Ngoja nitoe clue nyingine. Group hii ilikuwa inaitwa The Gypsies, ilitokana na kaka zao kuwa na bendi iliyoitwa Les Heroes. Mpigaji mmoja wa Les Heroes bado anapiga na ana mwanae ni mwana muziki

Anonymous said...

Dk John,

Umenichanganya kabisa nawakumbuka Les Heroes nawakumbuka The Gypsies, lakini kila nikizungurusha ubongo kupata kumbukumbu nazungurusha kichwa kizima bila ya kupata jibu.
Dares salaam upande wa magomeni kulikuwa na The Comets na kina mhuto`s, Les Heroes na Mohamed Makwinyo,Gabriel Sabuni,Gershom Chihota,Abby Sykes upanga kulikuwepo na sasa mhs. Mohamed Maharage(James Brown)willy Lukuta na The Groove Makkers,kulikuwepo Barkeys,changombe kulikuwepo na Mussa Gordon,Shabani Marijani na Les Trippers,Temeke kulikuwepo na Patric Balisidya na Afro 70,James, Kassim na The Sun Burst sasa hawa vijana jipukizi nakumbuka walipiga ma-gigi wakati wa mapumziko sehemu nyingi nilizokuwepo kama Splendid hotel,Karmjee Hall na secondary schools zote kama St Josephs sasa forodhani...nimekwama siwakumbuki, nimetuma maombi ya msaada kwa mshikaji wangu Freddy Macha wa 70`s hajanijibu nafikiri hata yeye kakwama hawakumbuki..
Nafuatilizia lazima zawadi iwepo kwa mwenye kumbukumbu ya vijana.

Mickey Jones
Denmark

John Mwakitime said...

Baba yao aliishi Temeke

Anonymous said...

ukoo wa sykes,kwa sasa anayetamba ni dully sykes(abdul)

Anonymous said...

Hii ya safari hii ni chemsha bongo. Mimi late 60's na early 70's nilikuwa nakwenda boogie na nilibahatika kufahamiana na wanamuziki wengi, k.m. kina Sabuni, marehemu Adam Kingui, marehemu Balisidya, Mick Jagger, Salim, Sunbursts, etc, na the Heroes. Cha ajabu hii picha doesn't ring a bell in my mind. Au huu ndio uzee??? Hapa ni case ya kuomba "msaada tutani". Eddy.

Anonymous said...

Kama asemavyo mchangiaji kuwa ni ukoo wa Sykes ambaye mtoto wake ni Dully Sykes, basi atakuwa Abby sykes wa Les Heroes akiwa pamoja na Mohamed Makwinyo,Gabriel Sabuni,Gershom Chihota na Choggy Sly rafiki au kundi langu la ujana 70`s.
Abby Sykes hakuwa mkaaji wa Temeke zaidi ya kuwatembelea jamaa na marafiki zake kama mmojawapo wakati huo alikuwepo jirani yangu marehemu Abushiri Kilungo,kina Sykes waliishi mitaa Ilala karibu na John Rupia,wakati ule kulikuwepo na The Rifters/Sparks mwimbaji alikuwa Ringo Star mpiga drums maarufu jina nikikumbuka alikuwa Mbaraka,jirani kulikuwepo kijana mwimbaji chipukizi wa The Comets akiitwa Huruka (HULKY) kina Sykes wengine walikuwepo upanga na magomeni.
Nimepoteza kumbukumbu,tuendelee kuwasikiliza wenye kumbukumbu za hawa vijana

Mickey jones

Anonymous said...

Brother John
Huyu ni Omari Sykes, mdogo wake Adam na Ebby Sykes, Ebby ni baba yake Dully Sykes
Balozi Maharage Juma

Anonymous said...

Hi Mickey Jones yaani umemsahau marehemu Omar Sykes? Ndiye huyo pichani!Habari za Denmark?
Balozi Mohamed Maharage Juma, tuwasiliane kwnye mabeans@gmail.com

John Mwakitime said...

Mheshmiwa Balozi welcome. niseme nini? I got soul and I am super bad.

Anonymous said...

Ahsante brother John unanikumbusha mbali sana nategemea kuwepo home July nasikia Njnje inatayarisha usiku wa vijana wa zamani tupande jukwaani!
Mohamed Maharage Juma

Anonymous said...

Karibu balozi ukumbini kwa kaka John Mwakitime,pongezi zote kwa kuturudisha miaka iliyopita.

Balozi nimeshapata habari hizo za July lazima niwepo nyumbani sitokosekana ratiba hiyo ya usiku wa vijana.

Nilipigiwa simu na waziri Mahanga wakiwa pamoja na balozi Cisco,pia nilipata bahati mara mbili kukutana na mhs Rose Migiro wote niliwaomba wapitishe salaam zangu kwako haswa wakati wa kifo cha marehemu mtoto.ahsante kwa kumbu kumbu za mtoto wetu Omary Sykes

Mickey Jones

Anonymous said...

Ahsante Mh. M.M.Juma. Kweli huyo ni Marehemu Omari Sykes. Hii picha imenikumbusha mbali na kunipa huzuni, lakini kazi ya Muumba haina makosa. Tunamwomba Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peoni. Amin.
Eddy.

Anonymous said...

Yep, Balozi Maharage is right, huyo ni Omari Sykes(RIP) was a good friend of my brother Andrew(RIP). Good to see you are in circulation. I guess you could consider me a groopie of the "Groove Makers" back then I attended all theeir "Boogies" As far as I am concerned together with my good friend and classmate Herbert Lukindo(RIP), the Jengo brothers, Sverne Kibira, you guys were the best

Sammy Mnkande

Anonymous said...

Very sad to hear that Herbert Lukindo has passed away. May he rest in peace. Amin.

Anonymous said...

Very sad to hear that Herbert Lukindo has passed away. May he rest in peace. Amin.

Anonymous said...

Hi Sammy..
kweli umenikumbusha mbali,ilikuwa hakuna "gigi/buggy" watakalopiga The Groove Makkers ukawakosa kina Jengo brothers,kibira,Anne Mkande,Makame wa Upanga na R.I.P Herbert Lukindo ambaye alikuwa na uhusiano na Willy Lukuta mpiga bass....
Mickey Jones

Anonymous said...

R.I.P Herbert Lukindo
yes...very sad,sote tulishikwa na majonzi makubwa kutoweka kwa rafiki Herbert Lukindo alikuwa "Gentle & Cool" mara ya mwisho mimi kumuona aliporudi toka China,tulienda kwake na Willy Lukuta wa The Groove Makkers.
Mickey Jones

Anonymous said...

Hi Sammy
Nice to know you are in circulation too, pia tumkumbuke rafiki yetu mwingine marehemu Hamis Mapezi mlikua naye Saint Josephs alikuwa hakosi Buggy!
MMJ

Anonymous said...

mwakitime tunashukuru sana kwa kazi yako nzuri kwa kutuletea habari ya wanamuziki wetu wa zamani na sisi tulioko nje ya nchi tunafaidi sana ubarikiwe sana nilikuwa naomba kama itawezekana utuletee habari ya wale wanamuziki wameamiga arusha long time walikuwa wanajiita kwa jina lombelombe baadhi ya majina yao siwakumbuki wote ila kuna baadhi ya majina msimbe,athumani alikuwa mpiga gitaa lkn marehemu kwa sasa

John Mwakitime said...

Nawakumbuka Orchestra Lombelombe, walikuwa ni kundi lililo break away toka kwa Mbaraka, nitatafuta data zaidi nikuletee, najua nina cutting moja ya habari zao ikiwa na picha ya Gumbo ambae alikuwa mpiga bass wao, ntaipost hapa..

Anonymous said...

nitashuku sana ukiipost utupostie picha nyinginyingi tu. HAVE A GOOD NIGHT

Anonymous said...

Ohhhh my God !!!!
Hamis Mapezi hatunaye tena....? sikuwa na habari za kutoweka kwake,ametutoka mapema mno,poleni ndugu na marafiki wote wa Hamis.
balozi MMJ ahsante kwa taarifa
Mickey Jones

chesi.com said...


...is Anne Mnkande any relation to Lucy Mnkande my classmate at Chang'ombe P/s in 1972/73?

Adbox