Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Monday, May 17, 2010

Orchestra Lombelombe

Niliahidi kuwa nitaweka kipande cha gazeti chenye habari ya Orchestra Lombelombe, bendi ambayo wanamuziki wake walitoka katika bendi ya Morogoro Jazz. Bendi hii ilikuja baadae kuitwa Kurugenzi Jazz baada ya kuwa chini ya Ukurugenzi wa Mkoa wa Arusha, pichani ni Gumbo ambae alikuwa mpiga Bass, miaka ya sabini alihamia Iringa ambako alikuwa mfanya biashara.

7 comments:

Anonymous said...

nashukuru sana kwa kutuwekea habari ya lombelombe japo ni kipande kidogo lakini nakupenda kwakuwa umeonyesha moyo ya kwamba unawasikiliza na kuwajali washabiki wako wanata kitu gani natumaini utaendelea kutafuta habari zaidi yahiyo band napenda sana nijue taarifa zao kwa sasa asante sana ubarikiwe na kazi yako nzuri kitu kingine naomba utuwekee ule wimbo jojina

Anonymous said...

Uninikumbusha mbali sanaa!!!!!,-ila sina hakika kama kiongozi wa lombelombe alikuwa ni Razaro Bonzo,-ila kumbukumbu zangu najua yaya ndie alikuwa kiongozi wa Kurugenzi jazz band,-akiwa na wadogo zake mmojawapo ni Suli Bonzo,-chukufurahisha huyu bwa Bonzo bado anaendelea na libeneke la muziki kama kawa.

Anonymous said...

Balozi ahsante sana kwa kutuwekea almasi hii pichani. Je una picha za Western, Uda, Super Bomboka, Sikinde enzi hizooooooo wakati wanaanza, msondo na bendi zingine za zamani ili tuwaone wanamuziki walikotoka. Ahsante sana.

Anonymous said...

Nikupongeze sana bwana John Kitime kwa kuanzisha uwanja huu ambao kwa kiasi kikubwa unasaidia kuturudisha nyuuma sisi a enzi hizo, nina mambo kadhaa ambayo ningependa kuyatoa kama ushauri/maswali kwako.
1. Kuna mwanamuziki mmoja mtunzi wa ule wimbo wa kipindi cha wagonjwa (Mzee Kungubaya) niliwahi kumuona akihojiwa nyumbani kwake na kituo cha channel 10,kwa kweli iliniuma sana maisha anyoishi na habari kwamba RTD waliacha kupiga wimbo wake baada ya yeye kudai alipwe mrahaba, sasa sijui wewe binafsi na wanamuziki wengine wenye upeo mkubwa wa mambo mulifanya/munafanya kitu gani kuwasaidia watu kama hawa japo wapate sehemu ya kuridhisha ya kulala?
2.Siku hizi kuna redio nyingi zina watu wanaochambua muziki wa zamani kwa kiasi kinachoridhisha sijui, je una link oyote na hawa watu? kama ni ndiyo kwanini usiwe unatuwekea historia za wanamuziki maarufu wa enzi hizo mfano wiki iliyopita nilisikia historia ya marehemu salum abdallah redio uhuru kwa kweli naamini kama ungeiweka humu ingewatoa watu wengi machozi na kutoa fundisho kubwa la mtu kutokukata tamaa katika kutafuta.
3.Sasa hivi ni wazi kuwa muziki wetu wa dansi niuite wa asili mliokuwa mkipiga nyie ambao sa sa umebaki kwa msondo,sikinde,vijana kidogo unapotea, vijana hawaonyeshi hamu ya kuundeleza inasikitisha kuona kuwa siku hizi taarabu/rusha roho iko juu. Swali langu wewe na wengine ambao bado mpo mna mkakati gani wa kuhakikisha kwamba huu muziki unarudi kwenye chati na kutoa burudani kama ilivyokuwa huko nyuma ili miaka thelathini ijayo watakaokuwepo wawe na simulizi kama hizi unazotuwekea hapa. Niliwahi kukuona wakati fulani ukiwa jaji kwenye bss,juzi tena nimemwona mzee kijana zorro nae ni jaji kwenye sijui serebuka binafsi sielewi kwanini nyie msianzishe kiti kama hiki lakini kwa minaajili ya kupata chipukizikwenye muziki wa dansi upande wa vyombo, uimbaji n.k
4.Ivi ni kitu kinawafanya nyie watunzi mahiri wa wakati huo ambao bado mko kwenye fani mshindwe kutoa tungo kama zile za wakati ule, najua wapo wakina mzee zahir,wewe shem karenga,salim zahoro,mapili,gurumo,bichuka,hamza kalala,mafumu na wengineo kimetokea nini au ndo vyakula vya vyetu vya sasa vinapunguza uwezo wa kufikiri?

Anonymous said...

Ndugu yangu ANONYMOUS 08:31, Muziki wa Dansi bado upo ila Tanzania siku hizi Vyombo vya Habari havitangazi Muziki halisi wa Tanzania,toka jina Dj(Disco Jocker) imeingia Bongo wanajifanya kuiga Wamarekani Weusi,basi promotion ya Hip Hop aka Bongo Fleva ndo inapewa kipaumbele katika Medias za Tanzania.

Muziki wa Dansi TZ hauna Recording Company,haupigwi katika Radios,Tv's ao Magazeti hautangazwi... basi Muziki huo una KUFA,Ndugu yangu ANONY 08:31 hatunabudi kuwalaumu WANAMZIKI wa zamani, wamefungua njia ila Kizazi kipya hakitaki kuwa enzi wa zamani Vijana wanataka SHOTKAT na ndio sababu Muziki wa Tanzania hauna ramani katika Soko la Dunia.

Sisi Wakereketwa wa Muziki wa Dansi Tanzania tulio katika Nchi za Teknolojia(Euro,USA,Asia...) ndo twaweza kuokowa Muziki halisi wa Tanzania kwaku wasaidia Wanamziki kuja huku na kurekodi katika Studios za huku,Ahsanteni.

Perez said...

Wangu Kurugenzi Jazz unanikumbusha wimbo wao mmoja nikiupenda sana.

"...Matumaini yetu waFrika siasa ya Ujamaa, Ohh..,

Ujamaa ni mzuri wenye kuleta usawaa...,
Ujamaa hautakufa Tanzania twaulinda...,

Tutaendeleea hatutarudi nyuuma..,

Mawazo sahau, ujamaa hautakufaaa,

...(ujamaa ooh, mama ho ho)...

Fungeni vibwebwe tujenge ujamaaa..."

We acha tu

Anonymous said...

Unanikumbusha sana pale Chinese restaurant- Arusha, opposite na Library....adjacent na mto Naura......ndio ilikuwa makao makuu ya Kurugenzi jazz...majina kama Gerald Nangati, Greygory Stephen, Chale Bonzo, Mohamed Msimbe, Maneno, John Masai, Ali Mtumwa, Chox na mzee Lazaro Bonzo...hii ilikuwa miaka ya 1980-87.
Mirindimo ya Super Volcano ulikuwa unaisikia kwa karibu sana...hasa gitaa la hawaii la Gerald...those will ever remain in my memory...

Adbox